Kama Lowassa ni Msafi, Nani Mchafu CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Lowassa ni Msafi, Nani Mchafu CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mfianchi, Dec 1, 2011.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Jamani hapa chini ni makala ya Msomaji Raia kutoka gazeti la Raia Mwema, swali langu hawa Wazee ambao EL aliwatumia kushinikza aliyekuwa raisi enzi hizo Mkapa ili EL aingizwe kwenye baraza la mawazili na baadaye hao wazee walimshinikiza Mkapa kusema chaguo ni Kikwete wakati wakijadili kumteua mgombea uraisi 1995 na hata juzi hao wazee walipewa mlungura kumtisha Kikwete,ingawa nina hakika mmoja wapo ni Kingunge na Mngeja je wengine ni nani.

  Je pia intelejensi siku hizi inafanya kazi tu kwa Chadema ina maana hizo pesa zilizotolewa kwa hao wazee na vijana walikuwa hawajui na je si ukosefu wa nidhamu kwa wajumbe kuacha simu zao wazi ili watu wa nje wasikie yanayosemwa kwenye kikao,hapo intelijensi iko wapi hawakuona watu wamefanya makusudi kumdhalilisha mwenyekiti ?

  kwa kuacha wazi hizo simu ,pia kwanini ni EL na Sumaye tu ndio walipewa nafasi ya kuongea,pia kwanini kauli ya Sumaye ilipindishwa kwa makusudi na waandishi wa habari?

  Nawakilisha iili tupembue pumba na mchele.

  [/FONT]
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  MSAFI NI andrew chenge,rostam aziz,ngeleja, ARTHUR MWAKAPUGI,ADAM MALIMA NA JK nyerere
   
