Kuna mstari mwembamba unaomtofautisha Askofu Gwajima na Kibweteere

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
KABLA Joseph Kibweteere, kushawishi mamia ya wafuasi wa kanisa lake kuamini dunia ilikuwa mwishoni, kisha kusababisha vifo vya watu 778, Uganda, dunia ilishakuwa na madhehebu ya Heaven's Gate (Geti la Mbinguni).

Heaven’s Gate ni kanisa lililoasisiwa mwaka 1972 na watu wawili, wa kwanza ni Bonnie Nettles na Marshall Applewhite. Wakahubiri kuwa waumini wao wangefika mbinguni hai, wasingekufa. Kisha, mwaka 1985, Nettles (muasisi wa kanisa), akafariki dunia, kwa maradhi ya kansa.

Kifo cha Nettles, kilitosha kuwa somo kuwa kanisa hilo lilihubiri maono batili. Hata hivyo, wengine wakaendelea kuamini. Mwaka 1996, wanachama hai wa imani hiyo, walikutana kwenye jumba lao waliloliita kwa siri, Air Heaven (ndege ya mbinguni), mjini Rancho Santa Fe, San Diego, California, wakanywa sumu. Wakafa.

Walitarajia Air Heaven ingewapaisha mpaka mbinguni. Walijiua waende peponi ili dunia ipokee mamlaka mpya. Miili yao ilipogundulika mwaka 1997, ilikutwa na ujumbe uliosomeka: “Miaka yetu 22 ya darasani hapa kwenye sayari ya dunia hatimaye inafika mwisho. Tunafurahi kuiacha dunia na kuondoka pamoja.”

Kibweteere, yeye baada ya kukutana na mwanamke kahaba, Credonia Mwerinde, wakatangaza kuokoka. Credonia akajinadi kumpokea Yesu na kuacha kujiuza kimwili. Kibweteere, ambaye alikuwa na shida ya ubongo, kwa pamoja wakaanzisha kanisa waliloliita “Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God” - “Vuguvugu kwa ajili ya Urejeshaji wa Amri Kumi za Mungu.”
Miaka ya 1990, Kibweteere alitoa kitabu alichokipa jina “A Timely Message from Heaven: The End of the Present Time” – “Ujumbe wa Wakati Mwafaka kutoka Mbinguni: Mwisho wa Wakati Uliopo.” Kibweteere na Credonia, wakahubiri dunia imefika mwisho. Waumini wao wakaamini. Wakauza nyumba na mali zao zote, fedha wakampa Kibweteere. Kisha Kibweteere akawateketeza kwa moto. Yeye na Credonia wakakimbia.

KIBWETEERE MPAKA GWAJIMA
Anzia katika mafundisho ya Nettles na Applewhite, kisha Kibweteere, halafu msikilize Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima. Utapata kitu kimoja cha kufanana; ni kuwafanya waumini wao wawaamini na waishi kwa kufuata hisia zao.
Nettles na Applewhite, walijidanganya kuwa wao wangeingia peponi bila kufa. Wakashawishi waumini wao. Nettles akafa kwa kansa mwaka 1985, hakuna aliyeshituka. Applewhite akaendeleza imani. Naye alikufa na waumini wake kwa kunywa sumu.

Gwajima anazo hisia kuwa Waafrika wapo hatarini ama kuteketezwa au kuharibiwa mfumo wao wa kimaumbile na Wazungu, kupitia chanjo za Covid-19. Anatuhumu kuwa wanaotetea chanjo, ni wanufaika wa mgawo wa kifedha kutoka nje. Ametajwa tajiri namba tano duniani, Bill Gates.

Kupitia mahubiri kanisani kwake, Gwajima amewataka waumini wake wakatae chanjo. Akasema, chanjo iliyoletwa nchini ni tofauti na waliyochomwa Waingereza. Akaahidi kuwa yeyote atakayeshinikiza chanjo kutumika nchini bila kuthibitisha ina madhara gani kwa Watanzania, atakufa.

