Kama ni wewe, Utaendelea na mipango ya ndoa?

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,503
6,406
Heri ya mwaka mpya JF??

Wewe ni kijana tayari umekua na umejitosheleza kiasi cha kuhitaji kuwa na mwenza wa maisha (kufunga ndoa). Umempata na procedure zote za awali mmezifanya ikiwamo mahari mmeshatoleana.

Una mdogo wako wa kiume baba mmoja mama mmoja, kamjua mdogo wa kike wa mkeo mtarajiwa nao pia ni ndugu wa baba mmoja mama mmoja kupitia pukushani zenu za maandalizi ya kuwa mwili mmoja! Wakatongozana huko na wakaanza mahusiano, kuja kushtuka wamepeana mimba kabla ya ninyi maharusi watarajiwa!! Ishu imefumuka, bibi harusi mtarajiwa anazimia zimia hovyo baada ya kujua hii ishu na wewe pia umechanganyikiwa halikadhalika familia zote zimepigwa butwaa!!

Mnaonaje hapo? Mipango ya harusi ihamishiwe kwa waliopeana mimba au sisi tuendeleee nayo tu??

Nawasilisha
 
Ninyi endeleeni na harusi yenu, ila hapo dogo kaharibu sana.

SWALI: Wao pia wamekubali kuoana?
 
Sasa hapo kuna shida gani? Kwa maneno mengine ni mnataka kuoa toka kwenye familia moja nao wataolewa kwenye familia moja.
 
hapo mnaweza mkafunga tu ndoa hata wao wakiamua wanaweza maana hakuna undugu kati yako na mdogo wa mke wako
 
Kwenye vitabu vya mapokeo kumeandikwa, "kila mmoja ataubeba mzigo wake". Sijaona cha ajabu cha kuzuia ndoa kufungwa.
 
Hii ilitokeaga somewhere, japo ni tofauti kidogo (kaka wa bwana harusi alimla ma mkwe(mama wa bi harusi)) na maharusi watarajiwa wakiwa na mtoto tayari mipango ya ndoa ilivunjwa
aise kuna watu majasiri
 
Back
Top Bottom