Kama nchi haina dini ni hukoBara sio Zanzibar

Kama nchi haina dini ni hukoBara sio Zanzibar

Quoted....."Professa Sherif amesema mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayofanyika yazingatia suala la dini kwani katiba ya Tanzania inazungumzia serikali haina dini lakini katiba ya Zanzibar haina kifungu hicho na hivyo suala la dini waachiwe watu wenyewe badala ya kuingizwa katika katiba."

Mkuu Kakke
Hapo kwenye red kama ni kweli pana tatizo. Ni vema katiba ya Zanzibar ikawa wazi kwa kutamka ama Zanzibar ni secular state ama theocratic. Kuzungumzia idadi ya majority residents na imani yao pekee haitoshi kuhalalisha kuwa dola ya imani fulani. Vipi kuhusu hao minority residents(1%)??? Hili ni swala la kikatiba na katiba haipaswi kuwa kimya kwa hilo.
Ahsante mkuu IVONYA; nilikuwa natafuta maneno muafaka ya kuelezea huyo professor alivyokiuka haki za binadamu!! kwa kushabikia "marginalisation of the minority" hakuna dhambi kubwa kama hii. Kwa sababu ni wachache then wasifikiriwe kwenye sheria mama!! A prudent learned person should be able to be analytical and think objectively. Kama huyu ndiye mkuu wa mchakato wa Katiba ZNZ then minority wameumia!!
 
sijamwelewe prof. hivi kukosekana kwa mahakama ya kadhi ni kwa sababu ya nchi kutokuwa na dini?.
sijamwelewa prof. mbona nchi yetu moja ya tanzania haina dini lakini znz kuna mahakama ya kadhi
sijamwelewa prof. hivi nchi huwa inaingia msikitini au kanisani huwa inaabudu kwa kutoa kauli gani?
sijamwelewa prof. hivi tangu tumeelewa kuwa nchi haina dini ni muumini gani(mwanaadamu) amekosa kusali?
sijamwelewa prof. hivi nchi inaweza kuwa na dini?,inaendeshaje ibada yake nijuavyo anayeabudu ni bin adamu tu.
 
Hakika umenea lazima kila kitu kiwe wazi kabisa. na kama hawataki no bora kila mtu achukue mbao zake na kuondoka.

Hongera Znz na waZnz kutetea maslahi yenu.
 
Oh, my God. Huyu ni profesa wa nini? Aliwaza nini kuandika hayo aliyoyaandika? Mbona ni mdini hivyo? Sasa atasaidiwaje? Nilishasema kwa jinsi mtu anavyokuwa anazeeka ubongo unakuwa senile. Huu ndiyo mfano hai. :majani7:
 
Quoted....."Professa Sherif amesema mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayofanyika yazingatia suala la dini kwani katiba ya Tanzania inazungumzia serikali haina dini lakini katiba ya Zanzibar haina kifungu hicho na hivyo suala la dini waachiwe watu wenyewe badala ya kuingizwa katika katiba."

Mkuu Kakke
Hapo kwenye red kama ni kweli pana tatizo. Ni vema katiba ya Zanzibar ikawa wazi kwa kutamka ama Zanzibar ni secular state ama theocratic. Kuzungumzia idadi ya majority residents na imani yao pekee haitoshi kuhalalisha kuwa dola ya imani fulani. Vipi kuhusu hao minority residents(1%)??? Hili ni swala la kikatiba na katiba haipaswi kuwa kimya kwa hilo.

Nafikiri Professor alikuwa wazi aliposema kuwa hiyo kwa Wazanzibari si issue ya kuwekwa kwenye Katiba kwani hakuna tatizo hilo. Sheria zilizopo zinatosha kuamuwa pale panapotokea tatizo la namna hiyo.
 
Oh, my God. Huyu ni profesa wa nini? Aliwaza nini kuandika hayo aliyoyaandika? Mbona ni mdini hivyo? Sasa atasaidiwaje? Nilishasema kwa jinsi mtu anavyokuwa anazeeka ubongo unakuwa senile. Huu ndiyo mfano hai. :majani7:

Si mdini bali ni Mwiislamu, sasa kuna ubaya kusemea dini yake?
 
sijamwelewe prof. hivi kukosekana kwa mahakama ya kadhi ni kwa sababu ya nchi kutokuwa na dini?.
sijamwelewa prof. mbona nchi yetu moja ya tanzania haina dini lakini znz kuna mahakama ya kadhi
Hivi umeelewa Tanzania haina dini lakini mbona Zanzibar ina mahakama ya Kadhi?
sijamwelewa prof. hivi nchi huwa inaingia msikitini au kanisani huwa inaabudu kwa kutoa kauli gani?
Hivi hii Katiba itakuwa inatumika na nani? Una maana nchi ni pande la ardhi? Jee pande la ardhi ndilo linalofanya makosa na kushitakiwa kwa mujibu wa Katiba?
sijamwelewa prof. hivi tangu tumeelewa kuwa nchi haina dini ni muumini gani(mwanaadamu) amekosa kusali?
Hivi tangu ulipofahamu wewe uliona nchi haina Katiba? Ya nini sasa muhangaiko wote huu?
sijamwelewa prof. hivi nchi inaweza kuwa na dini?,inaendeshaje ibada yake nijuavyo anayeabudu ni bin adamu tu.
Ni aibu kwa mwenye akili timamu kuuliza swali hili! Kwani hiyo Katiba huitwa vipi vile? Nahisi kama itaitwa Katiba ya Tanzania!

