GE2025 Kama kuna watu walizoea kutajirika, waambie Makonda anaingia kazini Oktoba 29

GE2025 Kama kuna watu walizoea kutajirika, waambie Makonda anaingia kazini Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,229
Naona jamaa ameshajihakikishia nafasi mapema, hadi ameanza kupiga mikwara watu mapema
=================
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema yuko tayari kupambana na mafisadi wote wanaowaonea wananchi wanyonge.

“Kama kuna watu walizoea kutajirika, waambie Makonda anaingia kazini Oktoba 29,” amesema Makonda.

Amesema hayo Alhamis Septemba 20, 2025 akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Soko la Morombo Kata ya Murieti.

 
Alikuwa RC kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama alifanya nini?

Leo awe mbunge tu atamwambia nani afanye nini?

Kwanza zile hela za ugomvi na Gambo walifikia wapi?
Anaamini kuwa yeye ni PM ajaye.

Apambane na Abdul pamoja na Rostam ambao ni mafisadi Papa kwanza bila kumsahau Mama Abdul na mzee wa Msoga aliye Fisadi nyangumi.

Lenyewe lijizi tu. Pumbavu zake.
 
Anaamini kuwa yeye ni PM ajaye.

Apambane na Abdul pamoja na Rostam ambao ni mafisadi Papa kwanza bila kumsahau Mama Abdul na mzee wa Msoga aliye Fisadi nyangumi.

Lenyewe lijizi tu. Pumbavu zake.
Atakuaje PM kama Nchi rafiki na wafadhili EU na US haruhusiwi kuingia?
 
Kwa ufisadi, inadaiwa na yeye yumo- hiyo kitaalam inaitwa self incrimination. Sasa ajiangalie na yeye kwenye kioo Kwanza Kama ni msafi kabla ya kuwapangusa wenzake kinyesi wakati kimetapakaa mwilini mwake kote.
 
Unaweza kutuelezea utajiri wake ameupataje ndani ya muda mfupi tu?

Magari na nyumba zake tu ukizijumlisha thamani yake haifananii na shughuli halali.

Tusidanganyane. Hakuna mkombozi mkombozi wa hili taifa zaidi ya raia wenyewe. Tukiwa wakali tukasuka katiba ya umoja wa kitaifa inayoweka mbele maslahi ya taifa hapo ndipo tutakuwa tumemaliza mzizi wa fitina.

Tukitengeneza katiba yetu vizuri hapo juu hata akikaa ng'ombe ataweza kuongoza inchi kwasababu kitakachotumika ni sheria na sio utashi wala matakwa ya mtu. Kwasasa tunaendeshwa na katiba yenye mtazamo wa chama yaani katiba ya chama kuongoza inchi.

Tunahitaji katiba inayohimiza sheria za wanainchi yaani raia kuongozwa kwa mujibu wa sheria na hiyo inaitwa ni katiba ya wanainchi.

Tunavyoendelea kusubiria mkombozi ndio tunavyozidi kuharibu na kupoteza zaidi.
 
Hata akiwa na akafanya bado si msafi na haaminiki tena maana ana vinasaba na kundi hatari la mafisafi wa nchi hii
 
Back
Top Bottom