Tutungeneze matawi matatu; la kwanza, kwamba wanaoshawishi Watanzania kuchanjwa ni wanufaika wa fedha. Je, nani anashawishi? Rais Samia Suluhu Hassan, jana alizindua matumizi ya chanjo ya Janssen kwa Watanzania. Janssen, inatengenezwa na taasisi ya kimarekani ya Johnson & Johnson.

Je, anamtuhumu Rais Samia bila ushahidi wowote, kwamba ana malengo ya kuwasababishia madhara Watanzania kwa manufaa ya kifedha? Gwajima ni mbunge kupitia CCM. Rais Samia ndiye Mwenyekiti wa CCM. Je, ni kwa jeuri na kiburi gani, Gwajima anamtuhumu mwenyekiti wake wa chama chake?

Pili, Gwajima sio daktari. Kwa nini anaingilia mambo asiyo na utaalamu nayo? Tatu, kwa nini watumishi wengi wa Mungu wanapenda kutishia watu kifo? Desemba 2016, Kiongozi wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo, alitoa ahadi kwamba waliotoa habari za yeye kuwa mlevi wangekufa kabla ya Machi 2017. Hatujawahi kupata ripoti ya vifo.

Gwajima anapokuja na vitisho vya kifo, ni dhahiri anarejea ya Lusekelo ‘Mzee wa Upako’. Maneno ya vitisho kutoka kwa Yona kwenda kwa watu wa Ninawi, kwamba wangeangamia kama wasingetii neno la Mungu na kuacha maovu, wahubiri wa siku hizi wanayatumia vibaya. Ukimkosea yeye anakuahidi kifo. Ukiruhusu chanjo ya Covid-19 ili kuokoa maisha ya wengi, pia unaahidiwa kifo. Halafu katikati ya hiyo ahadi jina la Mungu linatajwa.

Neno la Mungu katika Biblia linasema “watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", wakati kwenye Kuran, kusoma imewekwa ni wajibu ili mtu mwenyewe aweze kutumia elimu na akili yake kuchanganua mambo. Waumini wanapaswa kujiongeza ili kuchuja yatokayo kwenye vinywa vya viongozi wao wa kiroho na kweli halisi yenye kumwelekea Mungu.

Huu ulimwengu una mabadiliko makubwa. Sayansi hudhibiti uongo. Dunia ya leo si ya mtu kuja mbele yako na kukueleza kuwa Ulaya kila mtu anamiliki Mercedes Benz. Dunia ya sasa ipo wazi mno. Ndio maana, Karne ya 19, mwanafalsafa wa Ujerumani, Karl Marx, alisema: “Maendeleo ya sayansi yanasaidia kuondoa uhalali wa utawala wa wafalme na nguvu za Kanisa.”

Mantiki ya maneno ya Karl Marx ni kuwa ulimwengu wenye maendeleo mazuri kisayansi, hulazimisha demokrasia kutawala badala ya wafalme kuendelea kushika hatamu. Vilevile, viongozi wa dini wenye kutumia porojo kama mtaji, hawawezi kufanikiwa kwenye dunia ya kisayansi.

Mathalan, Gwajima wa leo, hahubiri misukule kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Habari za kumfufua Amina Chifupa, zilishapoteza uhalali na zilifeli. Sayansi ilisaidia Watanzania wengi kutambua kuwa Gwajima aliahidi angemfufua Amina lakini alishindwa. Hata habari ya Gwajima na Edward Sokoine, iliisha kienyeji.

Hata haya maagizo yake kwa waumini wake kwamba wasikubali chanjo, yatapoteza nguvu kisayansi. Watu wakichanjwa na maisha yakiendelea bila matatizo, Covid-19 ikadhibitiwa nchini, mwisho itaonekana Gwajima alikuwa anahubiri yasiyokuwepo duniani wala mbinguni. Kama dhana ya misukule ilivyomshinda, au Amina ambavyo hakukufuka.