Hivyo kwa muono wako nini Tanzania ni mlima , bonde au kisiwa? Hii ndio maana ya mwenzio kuwa Professor na wewe kuwa ulivyo!
 
Ahsante mkuu IVONYA; nilikuwa natafuta maneno muafaka ya kuelezea huyo professor alivyokiuka haki za binadamu!! kwa kushabikia "marginalisation of the minority" hakuna dhambi kubwa kama hii. Kwa sababu ni wachache then wasifikiriwe kwenye sheria mama!! A prudent learned person should be able to be analytical and think objectively. Kama huyu ndiye mkuu wa mchakato wa Katiba ZNZ then minority wameumia!!

Nafikiri uelewa wako umezonwa na fikira binafsi! Ndio maana akasema swala la Dini lisiingizwe kwenye katiba!
Kwani wengi wanaposhinda na kufuatwa wanayoyataka huwa na maana kuwa hawa kidogo wameonewa? Ingekuwa ameshauri kuwa kwa vile Z'bar asilimia 99 ni Waislamu basi nchi iwe ya Kiislamu pengine hoja yako ingekuwa na mshiko.
 
Hayo mabunge matatu na serikali tatu nayo ziainishwe nani anabeba gharama ya kuendesha. Sio mabunge matatu na anagharamika mmoja kubeba. Dhambi ya umimi ngumu sana kuhandle. Hayo mafuta yasipopatikana zanzibar mbona hapatatosha?

Kwani sasa tuna Bunge na Baraza la Wawakilishi nani anahandle nini?
 
Zanzibar inao wakristu waliosoma vizuri,wenye sifa zinazotosha kushika nafasi nyeti katika serikali ,lakini pia,zanzibar inao watu wasiofungamana na dini yoyote,au wasio waumini wa dini yoyote,wenye elimu nzuri tu,ni ujuha professor kuyapuuza makundi haya japo anayaona ni asilimia moja ya wazanzibar ,akahitaji zanzibar itambulike kama nchi ya imani moja ya kidini ,kwangu mimi mtazamo wa huyu proffesor sii sahihi,unless ni mtaaluma na mwanaharakati wa kiimani.

Ni wapi alisema kuwa iwe nchi ya kidini? Na hadi sasa nini tatizo la Zanzibar kubaki kama ilivyo? Jamani tumieni akili badala ya utashi wa kidini.
 
Kwa hiyo hawa 1% wasio Waislamu hawana haki ya kutambuliwa?Kama vigezo vyenu ni wingi wa watu hata nyie wazanzibari ni sehemu ndogo sana ya watanzania kiidadi,kieneo na kiuchumi hivyo tunaweza kupuuza tu matakwa yenu maana hamna athari yoyote.

Nashangazwa na nyinyi kweli! Kwani wale viongozi wenu waliposema wanataka Serikali tatu walikuwa hawajui kwa tuko wachache?
 
Huyu Professor ni Kilaza kabisa - Asome Clause Number 19 ya Zanzibar Constitution ambayo ni very clear - Dini sii shughuli ya Nchi bali ya Mtu Binafsi.

19.(1) Every person has the right to freedom of thought or
conscience, belief or faith and choice in matters of religion, including
the freedom to change his religion or faith.
(2) Without prejudice to the relevant laws the profession of
religion, worship and propagation of religion shall be free and a private
affair of an individual; and the affairs and management of religious bodies
shall not be part of the activities of the state authority.
(3) In this Article reference to the word "religion" shall be
construed as including reference to religious denominations and cognate
expressions shall be construed accordingly.
 
Huu mkoa wa Zanzibar una unamatatizo sana!........

wewe una akili ndogo sannna umeona wapi mkoa kuungana. rabda ni kuulize nini maana ya muungano?
hata huyu nyerere amesema tanganyika imeungana na nchi ya znz au mkoa wa znz?
 
Ni wapi alisema kuwa iwe nchi ya kidini? Na hadi sasa nini tatizo la Zanzibar kubaki kama ilivyo? Jamani tumieni akili badala ya utashi wa kidini.

wewe u meshawahi kufika znz au unajisemea tu. fika uone
 
wewe u meshawahi kufika znz au unajisemea tu. fika uone

Mbona unanichekesha ndugu yangu? Mimi ni Mzanzibari na ni mkaazi wa huko hivyo ninaposema kuhusu Z'bar nakijuwa nini ninachokisema sio kusikia , kusma vitabuni na magazeti au kwenda kwa kutembea? Hebu nieleze kuna nini ambacho ni cha kiajabu kuhusu dini?
Waislamu wa Zanzibar na Wakristo (tulikuwa tukiwaita "mishini" tulikuwa tukiishi bila ya matatizo yoyote, tukiingia makanisani na kusoma huko na wao wakiingia misikitini kwa shughuli za kijamii. Hapakuwa na matatizo yoyote.
Matatizo yamekuja baada ya kuletwa ushindani katika dini na watu kutoka nje. Laiti hao watu wa nje wangetumiia jitihada zao katika kujenga miundombinu ya kijamii, kama mashule na mahospitali badala ya kuleta ushindani wa kidini basi hali ingekuwa bado kama ilivyo,
 
Back
Top Bottom