Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
Ungekuwa unaweza ungeshayafanya.
Wachambuzi wa kwenye makochi ya kujipinda kinyume.
Maili elfu tano toka eneo la tukio, waliko hawaruhusiwi kugombea, maana hawajulikani wametokea dunia gani, ilibidi wadanganye kwamba kwao wamefukuzwa ili wapewa kipande cha uwepo na namba ya manamba.
Mimi "useful idiot" na nyinyi wenye akili msio na faida, yupi bora?...Au na wewe ni USEFUL IDIOT?
Mimi "useful idiot" na nyinyi wenye akili msio na faida, yupi bora?
Anachambua halafu iweje, akafanye anayochambua. Achambue amekaa kwenye jamvi, anachambua karanga? Nimeifanyia nini Tanzania, naijenga Tanzania kwa zaidi ya maoni na chambuzi tu. Wanasema maoni ni kama matundu ya nyuma, kila mtu ana lake. Tenda. Unachambua uko Udachi?
Ningekuwa mgombea ningehamasisha... ningehakikisha... ningeimarisha...ninge ninge... rudi ugombee!
Hao wametoka mezani wakenda fanya tafiti, wamekusunya hela wamechapa vitabu, wamehariri. We unasema "ningekuwa mgombea ningehamasisha, ningehakikisha, ningeimarisha..." umekaa kwenye kiti cha kubinjuka nyuma unachambua na kuchakachua uchaguzi. Tena kura hupigi, uko Kyubeek na Helinski mwisho wa dunia huko jua limezamia likapotea moja kwa moja usiku mwaka mzima. Utatusaidia uongozi kweli wewe? Ningekuwa mgombea? Gombea....Kwa mtazamo wako basi hata vitabu vya ELIMU wewe huwezi kuvisoma ukitaka kuwaona hao wasomi wenyewe wamewahi kufanya nini na sio kukaa mezani ..
Mimi "useful idiot" na nyinyi wenye akili msio na faida, yupi bora?
Anachambua halafu iweje, akafanye anayochambua. Achambue amekaa kwenye jamvi, anachambua karanga? Nimeifanyia nini Tanzania, naijenga Tanzania kwa zaidi ya maoni na chambuzi tu. Wanasema maoni ni kama matundu ya nyuma, kila mtu ana lake. Tenda. Unachambua uko Udachi?
Ningekuwa mgombea ningehamasisha... ningehakikisha... ningeimarisha...ninge ninge... rudi ugombee!
Unamuuliza atafanya nini kwani kakwambia anagombea?Je unaweza kuja na detail utafanya nini na kufanya mabadiliko gani.
Je Unaweza kuja na detail japo eneo/sekta moja ungefanya nini na kufanya mabadiliko gain?
Huyu ni mwandishi tu, anatuma makala kwa barua pepe hapa na pale, mchambuzi, anachakachua fikra, matendo sifuri yenye masikio. Yuko kwenye tarakilishi anasema angegombea.
Kama unajua cha kufanya ukigombea, gombea
Unamuuliza atafanya nini kwani kakwambia anagombea?
Mbona unamwekea maneno mdomoni? Katushirikisha kwenye njozi zake za uchambuzi tu. Angekuwa, angeligombea, angetaka, angekuwepo. Hayupo! Huyu ni mwandishi tu, anatuma makala kwa barua pepe hapa na pale, mchambuzi, anachakachua fikra, matendo sifuri yenye masikio. Yuko kwenye tarakilishi anasema angegombea. Kama unajua cha kufanya ukigombea, gombea!
Umenena vema mkuu...wako wengi kweli humu....wao ndo wakubwa wa kusema, mabingwa wa kukosoa..mahiri wa kuandika...na wakali mno wakikosolewa...wengi sana..na ninawajua wengi tu...wakimaliza kubeba mabox, huku wakiwa hoi bin taaban, wanakamata computer nakuanza kuandika kila wanachoona kinafaa...ukimkosoa tu, lahaulaaa! utaona tu wakati mwingine wanakuja na vijineno vyao uchwara vya kiingereza visivyo na kichwa wala miguu, wanavicopy toka kwenye internet au kuvikariri toka kwenye movie...mara useful idiot,,,lakini wapi..hawajui what is actually happening on the ground....hayo ya Kishoka kila mwanasiasa hapa tz anayasema, tena mazuri zaidi..endeleeni na lile la dual citizenship maana kidogo ndo mnalielewa kwani lazungumzwa zaidi mlipo kuliko huku, huku ni makubwa zaidi
... changanya na zako!