Kama ni kweli basi System ndo Tatizo


wasiraisishe hivyo kama system inashidwa kufanya analysis ya aina gani ya mtu watu wanaemtaka iko shida na wanaidanganya ccm,oke! Urais wanaweza kumfanya ashinde lkn,je wabunge wao atawaombea kura na je watu watajiuriza amewajuaje maana hakuwai kufanya nao kazi,naiona ccm ikipata anguka la nguvu ndani ya bunge kiasi cha kuwatisha,maana watu watamuona ni mpole hivyo watachangua wabunge wa upinzani wengi ili kubana serikali,
je watafanya kazi ?
Je watakuwa wameisaidia ccm?
Je je wanajua watu wanamtaka rais wa aina gani?
Kazi kwao wajipime
 
Ndugu duniani kote hii ni moja ya kazi kuu ya system. Ni kutengeneza mtu au kutafuta mtu kutokana na maitaji ya wakati husika,kitaifa na kimataifa na hii ni kwa MASLAHI MAPANA YA TAIFA narudia tena MASLAHI MAPANA YA TAIFA. Na maslahi ya taifa ni pamoja na kiusalama na kiuchumi sasa hapo ndo sidhani if walikuwa serious kwa sababu no one is disputing usafi,hekima na weredi wa Jaji Ramadhani ila je ataweza kuisimamia na kuisimamisha hii nchi vizuri kwenye dunia hii ya ushindani na jamii hii ya watanzania iliyoparaganyika kila kona???
 
\
Kwa kifupi kitakuwa kipindi kingine cha kuweka siasa kila mahala,serikali kuyumbishwa na watu na wafanyabiashara kwa sababu aliye juu sio mkali na hana haiba ya userious na kufuatilia mambo kwa ukali, kitakuwa kipindi cha watu kuona hamna lilalofanyika kwa sababu hata mawaziri wanajua aliyewachagua sio mkali na hana haiba ya kuwafuatilia watu kama kuona wamedeliver kwenye standards zinazotakiwa. Kitakuwa kipindi kigine cha uchumi kuyumba kwa kiwango kikubwa sana kwa sababu watu hawatazkuwa tena na hamu na serikali na hawataisikiliza kutokana na kukata tamaa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha hawa watu kutumia uwezo wao wa kiwango cha juu kabisa ili waipe hii nchi raisi atakaekumbukwa na vizazi na vizazi kwa mazuri. Hiki ni kipindi ambacho walitakiwa wakitumie vizuri ili hadi huko mbele nao waje kujisifu na kuona kweli tuliitendea haki Tanzania ya Mungu.
 
Tatizo ni system ikishakuwa na mahaba-weledi hupotea.
 

mkuu hongera kwanza kwa kutoa maelezo ya maana na yenye weledi wa hali ya juu.
Sidhani hata dkk moja kuwa Jaji Ramadhani ndio chaguo la system
hata Mkulu mwenyewe sidhani kama hili ndio chaguo lake
ninachaona hapa huyu Jaji Ramadhani na A. Mahiga wako pale kwa lengo la kumchinjia baharini Laigwani baaaasss! Na ni trik inayofanywa na chama
Chaguo la system kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya uhakika ni kati ya hao uliowataja hapo juu.
Wajanja wa nchi hii walishagutuka siku nyingi kuwa jamaa ndio anaandaliwa kuchukua nchi ndio maana wakamuingiza kwenye zigo la Escrow ili kumchafua
nadhani umenipata mkuu
System yetu iko makini sana sema siasa zinatuharibia
 
There is no way ukaniambia Tanzania tuna system bora kuliko zote wakati mambo madogo yanatushinda...
System ya Tanzania ni ile ya kuwanyamazisha wale wanaikosoa serikali badala ya kuishauri serikali jinsi ya kulinda maslahi yake ndani na nje ya nchi...
Miaka 10 ya Kikwete imedhihirisha kuwa system imeshindwa kuona na kusimamia mambo madogo sana ambayo wananchi wanakutana nayo kila siku...
System ya tanzania imekaa kisiasa sana....
 
Mimi nimependa uelewa wako, big up mkuu.
 
