Kama marefa wanaibeba Simba basi Yanga isingeshinda hata mechi moja

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Hakika nimekuwa nashangazwa na kauli ya Yanga na Mashabiki wake kuwa Simba inabebwa na Marefa.Binafsi napinga kwa sababu Uwanjani kuna Watu wengi wenye dhamana na mpira wanaofuatilia mambo mbalimbali uwanjani kuanzia Makamisaa,Marefa,Viongozi wa timu shiriki Wachezaji na watazamaji.

Hivi kama Simba inabebwa Basi viongozi hao niliowataja nao wanaibeba Simba.Na kama Marefa wanaibeba Simba nilitegemea Marefa hao hao Wangehakikisha Yanga inafungwa kwani kuibeba Simba na Yanga ikawa inashinda itakuwa haina maana.

Mashabiki wa Yanga wamesahau kuwa mpira una mambo mengi wachezaji hasa mabeki wanaweza wakawa wanacheza Offside Trick kwa timu penzi je Refa aseme Offside wakati mabeki wamemkimbia mshambuliaji?

Kwani timu pinzani hazilalamiki ila Yanga ndio inalalamika? Yanga maji mengi unga kidogo gologeni Uji tu Ugali hakuna.

Usiku mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba uzi wako uende mbali zaidi kwa kuchambua kishera na kanuna za FIFA kabisa hizo mechi zinazolalamikiwa, Usiishe kusema labda ni offside trick tu.

Uhalisia utawale kuliko hisia.

Huo ni mfano mdogo,Yaani Viongozi wote wa TFF na wa timu pinzani hawalalamiki Yanga tu ndio mnalalamika ina maana Yanga ndio wanajua kuona wengine Vipofu? Malizeni Viporo vyenu

Kocha wa Namungo hakulalamika? Wachezaji wa Namungo hawakumfuata mshika kibendera na mwamuzi wa kati kulalamikia goli la tatu? Wachezaji wa Mwadui hawakulalamika wakati wanaenda kupachika goli kisha mshika kibendera akanyosha kibendera cha offside wakati hakukuwa na offside? Vipi jana wachezaji wa Polisi Tanzania hawakulalamika na goli la kwanza lililofungwa na mchezaji wa simba mpaka wakamvamia mshika kibendera ila wakaambulia kadi tu? Vipi kocha wa mbeya city hakulalamika kuwa Simba inawahonga marefa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Screenshot_20200205-074751_WhatsApp.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika nimekuwa nashangazwa na kauli ya Yanga na Mashabiki wake kuwa Simba inabebwa na Marefa.Binafsi napinga kwa sababu Uwanjani kuna Watu wengi wenye dhamana na mpira wanaofuatilia mambo mbalimbali uwanjani kuanzia Makamisaa,Marefa,Viongozi wa timu shiriki Wachezaji na watazamaji.Hivi kama Simba inabebwa Basi viongozi hao niliowataja nao wanaibeba Simba.Na kama Marefa wanaibeba Simba nilitegemea Marefa hao hao Wangehakikisha Yanga inafungwa kwani kuibeba Simba na Yanga ikawa inashinda itakuwa haina maana.Mashabiki wa Yanga wamesahau kuwa mpira una mambo mengi wachezaji hasa mabeki wanaweza wakawa wanacheza Offside Trick kwa timu penzi je Refa aseme Offside wakati mabeki wamemkimbia mshambuliaji? Kwani timu pinzani hazilalamiki ila Yanga ndio inalalamika? Yanga maji mengi unga kidogo gologeni Uji tu Ugali hakuna. Usiku mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
. Swali LA kujiuliza kwanini waamuzi wetu hawaitwi kuchezesha mashindano ya kimataifa? Yaleyale Unatraining kizamani uchezeshe mpira kisasa.
 
. Swali LA kujiuliza kwanini waamuzi wetu hawaitwi kuchezesha mashindano ya kimataifa? Yaleyale Unatraining kizamani uchezeshe mpira kisasa.

Waamuzi wetu hawaitwi kuchezesha mechi za kimataifa kwa sababu ya ile skendo ya Yanga kuhonga Marefa, hadi kupelekea Yanga kufungiwa kushiriki soka la nje miaka 3 mfululizo na viongozi wa Yanga walioko madarakani kipindi hicho yaani mwenyekiti na mweka hazina kufungiwa kutojihusisha na soka maisha.... sema swala hili waandishi uchwara huwa hawalihoji wao wanakimbilia kusema waamuzi hawana viwango ila sababu kubwa tulipigwa blacklist na Fifa hadi watakapojiridhisha, Ila hapa inatakiwa jitihada za viongozi waliopo madarakani wa TFF...

