Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,104
- 8,037
Mfalme huyu anajulikana na kusifika dunia nzima kwa sababu ya hekima ya hali ya juu, utajiri mkubwa, maisha ya kifahari na idadi kubwa ya wanawake aliooa. Pamoja na yote hayo anakiri kwamba maisha ya dunia hii ni ubatili mtupu. Huyo si mwingine ila ni Mfalme Sulemani. Unapinga kauli yake hiyo? Mimi namuunga mkono. Ngoja nikuthibitishie ubatili wa maisha jinsi ulivyo.
Hebu jaribu kuwaza: Unatafuta pesa kwa jasho, unakuwa milionea; majambazi wanatokea wanakuibia pesa na mali zote. Unahamia Ulaya. Unajenga nyumba nzuri, drone za kivita zinakuja, zinarusha mabomu, mji wote na nyumba yako vinakuwa magofu. Unahamia nchi nyingine. Unajijenga tena. Unafunga ndoa kwa sherehe kubwa ya mamilioni, baada ya wiki moja mnapeana talaka. Unaamua kujifariji kwa kula vyakula vitamu, unaota kitambi, kisha unapata kisukari na pressure.
Unasafiri kwa ndege ukapumzike kwenye hoteli ya kitalii, mara paap, ndege inaanguka, inawaka moto, abiria wote wanakufa, wewe unaponea chupuchupu lakini miguu imevunjika umekuwa kilema!
Unaamua kuishi kimaskini, ukilala usiku, chawa, kunguni na viroboto kitandani wanakuchezea, unajikuna usiku kucha. Unapambana kujikwamua. Unabahatika kuwa kamanda, unaanza kuishi kifalme, wapinzani wanainuka, wanakuonea wivu - usiku usingizi hauji, unawaza tu uwafanyeje.
Unatoa pesa nyingi kumsomesha ndugu yako, awe kama wewe. Anasoma sana, anapata degree. Wenzake wanamroga, anaanza kuokota makopo. Unachukizwa na maisha haya, unaanza kumlaumu Mungu. Kisha unaamua kuwa Atheist. Shetani anafurahia amepata mteja, anakuletea wachawi na mapepo usiku. Ukiamka asubuhi unajikuta umelala nje ya nyumba! Unakimbilia kwa manabii wa uongo kutafuta msaada, wanakuambia nunua chumvi na mafuta ya upako, ongeza na sadaka ya kujikataa! Unafanya hivyo, lakini shida haziondoki. Umetapeliwa!
Unaamua kuwa shabiki wa mpira uburudishe moyo. Timu yako inafungwa, unakasirika, unaamua kujinyonga - kisha unajikuta uko kuzimu kwenye mateso mengine makali! Duh!
Hujasikia hayo yakitokea katika dunia hii? Kama huo sio ubatili ni nini? Hakika, kama Mfalme Sulemani alivyosema, maisha ya dunia hii ni ubatili na kufukuza upepo(Mhubiri 1:14).
Hata hivyo, kila chenye mwanzo kina mwisho. Dalili zinaonyesha wazi dunia hii yenye maudhi inaelekea mwisho. Yesu amekaribia kuja kutupeleka mbinguni kwenye raha ya milele. Ila wanaomkataa Yesu hawataingia mbinguni, badala yake watatupwa katika mateso makali zaidi, milele.
Ufunuo 20:15
Mtu yeyote ambaye jina lake halikuonekana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.
Ukitubu dhambi zako na kumwamini Yesu leo, jina lako litaandikwa katika kitabu cha uzima, na utakuwa na uhakika wa kuingia mbinguni kwenye raha ya milele, siku Yesu atakapokuja.