Kama Mfalme amesema hivi, nani wa kupinga?

Kama Mfalme amesema hivi, nani wa kupinga?

Mk 12:31
Na ya pili ndio hii, mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako. Hakuna amri iliyo kuu kupita hizi.
Hahaa! Umejitahidi kunukuu vifungu! Ila hicho kifungu hakina uhusiano na Andiko nililokupa la Yohana 15:13. Wewe ulisema unanipenda zaidi. Nami nikakujibu kwa kifungu hicho kwamba Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Mwenye upendo huo ni Yesu tu, aliyekubali kufa msalabani kwa ajili yetu.

Nomadix umeokoka? Kama bado, unasubiri nini? Maisha ya dunia hii ni ubatili. Tuyawaze yale yajayo: uzima wa milele mbinguni au mateso ya milele motoni. Yesu atakuja ghafla. Akija kabla hujaokoka itakuwa too late kwako. Utaachwa, maana watakaonyakuliwa na Yesu ni waliookoka tu.
1Thes 5:1-3
"Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Wakati watu bado wanasema, 'Kuna amani na usalama’"
 
Hahaa! Umejitahidi kunukuu vifungu! Ila hicho kifungu hakina uhusiano na Andiko nililokupa la Yohana 15:13. Wewe ulisema unanipenda zaidi. Nami nikakujibu kwa kifungu hicho kwamba Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.


Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo.

Ninaamini tayari nimeokoka kwa kila namna.
Yoh 3:16
"Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu....ili kila aaminiye asipotee..."

Amwaminie kristo yu na uzima wa milele.

Kuamini ni nini?
Imani inaenda sambamba na matendo,
Yak 2:17 imani bila matendo imekufa.

kwanza imani inaanzia akili,rohoni, kisha matendo ya mwili, akilini na rohoni tayari maana naamini mimi ni hekalu la Roho mtakatifu 1 Wak 3:16-17 pia namwamini Yesu ndie mkombozi wangu.

Mwilini, najitahidi kuyaepuka yote yanipasayo kuepuka nakula matunda ya roho, Gal 5:22. Amen
 
Hahaa! Umejitahidi kunukuu vifungu! Ila hicho kifungu hakina uhusiano na Andiko nililokupa la Yohana 15:13. Wewe ulisema unanipenda zaidi. Nami nikakujibu kwa kifungu hicho kwamba Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Mwenye upendo huo ni Yesu tu, aliyekubali kufa msalabani kwa ajili yetu.

Nomadix umeokoka? Kama bado, unasubiri nini? Maisha ya dunia hii ni ubatili. Tuyawaze yale yajayo: uzima wa milele mbinguni au mateso ya milele motoni. Yesu atakuja ghafla. Akija kabla hujaokoka itakuwa too late kwako. Utaachwa, maana watakaonyakuliwa na Yesu ni waliookoka tu.
1Thes 5:1-3
"Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Wakati watu bado wanasema, 'Kuna amani na usalama’"
sasa haya yote kisa nimekutongoza 😀
 
Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo.

Ninaamini tayari nimeokoka kwa kila namna.
Yoh 3:16
"Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu....ili kila aaminiye asipotee..."

Amwaminie kristo yu na uzima wa milele.

Kuamini ni nini?
Imani inaenda sambamba na matendo,
Yak 2:17 imani bila matendo imekufa.


kwanza imani inaanzia akili,rohoni, kisha matendo ya mwili, akilini na rohoni tayari maana naamini mimi ni hekalu la Roho mtakatifu 1 Wak 3:16-17 pia namwamini Yesu ndie mkombozi wangu.

Mwilini, najitahidi kuyaepuka yote yanipasayo kuepuka nakula matunda ya roho, Gal 5:22. Amen
Kama umeokoka, hongera sana. Zingatia sasa andiko hili:
Waefeso 5:3-4
Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
 
Inafikirisha kama unajiwazia mabaya tu.
Maadam tupo duniani mabaya yapo tu.
Mtume Paulo anayalinganisha mambo ya dunia hii na mavi.
Wafilipi 3:8
Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo.
 
