Kama Mahakama ni mhimili wa tatu wa serikali kwanini Jaji Mkuu ateuliwe na Raisi?

semzei

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
416
266
Kuna haja ya katiba yetu tuiangalie kwa upya na utafutwe utaratibu wa kumpata Jaji Mkuu kwani kwa mfumo ulivyo sasa mahakama ni tegemezi kwa mhimili mwingine.
 
Rasimu ya Jaji Warioba iliyaona yote haya na hii lilikuwa libadilishwe.

Madaraka ya Rais ni makubwa sana na hilo lilionekana wakati wananchi wakitoa maoni yao kwenye tume ya Warioba na walipendekeza lazima yapunguzwe.

Nilikuwa nafatilia uteuzi wa Jaji Mkuu wa Kenya hivi karibuni nahisi na sisi tulikuwa tuifate hii flow au ingekuwa vema tuifate.

Wana Independent Judicial Commission ambayo ndio inapokea maombi kutoka kwa applicants wote.

Kwaiyo huwa watu wanaojiona wanaimudu nafasi ya Jaji Mkuu wanaomba kwa kupeleka applications na CV zao.

Then judicial commission inapitia applications zote na ku select ambao wame qualify kwa interview.

Interview zinaanza kufanyika. Ni process ndefu kidogo.
Na hizi interview zinakuwa Live broadcasted on Television.

Baada ya hapo wao judicial commission wanaona ni yupi ambae ame score zaidi ya mwingine na ndio wanalipeleka jina lake kwa Rais for endorsement.

Kwa Rais anaweza kukataa kwa reasons zake.
Basi atapelekewa candidate aliyemfatia au kama ikishindikana mchakato unaanza upya.

Rais akisha endorse, jina lile linapelekwa kwenye Bunge lao kupitishwa na hapo ndio Jaji Mkuu anakuwa amepatikana.
 
Sasa ateuliwe na nani? Bunge ni Muhimili pia, Mahakama ni muhimili pia. Yes amiri Jeshi Mkuu ndiyo kazi yake ila hana mamlaka ya kumwachisha kazi au kumfukuza.
 
Issue hapo ni katiba huru isiyoangalia upande mmoja pamoja na tume huru,angalia wenzetu wakenya katiba yao imekaa vizuri sana.
 
Kuna haja ya katiba yetu tuiangalie kwa upya na utafutwe utaratibu wa kumpata Jaji Mkuu kwani kwa mfumo ulivyo sasa mahakama ni tegemezi kwa mhimili mwingine.

Kwa mfumo wa nchi yetu, raisi anaingia kwenye kila mhimili wa dola.

Bunge, raisi ni sehemu ya bunge, yeye ndo analifungua na yeye ndo analifunga na akiamua analivunja kabisa bunge lenyewe chaguzi zinarudiwa.

Mahakama. Raisi anateua jaji mkuu, jaji kiongozi, muendesha mashtaka, yeye mwenyewe anaingiza watu wawili kwenye composition ya judicial commision.

Serikali, raisi ndio mwenyekiti wa baraza la mawaziri na bla blah zingine zote.
 
Inasikitisha sana kusikia kampuni ya vodacom inatoa siri za wateja wake na kuisaidia jamhuri kwenye malengo ya kisiasa kesi ya Lema ina mlengo wa kisiasa ndoo maana nashangaa vodacom kampuni kubwa hii kuingia moja kwa moja kwenye kushabikia siasa au kukisaidia chama cha mapinduzi ukweli nashindwa kuelewa taifa hili linaelekea wapi ? Juzi mfanyakazi wa vodacom alijitokeza kutoa ushahidi mahakamani wenye lengo la kugandamiza mhe.lema je ? Watanzania hatuna imani tena na kampuni hii ya vodacom kutumika kisiasa kutoa siri za wateja wake hii tukiifumbia macho itakuwa ni hasara kwa taifa letu kwa ujumla.


Mkuu, sioni tatizo la ushahidi wote kutolewa kwa ajili ya kufanikisha masuala ya kisheria. Vodacom wanawajibika kisheria kutii sheria za nchi. Iko sheria inayosimamia usajili wa simu zote za mawasiliano tZ. Sheria hii ilitungwa kwa lengo la kuwafuatilia na kuwatambua kwa urahisi wanaovunja sheria kwa njia ya simu.

Vodacom kama kampuni nyingine ya simu iliyosajiliwa TZ, wanawajibu wa kutoa ushirkiano kwa vyombo vya sheria pale wanapohitajikakufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Utaratibu huo huo, unasaidia hata wewe ukikutana na mkora akaiba simu yako au akatumia mtandao wa simu kwa mawasilliano dharimu.

Tatizo langu linalonipa shida ni umahakama wa mahakama. Je MAHAKAMA ITASIMAMA KAMA MAHAKAMA ILI HAKI ITENDEKE? TUMEONA MENGI YANAYOPELEKEA WATZ KUTAMANI KWAMBA AWE NDOTONI NA ATAKAPOAMUKA AONE ILIKUWA NDOTO NA ALIYOYAOTA SI YA KWELI.

TANZANIA HII!
 
hii katiba ina loopholes nyingi ndo maana wameing'ang'ania ili waendelee kutawala milele
Katiba ya Ujamaa inatumika kwenye democracy ................!!

Kwa kweli Tanzania bado tuna kazi kweli kweli!! Halafu kuna watu wanataka kutuaminiasha kuwa kuna mtu anainyosha hii nchi kwa vile ilikuwa imefikia pabaya!!

Obama safari yake ya kwanza Africa 2009 kule Accra Ghana alisema "Africa does not need strong men but rather needs Strong Institutions". Kwa kiswahili changu ... Afrika haihitaji viongozi wakali bali inahitaji mising imara!! Slowly, I am getting it!!
 
Back
Top Bottom