Kinana ametumia mbinu ya kijeshi ijulikanayo " The art of psychological warfare" amewafanya "enemy" wa "dance to the tunes he plays".

Kwa hili nnampa kudos Kinana. Nilijuwa kile kichwa kama boflo hakijawa vile bila sababu na sasa nnaziona sababu.

[h=2]"Victorious warriors win first and then go to war, while defeated warriors go to war first and then seek to win."[/h]
 
System aliyoijenga Nyerere ilikuwa ni bora kwa ajili ya kulinda puppets wa nje wasipenye kwenye kuingilia affairs za nchi yetu, lakini alikuja kupiga fyongo kwa kutoandaa successor wa kuendeleza legacy yake. Ilikuwa mara mia kipindi ile amuachie Mrema kuliko Mkapa ni mtazamo wangu huu kwasababu yaliyotupata sasa ni matunda kwa sehemu kubwa ya kutocheza vyema karata zake mwishoni.
Sasa hivi system aliyoiunda Mwalimu, inatumika kinyume chetu, na kinyume cha matakwa na maslahi ya nchi. Na hapa ndipo kosa la Mwalimu kama binadamu linapotuumiza mpaka leo. Na mwarobaini wa hili hauwezi kupatikana ndani ya chama ambacho usukani wake na system yake inaendeshwa na puppets wa mataifa tajiri ya nje kupitia multinational companies zao mbalimbali ambazo zipo kila kona ya nchi zingine zikiwa zimekamata njia kuu kabisa za uchumi wa nchi. Ili tupone ni lazima tuwaingize wapinzani kushika hatamu za uongozi. Kwisha na si vinginevyo. Japo nao watakuwa na wakati mgumu sana kuiweka sawa system.
 

Kukemea ni mojawapo ya quality ya rais tunayemtaka...huwezi kuchukua hatu au kusimamia utawala bora kama huwezi kukemea...
 
Nakupa pongezi mtoa mada. Ni kweli Jaji Ramadhani sio mtu mbaya na ni mwadilifu mpaka hata watoto wake ako very humble and friendly.

Nachowaza ni kwamba Kikwete na watu wake wanataka kumtia mzee wa watu kwenye matatizo.
Nampa ushauri mzee wa watu ni bora aachane nao huo uraisi.

Sidhani kama ataibadilisha hii nchi kwa upole na fikra alizonazo. Tunahitaji ganster fulani ndani yao ambaye ndie atakayewasaliti wenzake kwamba jamani eeh,mimi nafanya hiv au itakuwa hv.

Mtazamo wangu hapa jaji Ramadhani anaingizwa mkenge. Nchi ina matatizo lukuki,mafarakano kati ya wananchi na wananchi,wananchi na serikali,vyombo ya usalama, nk bila kusahau umaskini uliozidi toka 2005.

Ushauri wangu kwa Mzee Ramadhani fikiria sana hili jambo. Hawa watu sio watu unaotaka kudeal nao.
 

Na hapa ndipo ccm walipotuharibia nchi...kuunganisha nafasi ya raisi wa nchi na mwenyekiti wa chama chao.hiyo ni sawa na mkono wako wa kushoto ukivunja glass eti uuambie mkono wako wa kulia uupatie adhabu mkono wa kushoto...uongozi wa serikali unatakiwa kuwa independent...pumba.fu sisiemu wametuharibia nchi...
 

Mimi naona uko irrelevant na substance ya huu uzi. Ukimwongelea kinana unaongelea system ya uchafu uliotukuka.
Sasa sijui kinana hapa amefanya effects gani za ajabu maana ndani ya CCM hakuna mwadilifu au mwenye nia ya dhati na hii nchi.
 
Mimi naona uko irrelevant na substance ya huu uzi. Ukimwongelea kinana unaongelea system ya uchafu uliotukuka.
Sasa sijui kinana hapa amefanya effects gani za ajabu maana ndani ya CCM hakuna mwadilifu au mwenye nia ya dhati na hii nchi.

Hapo ndipo uliposhindwa na Kinana. Unapigana vita na Kinana binafsi badala ya kupigana na adui yako wa ukweli ambae si mwengine bali ni Mtanzania anaekunyima kura miaka yote. Fikiri.