 3. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2013
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza vikao vyake mjini Dodoma wiki iliyopita. Kama kawaida yake kwa siku za karibuni, kumalizika kwa vikao vya chama hicho, ni mwanzo wa mnyukano mpya ndani ya chama na maandalizi ya harakati mpya za kumalizana.
  Kama wengi wetu tulivyotabiri tangu Aprili, mwaka huu kuwa dhana ya kujivua gamba ndani ya CCM ilikuwadaganya toto, imetokea kweli na safari hii Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) imegwaya mbele ya ubabe wa mafisadi na kuishia kuagiza eti suala hilo lirudishwe katika vikao vya ngazi za chini.
  Pamoja na utitiri na urefu wa vikao vya maandalizi ya NEC, haikuwezekana kutekeleza dhana ya kujivua gamba kama ambavyo ilikuwa ikipigiwa chapuo na watendaji wapya wa sekretariati ya CCM, wakiongozwana Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
  Alikuwa ni Nape pamoja na wenzake kina John Chiligati, Wilson Mukama na Mzee Pius Msekwa waliorindima baada ya kikao cha NEC ya April 2011, wakidai mafisadi ni ama wajiondoe haraka ndani ya chama au wafukuzwe ndani ya siku 90.
  Walianza kampeni hiyo baada ya kikao hicho wakisafiri kwa barabara na kufanya mikutano katika miji ya Dodoma, Morogoro, Chalinze na kupokelewa jijini Dar es Salaam kwa mbwembwe nyingi. Rais Kikwete alinukuliwa baadaye kidogo akiwa katika uzinduzi wa nyimbo za Injili kuwa aliyokuwa akiyasema Nape Nnauye yalikuwa na baraka za Chama cha Mapinduzi.
  Kwa mshangao wa wengi, katika kikao kilichopita, ambacho kilitarajiwa kutekeleza azimio muhimu la NEC ya April, aliibuka Edward Lowassa na kudai bila kigugumizi kuwa alichokifanya akiwa Waziri Mkuu na kutafsiriwa kuwa ni fisadi, kilikuwa na baraka za Rais Kikwete, Baraza la Mawaziri na timu ya makatibu wakuu. Alilalamika wazi kwa jinsi alivyoendelea kudhalilishwa huku uongozi wa serikali na chama ukikaa kimya kana kwamba haujui ukweli wa mambo.
  Kimsingi, Edward Lowassa alimaanisha kuwa yeye ni mtu safi kwa sababu alitekeleza yale aliyoelekezwa kutekeleza na kwa hiyo, kujiuzulu kwake kamwe kusitafsriwe kama alama ya kukubali kuwa fisadi. Alikumbusha na kuonya kuwa ikiwa tuhuma tu zinatosha kumfukuza mtu kutoka kwenye chama, basi hata Rais Kikwete asingeweza kuwa Rais, ila kwa busara na hekima za Mzee Mkapa, Rais Kikwete sasa ni Rais pamoja na tuhuma zote alizorundikiwa wakati ule. Kimahesabu, Lowassa alisema ikiwa yeye ni mchafu, basi wote au wengi sana ndani ya CCM ni wachafu, vinginevyo yeye ni msafi.
  Tunaambiwa ilibidi Rais Mkapa aingilie kati ili kuzuia Rais Kikwete asijibu tuhuma alizorushiwa na Lowassa na wala watu wasiruhusiwe kuendelea na mjadala huo ulioelekea kuchafua hali ya hewa ndani ya ukumbi.
  Hii ni kawaida sana katika falsafa ya utawala wa Kiafrika kwani tuhuma mbaya dhidi ya mtawala huwa haziruhusiwi kujibiwa ili kuepusha hatari ya watu wabishi kuja na ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zao dhidi ya mtawala.
  Swali la msingi tunalohitaji kujiuliza ni ikiwa Edward Lowassa anadai yeye ni msafi, na baadhi ya wajumbe wa NEC wanakubaliana naye, je ni nani ndani ya CCM ya sasa ni mchafu? Sina maana kuwa Edward Lowassa ndiye alikuwa mchafu peke yake na kwa kuwa sasa inadaiwa ni msafi, kwa hiyo wachafu hawapo! La hasha, hii si maana yangu.
  Maana yangu haswa ni kuwa, Edward Lowassa tangu enzi ya hayati Baba wa Taifa, hajawahi kuwa na sifa ya usafi au uadilifu. Yeye ana sifa ya uchapakazi, uthubutu na ukarimu. Tangu enzi hizo na hasa baada ya kuzodolewa na Baba wa Taifa juu ya utajiri mkubwa usiokuwa na maelezo, Edward Lowassa aliingia katika mgogoro mwingine na Rais Benjamin Mkapa pale alipohamasisha Umoja wa Vijana (UVCCM) kugoma kumpigia kampeni baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM, mwaka 1995.
