Kama Kanisa linafungamana na Serikali mpaka linashindwa kukemea maovu, kuna haja ya kuendeleza Sakramenti ya Kitubio?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,405
30,908
Ndugu zangu wakatoliki hebu tulitafakari kanisa letu kwa hii miaka mitano namna lilivyoshindwa kukemea maovu mbalimbali yaliyofanywa na serikali je Kuna haja ya kwenda kutubu kwao Kama zamani au ndio Hawa masnichi watatuchoma na kuuza madhaifu yet kwa watesi wetu?

Ukiona viongozi wa kanisa wanacompromise na state ujue hamkani si shwari Tena.
Imagine mfano Lissu akaungame kwa Pengo!

Kwakweli kanisa limetuangusha mno Kama waumini wake. Japo binafsi nilishaachana na hilo kanisa.

Mkulungwa makusudi
 
Ndugu zangu wakatoliki hebu tulitafakari kanisa letu kwa hii miaka mitano namna lilivyoshindwa kukemea maovu mbalimbali yaliyofanywa na serikali je Kuna haja ya kwenda kutubu kwao Kama zamani au ndio Hawa masnichi watatuchoma na kuuza madhaifu yet kwa watesi wetu?...
Wanaogopa mkuu..

Askofu Severine Niwemugizi alikemea, akaitwa ofisi ya uhamiaji akaambiwa siyo raia.

Alipokanusha tuhuma akaamriwa kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa:
Chake,
Cha baba ake
Cha mama ake
Cha babu
Cha bibi..

Viongozi wa dini nao wamelazimika kuwa "wanyonge" Kama raia wengine
 
Unapoenda kuungama,si unaungama kwa kutumia maneno ya JUMLAJUMLA, huwi SPECIFIC, mfano kama ulimpiga Lisu, husemi kwa padri kua ulimpiga Lissu risasi, wewe unasema tu, nilijeruhi unaishia hapo tu, then unaondolewa dhambi bila ya kumtaja uliyemjeruhi.
 
Wanaogopa mkuu..

Askofu Severine Niwemugizi alikemea, akaitwa ofisi ya uhamiaji akaambiwa siyo raia. Akalipokanusha tuhuma akaamriwa kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa:
Chake,
Cha baba ake
Cha mama ake
Cha babu
Cha bibi..

Na wao wamelazimika kuwa wanyonge Kama raia wengine
Halafu cha bibi akakitoe wapi wakati hata Mwakyembe wakati wa sakata la ndoa na cheti za kuzaliwa, aliambiwa pengine hata yeye hana cheti cha kuzaliwa..!!
 
Unapoenda kuungama,si unaungama kwa kutumia maneno ya JUMLAJUMLA,huwi SPECIFIC,mfano kama ulimpiga Lisu,husemi kwa padri kua ulimpiga Lissu risasi,wewe unasema tu,nilijeruhi unaishia hapo tu,then unaondolewa dhambi bila ya kumtaja uliyemjeruhi.
Kweli Religion is Opium of Man..yani na akili zako unaenda kuungama mbele ya mwanadamu mwenzako..tena hawa hawa wenye mapungufu kama yako...Kuna namna ya kutafakari upya hizi imani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama unachukizwa na huu udhalimu wa kutisha unaoendelea Nchini na nyumba ya ibada unayoenda kuabudu iwe kanisani au msikitini viongozi wake wako kimya kabisa na wengine hata kuthubutu kuwasifia hawa wadhalimu, kwanini uendelee kuhudhuria nyumba ya ibada inayoongozwa na viongozi WANAFIKI!? 😳
 
Kweli Religion is Opium of Man..yani na akili zako unaenda kuungama mbele ya mwanadamu mwenzako..tena hawa hawa wenye mapungufu kama yako...Kuna namna ya kutafakari upya hizi imani.

#MaendeleoHayanaChama
Rejea Reform 1571
 
Niseme tu hili sio kanisa aliloacha Kristo kupitia mtume Petro.

Kanisa la kweli halifungamani na wadhalimu. Kanisa limepwaya, Ukristo umepwaya kwa kuendekeza maslai ya dunia thus wako radhi kuwakaribisha watu dhalimu Hadi kwenye madhabau ya Mungu. Laiti Kama kanisa lingewatenga watu dhalimu ikiwemo kuwafuta hata uumini ingeweza badili mioyo yao. Ulegezi wa kanisa ndio umechangia kuzaliwa kwa madikteta.

Check mfano nkurunziza jumapili yupo kanisani anaimba kwaya anapewa mimbari ahubiri week days anauwa watu. Kanisa linafaa lipinge udhalimu lijitenge na madhalimu wanaobomoa misingi ya utu. 90% ya madikteta ni wakristo sababu kanisa la sasa limeacha misingi ya Ukristo na kufunga ndoa na maslai ya dunia.
 
Rejea Reform 1571
Mi nilishaga achaga huo upuuzi..mana hakuna kitu kama hicho kwenye maandiko matakatifu..hayo ni mapokeo ya wanadamu ili kujivika ukuu,heshima na utukufu..

Dhambi zako Mweleze Muumba wako atakusamehe kupitia jina La Yesu Kristo.

Over

#MaendeleoHayanaChama
 
Ndugu yangu kama hulijui kanisa katolik kwenye maslah linakuaje, angalia ccm inaendeshaje mambo yake, ni C&P

kama huijui ccm basi angalia kanisa katoliki, no C&P
 
Mitume hawakutegemea sadaka wala fungu la kumi la mtu ili waishi, ndiyo sababu walikemea maovu.
So means wakikemea uovu watakufa njaa.
Naamini siku waumini wakigoma kutoa sadaka na michango wakashinda njaa watakemea.Shida kwao maslai ni muhimu
 
Back
Top Bottom