Kama Kanisa linafungamana na Serikali mpaka linashindwa kukemea maovu, kuna haja ya kuendeleza Sakramenti ya Kitubio?

Ndio maana siku hizi nimeamua nisali nyumbani sadaka nipeleke kwa wenye uhitaji.
 
kwanini unataka kanisa kuanza kuingilia mambo ya serikali?,
kwanini unasema kanisa wakati tuna madhehebu mengi?,
hii nchi si ya kidini,nijuavyo,tusipende kutumia dini au imani kwenye kukemea mambo ya kisiasa;

Mbona wakati wa Kikwete kila mara kanisa lilikuwa linatoa waraka?

Kwani mitume na manabii wa zamani walikuwa hawakemei serikali? Hao viongozi wa serikali si ndio waumini wenyewe?
 
Padri anapoadhimisha sacramenti yoyote na kwa kuzingatia kuwa Kanisa ni la waumini wakosefu na wakatifu (yaache magugu yakuwe pamoja na ngano) linatumia kanuni hii ambayo kwa Kilatini inasema: 'ex opere operantis' - yaani muumini anapopokea sakramenti anapokea neema ya Mungu na si kwa stahili ya mtu (padri) anayeitoa. Hata kupokea sadaka za waumini kunafuata mantiki hii kwa sababu hakuna anayejua 'worthiness' ya mtoa sadaka au lengo lake ila ikishatolewa padri naye anaipokea sadaka kwa kuamini kwamba ni kwa ajili ya Mungu.

Sijakasema hawapaswi kusimama imara, nilichosema ni je kama wameshindwa then hata sakramenti wanazotoa zimeshindwa/hawawezi kuzitoa tena? Mimi nasema hapana. Hata kama wameshindwa bado Mungu anaweza kuwatumia. In the circumstances, hata kama kiongozi ni useless sacramenti anayotoa ina nguvu ya kuokoa/kuponya kupitia yeye. Ndiyo maana ya dhana ya 'ex opere oprerantis'.

Unampataje sacrament mtu dhalimu ambae KILA siku urudia dhambi hizo hizo za kumkufuru Mungu kwake sacrament Ina haja gani Kama ajui nn maana ya sakrament huoni hapo ni sawa na kumkufuru Mungu.
 
Kanisa haliwezi kukurupuka kama wewe ulivokuja na ki thread uchwara hapa!!!
 
Unampataje sacrament mtu dhalimu ambae KILA siku urudia dhambi hizo hizo za kumkufuru Mungu kwake sacrament Ina haja gani Kama ajui nn maana ya sakrament huoni hapo ni sawa na kumkufuru Mungu.
Yaani recipient wa sacramenti inatosha tu kuamini kuwa sacramenti ameipata kutoka kwa right source - minister of the church. Hata wewe hapo ulipo sidhani upo kwa vile wewe ni mtakatifu, bali inatosha tu kwa wale wanaokuamini kwamba wewe ni muumini mzuri na wanafanya kila kitu kwa kuamini hivyo hata kama wewe ni "bure kabisa". NB: hapa 'bure kabisa' ni mfano tu na simaanishi kwamba wewe ni 'bure kabisa'!
 
Unapoenda kuungama,si unaungama kwa kutumia maneno ya JUMLAJUMLA, huwi SPECIFIC, mfano kama ulimpiga Lisu, husemi kwa padri kua ulimpiga Lissu risasi, wewe unasema tu, nilijeruhi unaishia hapo tu, then unaondolewa dhambi bila ya kumtaja uliyemjeruhi.
Mungu siyo bwege kiasi hicho , ondoleo la dhambi siyo rahisi kiasi hicho
 
Back
Top Bottom