  Rais Mkapa alinyenyekea na kukubali masharti aliyopewa na ndipo vijana wakaingia katika kampeni. Hata hivyo, Mkapa aliamua kumwacha nje Edward Lowassa katika serikali yake ya kwanza hadi alipofuatwa na wazee miaka kadhaa baadaye na kumrejesha tena serikalini. Rais Mkapa alikiri baadaye kuwa alimrejesha serikalini kwa heshima ya wazee wale na wala si kwa uadilifu wake.
  Edward Lowassa ana kipaji cha kuhamasisha na kutisha watawala wasiojiamini. Alifanya hivyo mwaka 2005 ili kumwingiza Jakaya Kikwete madarakani. Kama alivyodai mwenyewe wiki iliyopita mbele ya NEC, tuhuma nyingi zilimkabili Jakaya Kikwete na kutishia kuondoa jina lake katika kinyanganyiro cha urais.
  Edward Lowassa kwa umahiri mkubwa, alikusanya vijana kutoka nchi nzima na kuwaleta Dodoma ili kuwatisha wazee kuwa Jakaya Kikwete asipoteuliwa, CCM ingesambaratika vibaya sana. Pamoja na jeuri yake na msimamo wake, Rais Mkapa aliogopa sana pale alipoitwa na wazee aliowakuta Dodoma na kuambiwa kuwa “chaguo ni Jakaya” vinginevyo Dodoma hapatatosha.
  Mkapa alinywea na kujikuta anaimba wimbo wa Jakaya huku Lowassa akiwa anachekelea kwa kejeli ya hali ya juu. Akiwa ni kamanda wa mtandao uliomwingiza Kikwete Ikulu, Lowassa kwa wema na ubaya, aliufahamu udhaifu wa Kikwete na kuufanya mtaji wa kumhujumu wakati wowote. Alichokifanya wiki iliyopita ni utangulizi wa makubwa yajayo.
  Mbinu aliyoitumia Lowassa mwaka 2005 kumtisha Mkapa ili kumwachia Jakaya aingie bila mikwaruzo, ndiyo hiyo hiyo aliyoitumia ‘kummaliza’ Kikwete wiki iliyopita mjini Dodoma. Alikusanya makundi ya vijana kutoka sehemu mbalimbali na kuwaleta Dodoma huku akiwachochea kuwa umoja wao unafutwa; aliwakamata wazee kadhaa maarufu katika chama na kuwafadhili; akawakamata baadhi ya wenyeviti wa mikoa; akaigawa sekretariati ya CCM na kisha akawapata Wazanzibari wengi upande wake.
  Hii ilitosha kumtisha Kikwete mpaka akawatosa majemedari wake waaminifu akina Nape, Chiligati, Sitta, Membe, Makongoro Nyerere na Kinana. Tishio la kuenguliwa katika nafasi ya uenyekiti wa chama lilimfanya hata amtose katibu wake Mkuu, Wilson Mukama, ambaye ndiye mjenzi wa dhana ya kurejesha hadhi ya chama kwa kuwaondoa wanaokichafua.
  Kama ilivyokuwa kwa Mkapa mwaka 2005 kwa watu kudhani amerogwa na nguvu za giza, ndivyo ilivyokuwa kwa Jakaya Kikwete wiki iliyopita ambaye watu wengi wa karibu naye wanaamini amerogwa na nguvu ya “TV Emmanuel” au nguvu ya aina fulani inayomfanya awe na kigugumizi kisicho cha kawaida.
  Waafrika ni wepesi wa kuamini ushirikina lakini kilichofanyika si kigeni katika siasa za makundi. Wanasiasa wajanja hutumia mbinu za kuwafitini wenzao kwa kuwatisha kuwa watatoa hadharani madhambi yao na kuwafanya wafyate mikia yao. Edward Lowassa anajua vema kutumia nafasi hii na anaelekea kufanikiwa. Pigo alilotoa kwa Kikwete wiki iliyopita linatishia kabisa kuua fikra zozote za kuibua tena dhana ya ufisadi katika nafasi na haiba ya Edward Lowassa.
  Pigo hilo lilimfanya Kikwete akatae au asahau hata kuwapa nafasi ya kuongea wale aliokuwa amewapanga waongee ili kumtetea yeye binafsi au kummaliza Edward Lowassa. Baadhi ya marafiki zake wanaomboleza kwa kunyimwa nafasi ya kumsaidia baada ya Edward Lowassa kuwa amemrushia makombora mazito sana.
  Mpaka hapa, bado swali linabaki, ikiwa Edward Lowassa amefanikiwa kujinasua katika tuhuma za ufisadi na kuwafanya washtaki wake wagwaye, ni nani basi anaweza kumzuia kuwa Rais ajaye kupitia CCM?
  Je, wale waliokuwa msitari wa mbele kumtuhumu hadharani watafanya nini watakapotakiwa kupanda jukwaani kumnadi kama “tumaini la pili lililorejea”? Jambo moja ni wazi: Uongozi dhaifu waweza kuwafanya mamluki kuwa mashujaa na wahenga wa kizazi husika;

