Duh hii imekaa kushoto vile, huyu msela ana makosa mawili, kosa lake la kwanza ni kumpa mke wa mtu ndoo ya kuogea na kosa la pili ni kusema ingia uchukue.
Kwenye kosa la pili alitakiwa atoe ndoo yenye chupi nje ili yule mke wa mtu aichukue mwenyewe na kuondoka zake.
Nikirudi kwenye mada husika, huyu mke inabidi atoe maelezo ya kina sana juu huo mkasa, haiwezekani uishie hivyo tu kwa maelezo mafupi tu.
Hainingii akilini kwa mwanamke makini kuazima hadi ndoo ya kuogea, tena kwa msela, hapana,lazima kuna kitu zaidi ama kuna kitu kinatafutwa na hata hiyo chupi itakuwa iliachwa for the purpose.
Hilo ni jaribu kama majaribu mengine, shetani kazini kutafuta na kukusanya wafuasi wengi kadri inavyowezekana.