Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Leo ningependa kuwaambia wanawake ambao wanafanya kazi, ambao wameajiriwa katika kazi zinazowaondoa nyumbani asubuhi hadi usiku, huku waume zao nao wakiwa makazini kwa muda kama huo au zaidi. Katika familia hizi, wazazi ni watumishi wa majumbani ambao wengine wanalingana na watoto wa matajiri zao. Unapomuuliza mwanamke huyu kwamba inakuwaje wanazaa watoto na kuwaachia majukumu watumishi majukumu ya kuwalea watoto wao, atakupa majibu ya ajabu sana.
Atakuambia, ‘maisha'. Yaani ni lazima afanye kazi ili aweze kukabiliana na ugumu wa maisha. Mwingine atakwambia anatamani kuacha kazi, lakini akiacha kazi, mumewe anaweza kumbadilikia na kuanza kumnyanyasa. Hayo yote ni majibu yenye makengeza. Ukweli ni kwamba hakuna maisha bora kama kulea mtoto wako mwenyewe ambaye baadae anakuja kuwa mfano wa kuigwa kesho, na kama mume anaweza kumdhalilisha mkewe kwa kuwa hana kazi, basi huyo siyo mume wa kukaa naye hata kama mke huyo ana kazi.
Huenda nikaonekana nawavunja nguvu wanawake wanaofanya kazi lakini huo ndio ukweli. Imebainika kwamba watoto ambao wazazi wao wote wanafanya kazi zinazowafanya kukosekana nyumbani muda mwingi, huwa na nidhamu mbovu sana. Watoto hao huwa na matatizo mengi ya kisakolojia pia kwa sababu ya kukosa mapenzi ya wazazi, kwa sababu ya wazazi kushindwa kujua matatizo yao na kuweza kuwasaidia na kwa sababu ya watoto hao kukosa mifano ya kuiga, hivyo kuiga ya watumishi wa nyumbani na watu wa mitaani . tukumbuke kwamba kila mtoto ana ‘shujaa' wake anayetaka kumuiga na ‘shujaa' wa awali ni mama na baba yake.
Kama mwanamke anaamini kwamba hawezi kuwalea watoto wake mwenyewe, hana muda wa saa nne au tano za kukaa na wanaye kila siku, ya nini azae? Watoto wanahitaji mzazi au wazazi katika muda mwingi wa makuzi yao, labda tu pale ambapo hilo haliwezekani kutokana na sababu zisizoepukika.