  Source: Raia Mwema
   
 4. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2013
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,303
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Umeyachambua vizuri hayo mafisadi lakini hawana chao2015 sanasana serikali ya mseto itawaokoa na ndiyo mwanzo mwa nchi yetu kuwa maskini zaidi ya hapa

  "To know the enemy is half the victory"
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2013
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana 2010 Dr Slaa alisema kuiingiza CCM madarakani tena ni kuleta balaa la kujitakia nchi nzima.
  Edward hakutolewa kafara wala hakuonewa.
  Ndiyo alikalia Benchi lakini miradi yake ya RichMonduli bado inampa Mabilioni mpaka leo na kumpa uwezo wa kupita na kuhonga Waumini wa dini zote Wachungaji, wainjilisti mashemazi Mapdre, mashehe Mamufti Maakofu, sasa hivi anajaribu kumhonga Mungu na fedha zake za Mavi.
  Amekalia Benchi lakini Miradi yake ya umeme hewa wa Dowans bado inamwingizia Dola $$$200,000 kila siku sawa na Tshs 500,000,000.00. Nusu billioni za Tanzania.
  Edward hakuwa victim alipo wekwa benchi bali Wananchi wa Tanzania ndiyo wanaendelea kuwa victims. Hii ndo asili ya Serikali ya CCM kushindwa kabisa kumtaja Mmiliki wa DOWAN mpaka leo hii.
  Edward ndiye beneficially mkubwa wa DOWANS AKA RICHMONDULI kampuni ya kufua umeme hewa Tanzania.

  Wote ndani ya CCM wameoza. Miili yao imeoza, akili zao zimeoza, Hata roho zao zimeozeana, wote kabisa.
  Na hii ndiyo sababu ya kweli iletayo hali hii tuliyo nayo sasa hivi kama nchi.

  Mtu yeyote anayetegemea kwamba Tanzania itapata maendeleo chini ya CCM,
  Mtu huyo anajidanganya mwenyewe kwa kulazimisha kuamini kwamba hali ya uchumi na ustawi wa jamii Tanzania ni mfano wa kuigwa.
  Tuko hoi kiuchumi kwa sababu ya CCM yote si mtu mmoja mmoja.
   
 6. t

  tenende JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2013
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna serikali ya mseto... Zenj sawa hapa uhuni huo hapana!
   
 7. Mwamba Usemao Kweli

  Mwamba Usemao Kweli JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2013
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ni mapepo ccm yanaleta dhiki na mauaji tz.
   
 8. Eng mwang'oko

  Eng mwang'oko Member

  #8
  Jun 24, 2013
  Joined: Apr 14, 2013
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hii habari hapa inaonyesha mkapa ndo Alikuwa starring mzuri...na anajua kuwa wote hao wawili JK na Richmond's ni watu wawili kama million 2...wanasemana ila pembeni ni jeshi la wa2 wawili....swali langu nani atasimama CCM 2015, na nani atakaye mdefend huyo mgombea,kama mkapa alivyokuwa hataki kikwete kupewa nchi?
   
 9. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2013
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ushindani ndani ya CCMni mkubaw kuliko nje: kwa maono yao. lakini cha maana ni kuyaacha yapambane, yapeane sumu, watukanane, yachafuane yakimaliza. kwa kifupi tutawaonesha wakati wao wa kutunyonya umeisha. Sasa tunataka tuifaidi Tanzani ayetu bila ufisadi mauaji na propaganda
   
 10. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2013
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  mungu ibariki tanzania, hakuna marefu yasio na ncha. tusife moyo ipo siku tutawashinda hawa mashetani.
   
 11. s

  shibwe Senior Member

  #11
  Jul 17, 2013
  Joined: Mar 18, 2013
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nacho kijua ccm kina wenyewe sinape,chiligati,msekwa,muukama wa mangula wanaweza kumtoa lowasa ccm wote wageni ndani ya chama wate makapuku wana nunulika
   
 12. c

  chuuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2015
  Joined: May 19, 2015
  Messages: 317
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Mh EDWARD NGOYAI LOWASSA NI MSAFI.

  Watu wengi wataishangaa kauli yangu, watakaa midomo wazi na kujiuliza maswali kibao moja ya maswali watakayojiuliza ni kama yafuatayo.

  Anasema EL ni msafi wakati alithubutu kumuita Fisadi?

  Usafi wake uko wapi au kwa kuwa kahamia Chadema?

  Huyu anayesema haya ni mamluki au Chadema kweli?

