Kama Lowassa ndiyo amekuwa mshauri wa Maalim Seif, basi ni mchanga na ulezi mtaona

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Kususia Uchaguzi hakuwezi kumnufaisha Maalim Seif au CUF bali kutanufaisha CCM Zanzibar na ADC kupitia kwa Hamad Rashid.

Maalim Seif aachane na fikra za baadhi ya wana CUF ambao hardliner kwa sababu hawamsaidii in long run. Ifahamike kuwa CUF ina wajumbe wawili kwenye Tume ya Uchaguzi lakini pia ina wananchama ambao hata wakiwekwa kama mawakala hawawezi kukubali kuhongwa wakati huo huo, by default, Maalim Seif bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Kwa maana nyingine, CUF ina nyenzo za kuwezesha kukabiliana na mbinu zozote za kuhujumu matokeo.

Kama Maalim Seif anadhani Serikali ya Mapinduzi itaogopa kufanya uchaguzi kwa sababu ya kuogopa kunyimwa misaada na wahisani atakuwa anajidanganya kwa sababu wahisani wakubwa wa serikali ya Mapinduzi ni kodi za Watanganyika na siyo Jumuiya ya kimataifa. CCM Zanzibar pia ni sugu kwa sababu hata kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 1995 na 2000 waliwekewa vikwazo lakini wakadunda tu kiutawala kwa sababu ya mgongo wa Tanzania Bara.

Mbaya zaidi, hata wahisani wa serikali ya Muungano hawawezi kukataa kutoa misaada kwa serikali ya Muungano kwa kutumia kigezo cha suala la Zanzibar hasa ikichukuliwa hata Katiba ya Zanzibar inasema Zanzibar ni nchi wakati huo huo uchaguzi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ulifanyika kwa uhuru na haki kama walivyohitimisha kwenye repoti zao za waangalizi wa uchaguzi. Rejea chaguzi za 1995 na 2000

Kama Maalim Seif anategemea ushauri wa Lowassa, basi atakuwa anapotea kwa sababu Lowassa ni msanii mzuri sana!

Lowassa always pretend to act big but in reality, it’s empty action!

Lowassa aliweza kucheza sanaa na kutuaminisha ni zaidi ya CCM lakini kumbe alikuwa ni sawa na samaki ndani ya maji!

Lowassa aliweza kuwaaminisha kina Tundu Lissu anakuja CHADEMA na wabunge wa CCM wanaomaliza muda wao wasiopungua 50, wenyeviti wa CCM wa mikoa wasiopungua 22 pamoja na wenyeviti 88 wa wilaya wa CCM lakini matokeo yake hata wenyeviti watatu wa mikoa hawakuambatana naye CHADEMA.
 
Inahitaji uwe na akili huru kujuwa mchezo unaoendelea ila CCM inajuwa kucheza na njaa za wanasiasa uchwara,kila maji yanapochemka wanadumbukiza bonge la barafu maji yanapoa.Wamefanya kwa uraisi na wabunge JMT na sasa yametimia Zanzibar.Nimemwelewa Kinana aliposema ukawa umebaki ukiwa.Kwa akili za kawaida huwezi kuona utaishia kutukana naiona miaka mingi mbele ya CCM kutawala Tanzania kukiwa na upinzani unaodhoofu.Mbaya zaidi wamewaacha watu wao kwa upinzani ili kuushauri na kuwa wasemaji wakuu,na hii inauweka upinzani kuwa na wasaliti/spy wengi kuliko kipindi kingine chote.Ni ngumu kuelewa kama hujuwi sayansi ya siasa.
 
Back
Top Bottom