Kama maeneo yana ramani kwanini serikali inaruhusu ujenzi holela?

lalie

Member
Jan 6, 2024
26
33
Ndugu zangu wanajamii forums nielimisheni:

Hapo kwetu Bagamoyo kuna ramani mbili; moja ni mpango mjini yaani kwa Chingereza wameniambia wanaita TP. Nyingine wanaita kitu kama saveyi.

Vyote hivi vipo katika ofisi ya mkurugenzi idara ya ardhi kwenye makabati. Kwenye eneo husika wameweka vinguzo vidogo vidogo juu yake wameandika namba. Mimi nilidhani hawataki tena watu wajenge kiholela . Wapi?!

Nimemwandika mkurugenzi mara tatu kwa nyakati tofauti tofauti kumuomba azuie ujenzi holela kwenye barabara zilizopo kwenye ramani na michoro ambayo ofisi yake imetengeneza na Waziri wa Ardhi na vilivyoko juu yake nimempa nakala kila wakati.

Hakuna kilichofanyika! Barabara zimezibwa, mashimo yamechimbwa. Mimi namuuliza Mkurugenzi wangu; kulikuwa na haja gani kugharamia pesa nyingi kutoka kwa watu kutengeneza ramani ambazo haziheshimiwi, hazipo wazi? Kwani kazi ya maofisa ardhi ni nini? Wao sio wanaopaswa kuangalia mipangilio ya vibanda vyetu? Siku tukipata pesa tutajengaje kwenye maeneo ambayo vibanda vimeota kama Zaraninge?

Naomba tena mkurugenzi mara hii hadharani na boss wake natamani aone kuwa anapaswa kuzuia ujenzi holela kwenye maeneo ambayo tayari yamepimwa. Nimemwandika mara tatu; mara ya mwisho ilikuwa mwezi wa sita/ saba mwaka huu. Sijaona lolote. Nimepoteza wino, karatasi, muda, hisia zangu,nguvu na pesa. Hasara tupu!
 
🙄🙄
 
Attachments

  • IMG_20240113_003425.jpg
    IMG_20240113_003425.jpg
    31 KB · Views: 1

Utakuta hata hizo barua hajasoma zimeishia kwa sekretari, ndo ofisi zetu zinavyo 'operate'
 
Back
Top Bottom