Kama ni kweli,nchi wahisani sitisheni misaada na mikopo kwa Tanzania

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,685
149,894
Kama kweli kuna mpango wa kununua ndege nyingine kwa ajili ya viongozi kama hii tetesi inavyodokeza, wakati bajeti hazitekelezwi viziru,wanafunzi wanakosa mikopo,bajeti ya maji haitekelezwi, watumishi hawaongezewi mishahara,n.k,natoa wito kwa nchi wahisani wasitishe mikopo na misaada yote kwa hii nchi.

Sisi ndio tutakaopata shida lakini ni bora tukapata shida ili akili zitukae sawa next time tuchague viongozi wanaojali wananchi na si hizi anasa.


Haiwezekani tunakopa kila wakati na kuongeza deni la Taifa alafu tunakuwa tuna matumizi ya aina hii.

Ile ndege iliyopo mbona ni nzuri tu(jet stream) na inabeba abiria wengi zaidi.

Kwanini wao hawataki kuumia na dhana ya kubana matumizi kama sisi wengine?

Kwanini mnaanzisha jambo ambalo nyie wenyewe mnashindwa kuwa mfano katika kulitekeza?

This is too much!!!

Kuhusu tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu someni huu uzi kupitia hii link hapa chini ndio mjue kwanini wengine tunapinga mambo haya.

Huu uzi hapa chini una ripoti maalumu kuhusu tatizo la mikopo kama ilivyochapishwa na gazeti la The Citezen la siku ya jana tarehe 15/05/2017.

Kama tumeamua kubana matumuzi,futeni na sitting allowance wa wabunge elekezeni fedha hizo HELSB
 
Hivi wewe kuna kipindi ulishawahi kuliwazia mema taifa lako?? Wewe nafikiri siyo RAIA Wa nchi hii!! Au wewe ni jasusi wamataifa mengine
 
Hivi wewe kuna kipindi ulishawahi kuliwazia mema taifa lako?? Wewe nafikiri siyo RAIA Wa nchi hii!! Au wewe ni jasusi wamataifa mengine
Acha kuwa mpuuzi wewe!Huko vijijini mamawajawazito wanakufa kwa kukosa huduma za uzazi alafu wewe unashabikia ujinga gani?Huu ubinafsi wako ni laana.
 
Nimejitoa kwenye kundi la kufanyia maamuzi tetesi tena za upande mmoja ili nifiche upumbavu wangu.
 
mlifurahi sana tulivyonyimwa hela za MCC lakini CCM na serikali yake imetumia fedha za ndani kuendeleza mradi wa REA.
 
Back
Top Bottom