Bado kuna yale maono yake ya kugeuza misikiti kuwa Sunday Schools. Akaahidi yeye ni mbeba maono na hatakufa kabla hajatimiza hayo. Mahubiri ya shari kabisa. Siku alipoutamani mlango wa siasa, akajiita Rashid. Udini!

CHANJO YA JANSSEN
Janssen ndio chanjo iliyozinduliwa kwa ajili ya Watanzania kuchanjwa. Wakala wa Dawa Ulaya (EMA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) Marekani, wamethibitisha kuwa Janssen ni salama. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), nalo limeridhia Janssen itumike. Wataalam wa Umoja wa Afrika (AU), wamejiridhisha kwamba ni salama.

Ufanisi wa chanjo ya Janssen ni asilimia 85.4 mpaka 93.1 hadi kwa watu wenye magonjwa sugu na wanaokuwa wamelazwa. Katika kila watu 100,000 wanaochanjwa, hutokea kesi zisizozidi nane za kuzimia. Hiyo ni asilimia 0.008. Hapo ni sawa na hakuna.

Inashauriwa kwa watu wenye matatizo ya mzio (allergy) na sindano za chanjo, wasichanjwe. Kwa ambao hawana shida ya allergy, kwao ni ruhusa kuchanjwa, maana ni salama.

Kuhusu kesi za kuzimia; kwa mujibu wa chapisho la Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga (CDC), mtu anapochanjwa Janssen, anatakiwa kupumzika kwa angalau dakika 15, hapo itakuwa rahisi kuepuka kuzimia.

Credit: Luqman Maloto
 
Hata hivyo watu kama gwajima wanatakiwa wawepo ili chanjo itoshe. Kama wote tungeinadi na kuihitaji chanjo basi isingetosha. Tanzania inawatu milion 60 na chanjo ni milion1. Tunahitaji watu kama gwajima 1000 ambao watashawishi watu 59000 kila mmoja ili wanaobaki ndo waendane na idadi ya chanjo iliyopo. Mi nasema tena gwajima hajatosha. Tunahitaji watu wengi zaidi ya aina yake ili tuendane na idadi ya chanjo
 
Watu wanajifunza kutoka mataifa mengine,watu wana network ambayo mwingine anaweza kua hana,Gwajima si punguani,yamkini anaye mponda hana hata uwezo wa kuwafanya watu sita tu wamsikilize ila yeye ana watu karibu elfu tatu wamfuatao nyuma kuonyesha wazi kuna kitu ndani yake, watanzania tumezoea kusifia na kufuata maneno kama ya kina Malcon X au wengineo wa huko Ulaya na kudharau wa nyumbani mwao.

Zaidi ya yote presha ya Covid-19 ni ya wazungu na wanalazimisha taharuki iwe ya dunia yote, huku Uswahilini kwa 90% hakuna Covidi-19 tusidanganyane na kutishana
 
Dalili moja ya manabii fake ni kutoa vitisho. Wanatumia vitisho ili watu wawaamini!!!!
 
Watu wanajifunza kutoka mataifa mengine,watu wana network ambayo mwingine anaweza kua hana,Gwajima si punguani,yamkini anaye mponda hana hata uwezo wa kuwafanya watu sita tu wamsikilize ila yeye ana watu karibu elfu tatu wamfuatao nyuma kuonyesha wazi kuna kitu ndani yake, watanzania tumezoea kusifia na kufuata maneno kama ya kina Malcon X au wengineo wa huko Ulaya na kudharau wa nyumbani mwao.

Zaidi ya yote presha ya Covid-19 ni ya wazungu na wanalazimisha taharuki iwe ya dunia yote, huku Uswahilini kwa 90% hakuna Covidi-19 tusidanganyane na kutishana
"Presha ya covid wazungu wanalazimisha kivip and how?
as far as concern hakuna mahali wamandika nchi fulani isipotumia chanjo watakula sanction au kutengwa kimataifa.

ni nchi husika serikali na serikali zao wanaomba wenyewe.. na nchi zingine wananunua kabisa..

