Kama nchi tupo gizani

Kama nchi tupo gizani

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
11,561
Reaction score
14,627
Habari za weekend wakuu,

Ikiwa leo ni kumbukizi ya siku ya muungano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ila bado naona giza totoro kwenye nchi yetu na taifa likiwa kwenye simanzi kwasababu zifuatazo:–

1.Wanafunzi wa chuo ambao ndio future ya nchi wanawake wapo bize na connection na kudanga na wanaume wameanzisha campaign ya kusifu na kubudu utawala tupo gizani.

2.Bungeni badala wajadili ripoti ya CAG yenye madudu ya kutosha wanajadili habari za mwinjaku na baba level pamoja na mrisho gambo na mchegerwa it's dangerous tupo gizani.

3.Redio na TV zote zinajadili umbea na kutangaza kamari pamoja na kuchambua mechi za simba na yanga huku zikiacha mambo muhimu ya nchi nani alituroga Tanzania.

4.Wasanii ambao ndio wanaushawishi kwenye jamii wamegeuka machawa kwa kusifia na kuabudu baada ya kupewa mikopo na kukosa hela za marejesho. Wakati kule kenya Eric Omond anaingia barabarani na raia kudai haki.

5.Kila Siku wanazindua shule na vyuo ili wanafunzi wapate sehemu nzuri za kusoma ila ukimaliza kusoma,ukijaribu kutoa ushauri au kukosoa wanakupoteza sasa shule na vyuo vya Tanzania vina kazi gani kama vinazalisha wajinga na machawa it's very sad.

6.Haki inakanyagwa na wenye mamlaka huku wamevaa miwani za mbao machoni ukijichanganya wanakumaliza hata kama unachodai ni haki yako.

7.Watu wanaiba hela kila siku na ushahidi upo ila wanahamishwa tu vitengo huku wakiendelea kula maisha wahuni wamepiga 1.2 trillion mungu tusaidie.

8.Makosa ni ya upande mmoja tu ila wenyewe hawagusani waziri mmoja alisema tuhamie Burundi, kiongozi mwingine alisema upinzani wamedhamiria kuleta Ebola na mpox,mwingine alisema mpige kura usipige wo wanajua wanashindaje uchaguzi.

9.Machawa wanapewa nafasi tena za juu wenye uwezo na wasema kweli wanauliwa au wanawekwa benchi na kubambikiwa kesi zisizo na mbele wala nyuma.

10.Wanasema tujiajiri wakati wao wanang'ang'ania nafasi mpaka wanafikwa na umauti na watoto wao wanawatafutia nafasi. Wakati huo mzee wasira anajiandaa kurudia tena bungeni na mzee muliro mtoto wake ndio mlinzi pale bwawa la mwalimu nyerere.

Umasikini ni laana sana ukizaliwa masikini unakosa kila kitu mpaka kujiamini hawa watoto wa vigogo wamewezaje?

Maria sarungi:Baba yake alikuwa waziri lakini anapinga uhuni unaofanyika nchini.

Mange kimambi:Baba yake alikuwa kiongozi lakini anapinga uhuni wa watu wachache.

Fatuma karume:Amekulia ikulu ila anapambana na wajinga wanaojiona miungu watu.

ILA KALUMANZIRA WANA EXCUSE KIBAO.

ALAMSIK.
 
Back
Top Bottom