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwaka gani ilikuwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tunataka soka letu liendelee tuweke ushabiki pembeni tuzungumze ukweli. Mimi nitajikita kwenye matukio matatu yaliyoniacha mdomo wazi. Nilitazama mechi zifuatazo:-
1. Simba na Mwadui - Venance Ludovick alitoka mbele ya Kapombe akawapita Wawa na Nyoni wamesimama akaufuata mpira uliopigwa na kipa wake ukampita Mkude ukadunda ukawaruku Wawa na Nyoni kwa maajabu kabisa mshika kibendera akainua kibendera kuashiria ni offside na refa akakubaliana naye kuwa ni offside.
2. Simba na Namungo - Goli alilofunga Kagere alikuwa tayari kazidi lakini refa na mshika kibendera wakakubali kuwa ni goli halali
3. Simba na Polisi - Goli alilofunga John Boko alikuwa tayari kashaotea lakini refa akasema weka kati

Ukweli mchungu kwetu mashabiki na wapenzi wa Simba tunaweza kujisifu sana na kuwakoga wapinzani wetu kwa huu ushindi tunaopata lakini mficha maradhi kifo humuumbua. Tutachukua kombe la ubingwa lakini huku mbele ya safari tujiandae kula 10 - 0 tukikutana na akina AS Vita, Mazembe, Al Haly n.k. labda baada ya ligi ufanyike usajili mpya makini pamoja na kuleta kocha mwingine mwenye viwango.

Simba inatakiwa sasa hivi imtimue huyu kocha mzungu timu aachiwe Matola mpaka mwisho wa msimu kabla mambo hayajaribika. Timu haijulikani inacheza mfumo gani sasa hivi, wachezaji wanakimbia kama wamefungwa mawe viunoni, wachezaji wanakaba kwa macho, timu inakata pumzi ikifika dakika ya 60, mabeki wakati hawana mbio kabisa halafu kijana Mlipili hata benchi hakai, viungo wako taratibu mno badala wakati mwingine kupiga counter attack hata kama wamenasa mpira wakati wanashambuliwa na timu pinzani ina watu wachache nyuma wao kila mpira wanataka wapige square pass wakifika golini unakuta mabeki wa timu pinzani wamesharudi golini kwao. Yaani siku hizi ushindi wa Simba ni wa mbinde sana mashabiki roho juu dakika zote tisini. Na kila siku tunaokolewa na waamuzi pamoja na kipa wetu Kakolanya ambaye amejitahidi sana kufuta makosa ya mabeki wake.

Najiuliza hivi viongozi wetu hawayaoni hayo mapungufu yote toka kocha mpya kapewa timu au huyu mzungu ni kocha wa bei rahisi? Hivi kulikuwa na haraka gani ya kumfukuza Uchebe halafu analetwa kocha mwenye kiwango cha chini kiasi hiki?. Kama kuna kosa viongozi wa Simba watalifanya ni kumuacha huyu mzungu afundishe timu mpaka mwisho wa msimu kwa sababu lolote linaweza tokea japo wanaifuatia Simba wapo pointi 10 nyuma lakini mechi bado nyingi na kiwango cha Simba kinazidi kuporomoka. Mbaya zaidi wakati kiwango cha Simba kinazidi kuporomoka wapinzani wake wa karibu wao wananza kuimarika.
 
Hakika nimekuwa nashangazwa na kauli ya Yanga na Mashabiki wake kuwa Simba inabebwa na Marefa.Binafsi napinga kwa sababu Uwanjani kuna Watu wengi wenye dhamana na mpira wanaofuatilia mambo mbalimbali uwanjani kuanzia Makamisaa,Marefa,Viongozi wa timu shiriki Wachezaji na watazamaji.

Hivi kama Simba inabebwa Basi viongozi hao niliowataja nao wanaibeba Simba.Na kama Marefa wanaibeba Simba nilitegemea Marefa hao hao Wangehakikisha Yanga inafungwa kwani kuibeba Simba na Yanga ikawa inashinda itakuwa haina maana.

Mashabiki wa Yanga wamesahau kuwa mpira una mambo mengi wachezaji hasa mabeki wanaweza wakawa wanacheza Offside Trick kwa timu penzi je Refa aseme Offside wakati mabeki wamemkimbia mshambuliaji?

Kwani timu pinzani hazilalamiki ila Yanga ndio inalalamika? Yanga maji mengi unga kidogo gologeni Uji tu Ugali hakuna.

Usiku mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewasikia Karia Msomali na Useless Mwakyembe?
Ingekuwa malalamiko hayana msingi, wasingechukua hatua za kujikosha.
 
Back
Top Bottom