Wakati wewe unapigana vita vya kusadikika na Kinana na CCM, Kinana yupo huko kwa wapiga kura anawakinaisha waipe kura CCM.

Kila unavyowaambia Watanzania CCM ni mbaya, Kinana ni mbaya, Watanzania hao hao wao wanakuona wewe ni fataani.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Kama huyo ramadhani ni chaguo la jk basi na ampigie kura na hiyo kura imtoshe kuwa rais.Rais wa tanzania huchaguliwa na watanzania kati ya 45m waliopo sasa unaposema ni chaguo la system na jk sikuelewi.hakuna mwenye ubavu wa kutuchagulia rais.wananchi watamchagua rais wanayemtaka,hata putin hakuwekwa na mtanguliz wake bali wananchi na duniani mfano marekani wanachaguliwa kwa kura za wamarekani,tusijazane ujinga eti jk atuteulie,tutamkataa na ccm sio mungu wetu tutaikataa pia.
 

Mkuu, let me be clear, Justice Ramadhani hana mfano kama ni Integrity, Honesty and Patriotism. Hana mfano. Ni mpole, mtaratibu, na hapendi kuumiza hisia za mtu katika maamuzi. Huyu bwana angekuwa Rais baada ya Mkapa ingekuwa safi sana tena mno, kwasababu angepooza kidogo ukali wa Mzee Mkapa lakini angeendeleza Utawala Bora na trust ya system kufanya kama ambavyo Ben aliianzisha.
Miaka 10 leo Tanzania na niseme bila kumung'unya Tanzania inanwitaji "dictator" period. Ili kuirudisha Tanzania kwenye Mstari lazima Rais awe na sifa za Magufuli, Mrema, Dr Slaa, Kinana, Nchemba and the likes
Kikwete ni mpole by nature, kwake yeye watu wapole anawachujukia kama viongozi bora, not all the time. Huwezi kumpa mpole nchi kama venezuela, mexico, colombia, DRC. Marais wapole wape nchi kama Botswana, Zambia.
 

ukiipinga system watatokea wapinzani wenzio kukupinga , elimu duni ndio imetufanya mateka wa kudumu wa system
 

ukiacha masihara yako upo vizuri sana kwa hoja endelea kubadilika nipo kando yako kimaono
 

Kaka, nashukuru sana, System inatakiwa iwe juu ya Executive, meaning System has the power to Nixon any President. System ya Nyerere ilifanya hivo kwa Mwinyi kwenye OIC. System ilifanya the same kwa Dr Salmin Zanzibar. That system ilikwenda wapi. System ilikuwa na majukumu ya kuchunga Usalama wa Tanzania wakiwa Uganda, Rwanda, Msumbiji. Hakuna Rais aliyeingia Madarakani kwa hawa Majirani yetu kama hakuwa rafiki wa Tanzania.
System ya Tanzania ilikuwa inamyima usingizi Daniel Arap Moi wa Kenya. System iliyowashinda Makaburu. Where is the Tanzanian System.
Rais Paul Kagame inasemekana ameoenyeza Wanyaryanda kwenye System ya Tanzania kadhalika M7.
Tunaandika haya sio kwa ajili ya kudhalikisha nchi yetu. hapana tunahitaji kuangalia wapi tumejikwaa tunyanyuke tupanguse suruali/skirt zetu tujenge taifa letu.
Tulikuwa kimbilio la wanyonge, wasababu wote waliokuja kwetu wakiwa wakimbizi, walirudi kwao Marais, mawaziri, na wakachukua ujuzi wetu kutengeneza nchi zao.
Tunapoiona Rwanda inanidhamu ya paka, Uganda imetulia kama mbingu, tunajisikiaje sisi kama taifa na haya Maescrow, maRada, maEpa yakitulipukia kama chunusi.
Yanayotokea Tanzania leo yalitakiwa yatokee Kwenye kama Somalia na Sudan Kusini,
Nimesikitika sana. Nimesikitika mno. Inaniuma sana kama Mtanzania
 

nimewasikia watia nia wanasema nagombea uenyekiti wa chama changu na urais, mwanzo ilikua urais kisha uenyekiti unakuja automatically sasa uenyekiti ni focus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…