Mahitaji ya chakula ya kila siku ya Mfalme Sulemani yalikuwa:
Vipimo 30 vya unga laini
Vipimo 60 vya unga wa kawaida
Ng'ombe 10 waliolishwa vizuri
Ng'ombe 20 waliolishwa malishoni
Kondoo na mbuzi 100
Pia kulikuwa na swala, paa, kulungu, na ndege walionenepeshwa.
Vipimo hivi vinaonyesha ukubwa wa mahitaji ya chakula katika ikulu ya Mfalme Sulemani kila siku.

Hatimaye akaona yote hayo ni ubatili mtupu.
 
Kama umeokoka, hongera sana. Zingatia sasa andiko hili:
Waefeso 5:3-4
Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
Yeah naelewa me nakupenda upendo wa kweli sijakutamani, upendo wa 1 Wak 13
 
Mfalme huyu anajulikana na kusifika dunia nzima kwa sababu ya hekima ya hali ya juu, utajiri mkubwa, maisha ya kifahari na idadi kubwa ya wanawake aliooa. Pamoja na yote hayo anakiri kwamba maisha ya dunia hii ni ubatili mtupu. Huyo si mwingine ila ni Mfalme Sulemani. Unapinga kauli yake hiyo? Mimi namuunga mkono. Ngoja nikuthibitishie ubatili wa maisha jinsi ulivyo.

Hebu jaribu kuwaza: Unatafuta pesa kwa jasho, unakuwa milionea; majambazi wanatokea wanakuibia pesa na mali zote. Unahamia Ulaya. Unajenga nyumba nzuri, drone za kivita zinakuja, zinarusha mabomu, mji wote na nyumba yako vinakuwa magofu. Unahamia nchi nyingine. Unajijenga tena. Unafunga ndoa kwa sherehe kubwa ya mamilioni, baada ya wiki moja mnapeana talaka. Unaamua kujifariji kwa kula vyakula vitamu, unaota kitambi, kisha unapata kisukari na pressure.

Unasafiri kwa ndege ukapumzike kwenye hoteli ya kitalii, mara paap, ndege inaanguka, inawaka moto, abiria wote wanakufa, wewe unaponea chupuchupu lakini miguu imevunjika umekuwa kilema!

Unaamua kuishi kimaskini, ukilala usiku, chawa, kunguni na viroboto kitandani wanakuchezea, unajikuna usiku kucha. Unapambana kujikwamua. Unabahatika kuwa kamanda, unaanza kuishi kifalme, wapinzani wanainuka, wanakuonea wivu - usiku usingizi hauji, unawaza tu uwafanyeje.

Unatoa pesa nyingi kumsomesha ndugu yako, awe kama wewe. Anasoma sana, anapata degree. Wenzake wanamroga, anaanza kuokota makopo. Unachukizwa na maisha haya, unaanza kumlaumu Mungu. Kisha unaamua kuwa Atheist. Shetani anafurahia amepata mteja, anakuletea wachawi na mapepo usiku. Ukiamka asubuhi unajikuta umelala nje ya nyumba! Unakimbilia kwa manabii wa uongo kutafuta msaada, wanakuambia nunua chumvi na mafuta ya upako, ongeza na sadaka ya kujikataa! Unafanya hivyo, lakini shida haziondoki. Umetapeliwa!

Unaamua kuwa shabiki wa mpira uburudishe moyo. Timu yako inafungwa, unakasirika, unaamua kujinyonga - kisha unajikuta uko kuzimu kwenye mateso mengine makali! Duh!

Hujasikia hayo yakitokea katika dunia hii? Kama huo sio ubatili ni nini? Hakika, kama Mfalme Sulemani alivyosema, maisha ya dunia hii ni ubatili na kufukuza upepo(Mhubiri 1:14).

Hata hivyo, kila chenye mwanzo kina mwisho. Dalili zinaonyesha wazi dunia hii yenye maudhi inaelekea mwisho. Yesu amekaribia kuja kutupeleka mbinguni kwenye raha ya milele. Ila wanaomkataa Yesu hawataingia mbinguni, badala yake watatupwa katika mateso makali zaidi, milele.

Ufunuo 20:15
Mtu yeyote ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.

Ukitubu dhambi zako na kumwamini Yesu leo, jina lako litaandikwa katika kitabu cha uzima, na utakuwa na uhakika wa kuingia mbinguni kwenye raha ya milele, siku Yesu atakapokuja.
Umenifurahisha kwa tafakuri yako hii.
 
Back
Top Bottom