  Hayo ni baadhi tu ya maswali japo najua kuna maswali mengine mengi zaidi juu ya mh EL.

  Wanapoendelea kujiuliza ni vyema na mm niwaulize maswali kadhaa kama ifuatavyo?

  Kama EL ni mwizi au fisadi ni kwanini hadi leo hajakamatwa na kupelekwa Mahakamani?

  Je hajakamatwa kwakuwa serikali ni dhaifu au haijui sheria inazosimamia yenyewe au iliogopa kuumbuliwa zaidi?

  Toka 2008 hadi leo nini kimefanyika baada ya EL kwa kulinda heshima yake na kuamua kujiweka pembeni?

  Tunadhani ni kwanini jina lake liliishia njiani? papo hapo jiulize kwanini Rizone alitweete akionesha hayupo tayari kuona Rais akitokea kaskazini kipindi cha Uhai wake?

  Je ni kwanini Rais JK hajawahi kuthubutu kumsema EL hadharani?

  Je ni kwanini Upinzani walimpiga sana mitandaoni na hata majukwaani lakini leo wapo meza moja?

  Ni kwanini CCM walimuamini tena 2010 akapeperusha Bendera yao jimbo la Monduli? utamuaminije Mwizi?

  Je ni nchi gani upinzani ilishawahi kuing'oa serikali bila kutumia watu waliokuwepo au waliopo Madarakani?

  Je tunapenda kuendelea kuwa masikin kwa mfumo uliopo?

  Bado nina maswali ambayo sitayamaliza sasa hivi ila endelea na ww kujihoji na kujipa majibu huku ukiangazia mfumo mzima wa chama cha mapinduzi na serikali yake ndipo utapata majibu.

  Narudia kusema "EL si Mchafu hata kidogo" lakini katika yote Mfumo wa CCM ndio mchafu na ndio unaowafanya wachafuke hata wasio wachafu, yawezekana kabisa msielewe dhana yangu lakini pia mkanielewa dhana yangu.

  Mimi kama mwanachama wa chadema sipo tayari kuendelea kuitwa mpinzani lakini nipo tayari kuona nchi hii ikiwa upinzani kwa masilahi mapana ya watz wote.

  Nitaeleza kwa kina nikitulia sehemu yenye upepo mwanana

  Jiunge na Team ya Ushindi
  Dr. Kilawa
   
 13. c

  chuuma JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2015
  Joined: May 19, 2015
  Messages: 317
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  sio mtoe tena kama mlivyozoea
   
 14. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2015
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Aturudishie ranch yetu, tugawane kwanza ndio tujue kaungama?
   
 15. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2015
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,692
  Likes Received: 13,632
  Trophy Points: 280
  Aturudishie fedha zetu alizokwiba kupitia Richmond
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2015
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
 17. DuppyConqueror

  DuppyConqueror JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2015
  Joined: Mar 30, 2014
  Messages: 9,060
  Likes Received: 4,183
  Trophy Points: 280
  Umeshindwa kutetea hojayako mwenyewe...
   
 18. Crocodiletooth

  Crocodiletooth JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2015
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 9,650
  Likes Received: 3,503
  Trophy Points: 280
  TOOLS AMBAYO ILIKUWA KTK MFUMO IKAJIENGUA NDIYO TOOLS HIYOHIYO INAYOUTAMBUA MFUMO NA NDIO TOOLS HIYO HIYO ITAKAYOWEZA KUTUKWAMUA!

  FRESHLY EXTERNAL TOOLS NI NGUMU SANA,UNLESS LABDA MAPINDUZI!

  MFUMO ULIOPO MADARAKA UMEJIZATITI SANA.

  **it needs special tacts**

  lowassa can coup! and has an ability!
   
 19. Crocodiletooth

  Crocodiletooth JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2015
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 9,650
  Likes Received: 3,503
  Trophy Points: 280
  nazile nyumba zetu za serekali ZIRUDISHWE PIA!
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  Mzimu wa ufisadi wa Lowassa utamwandama mpaka mwisho wake.
   
Loading...