Kama Muungano ni mzuri Africa ingekuwa moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Muungano ni mzuri Africa ingekuwa moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jan 25, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  haewezekani masuala ya hatma ya nchi yakamuliwa na wajumbe wa chama tena chama kimoja.itakuwa sere ni ile ile serekali 2-1.
  Katika kumbukumbu zangu zote hakuna nchi hata moja Africa iloko katika Muungano ispokuwa Muungano wa (Replic of Tanzania.). Hata huo Muungano wa Eurapian EU,AU nitafauti na huu wetu. Ingekuwa Muungano wetu ni mzuri basi nchi nyingi za Africa zingeiga?.
  Lakini ni mkuubwa kumeza mdogo Watanganyika millioni 44 kungana na Wzanzibari 1.2 millioni moja laki mbili? Yani Zanzibar kupoteza utaifa wake kwa ya ujanja na udanganyifu na wenzetu ccm/smz kutusaliti kwa vikao vya halmashauri ya chama cha ccm, ndio ukaona nchi zote za Africa sio wapumbavu kuungana kwa kupoteza utaifa wa watu wao na ardhi yao,
  Sisi viongozi wetu wa ccm/smz niwatu wakuunyonga tu hawana faida yoyote ispokuwa kwenda mbio na jaa zao huku nchi wakitowa mlango wa nyuma Vishwa usaha mtupu. Kama kwela Tanganyika walikuwa wanataka Muungano na sio wizii wangeweza kuwa na Serekali yao ya Tanganyika na katiba yao ya Tanganyika kwa kusimamia mambo ya Tanganyika?. Lakini leo ktk Muungano huu kuna ubabaishaji mwingi na utapeli tufanyiwao Wazanzibar na viongozi wetu kutumbua macho tu kwa madamanio ya Dunia na kutokuziweza njaa zao.
  Hawa machongo ni wezi na hawana nia njema ya Muungano, umeuna lini Rais wa Tanzania mara zote katika maisha yako kuwa Zanzibar? Wao siwana sema Tanzania ni Zanzibar na Tanganyika? Mbona hakuna haki yakuwa Urais kwa awamu? Mara hii atatoka Zanzibar mara nyengine Tanganyika?. Mimi nahisi huu ni wizi wa kitanganyika kuvaa koti la Tanzania na kujikumbizia mazuri ya Muungano kwao tu, na Tanganyika iipo haikuwa wakfu ikawa mali ya Tanzania no, bali Tanganyika ndio hii Tanzania na ndio hupashikana Uraisi wa Tanzania na Balozi za njee wenyewe kwa wenyewe na sisi tukambulia kuramba makoko na kujidanganya kuwa tuko ktk Muungano.
  Wewe unazani hizo nchi za Ulaya zilizo ungabna kuna nchi ilio itumbukiza nchi yake kwa mwengine? Kila nchi ina mambo yake na mamlaka yake kamili ya nchi ispokuwa Muungano ni mambo Fulani tu tena yasio haribu utaifa wa mtu mwingine, na kama mundane wetu ni mzuri nchi nyingi za Africa zingeiga. Mungu kibariki kizazi cha Wzanzibar kupotea.

  [​IMG]Majadiliano ya kero za Muungano kutatuliwa ki-chama

  [caption id="attachment_27433" align="aligncenter" width="300" caption="kesi ya Tumbili kumpa Gedele muhukumiwa ni huyo huyo na wenye kuhukumu ni huyo huyo."][​IMG]
   
 2. m

  mshaurimkuu Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kati ya Tanganyika na Zanzibar nani kapoteza utaifa wake? Rais mnaye, wimbo wa taifa, bendera, katiba, bunge(baraza la wawakilishi), mahakama, n.k. Kama ni suala la urais wa Muungano pia hutoka Zanzibar. Au mlitaka muwe pia na majeshi, n.k? Lakini hata jeshi lililopo si la Tanganyika (ambayo kwa kweli haipo), ni la watanzania wote (na Zanzibar ikiwemo). Hebu tembelea miji yote na mashambani upande wa bara uone wapemba na wazanzibar kwa ujumla walivyotapakaa kila kona. Ni kiongozi yupi wa Zanzibar iwe yuko madarani au amesataafu awe CUF au CCM,awe mpemba au muunguja ambaye hana nyumba, biashara, n.k Dar-es-Salaam kama sio Bara kwa ujumla? Kabla ya kutoa kauli fikiria mara mbili mbili.

  Kama kweli muungano una matatizo toa hoja za msingi na sio kuishia tu kulalamika ooh tunaonewa, tunanyonywa, tunanyanyaswa, .....! Hebu eleza kwa ufasaha kuwepo huu muungano kumechangiaje wewe kuwa katika hali uliyo nayo na kama usingekuwepo wewe ungenufaika vipi? Sisemi kwamba muungano ni mzuri au ni mbaya ila twende kwa hoja? Hivi kwa mfumo huu uliopo ni kweli Zanzibar ndiyo inayopoteza au kinyume chake? Na inapoteza au kufaidi kivipi? Au ni "win-win" situation? Tuache kulalama bila sababu. After all, KATIBA MPYA on the pipeline, utatoa duku duku lako kadiri utakavyoweza ila sitashangaa hata kwenye mikutano hutahudhuria zaidi ya kulalamika tu.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Comoros ni mfano mzuri wanaomba wawe kwenye muungano wa Tanzania !. Tatizo la Zanzibar ni utamaduni wa kule kama wangekuwa na elimu nzuri Zanzibar ingekuwa sehemu nzuri kufanya biashara. Tatizo lingine la utamaduni ni kwamba ni vigumu kuwaleta watalii kwani watalii wa baharini wanapenda kuvua nguo na utamaduni wa Zanzibar hauruhusu vitu kama hivyo.
   
Loading...