Kuna na network kubwa hapa duniani hakukufanyi uwe smart kuliko wengine.. after all ni nothing special coz dunia ni kijiji sikuiz.. mawasiliano yame kuwa kwa kasi so ni rahis watu kupata taarifa..


the only difference hapa unapata taarifa kutoka kwa nani.
 
KABLA Joseph Kibweteere, kushawishi mamia ya wafuasi wa kanisa lake kuamini dunia ilikuwa mwishoni, kisha kusababisha vifo vya watu 778, Uganda, dunia ilishakuwa na madhehebu ya Heaven's Gate (Geti la Mbinguni).

Jamaa halafu anasema anafufua wafu mbona mbona kashindwa kumfufua yule mwenzake wa Nigeria kalala mpaka leo hajaamka?
 
Kuna mambo kadhaa ya MSINGI na UKWELI umeandika lakini pia kuna UZUSHI
1.Kuhusu extremist za kidini na kuwaaminisha Uongo hususan kufufua waliokufa hiyo ni UKWELI.
2. Kuhusu akina KIBWETERE na wengine uliotaja ni UKWELI
3. Swala la Uhakika wa CHANJO ni UZUSHI, maana si Gwajima tu anayelalamika ni issue ya dunia. Si USA au UK na sehemu kadhaa za Afrika nako wanakataa.
4. Kuhusu proffesionalism za Udaktari ni UZUSHI kuna prof wa NimR mwaka jana kwa hiyo professional aliyo nayo alisema Chanjo si za KUAMINI maana zilihitaji utafiti usiopungua miaka 15, na kufanya study kadhaa lkn hizi zimepatikana chini ya mwaka na kuanza kutumika
Mwaka huu amesema ziko safi ziko salama.
Swali mtu wa namna hii hata kama ni daktari utamuaminije? Ana kuletea hisia na kukulazimisha uamini ni munufaika.
 
Mkuu, mambo ya kiimani Ni mazito, rahisi Kama wewe unavyoyachukulia.

Iliyobaki wewe usiekuwa na imani baki na msimamo wako kwanini upate shida na imani za watu? Kwani chanjo Ni lazima?

Hata unajaribu kurefer maandiko ya imani za wenzio , bado Kwakuwa so imani yako Wala huelewi vizuri , unapika majungu yako tu.

Kwani unafikiri neno la Mungu linaposema 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, wewe unadhani Ni maarifa ya wanasayansi?
Soma vizuri..
Hosea 4 : 6

'Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. '

Tena katika mambo ya kiimani hatutakiwi kutegemea kitu chochote zaidi ya Mungu, si wanasayansi, si elimu, si akili zetu, Soma..

Mithali 3 : 5
'Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; '
 
Jibuni hoja za Gwajima, sio kumthiki na kumtuna, kinyume na hapo nyinyi ndio akina kibwetere.
Hivi ni Gwajima pekee anae pinga hizo chanjo?
Mbona iko wazi mpaka huko duniani (Marekani na ulaya kwa ujumla) zina pingawa?
Ushahidi, Raisi wa Marekani ameamua kutoa hongo ya dollar 100 kwa raia atakae kubali kuchanjwa.
Bro hii sio nyakati ya Nyerere, yakuangalia habari kwenye tivii kisha kuwaongopea wazee wetu eti ameota ndotoni.

Nb. Chanja chanjo, mimi nachanja mbuga.
 
"Presha ya covid wazungu wanalazimisha kivip and how?
as far as concern hakuna mahali wamandika nchi fulani isipotumia chanjo watakula sanction au kutengwa kimataifa.

ni nchi husika serikali na serikali zao wanaomba wenyewe.. na nchi zingine wananunua kabisa..

Kuna na network kubwa hapa duniani hakukufanyi uwe smart kuliko wengine.. after all ni nothing special coz dunia ni kijiji sikuiz.. mawasiliano yame kuwa kwa kasi so ni rahis watu kupata taarifa..


the only difference hapa unapata taarifa kutoka kwa nani.
Kuzuia watu Hijja sio sanction?
 
Back
Top Bottom