Kama JF ni ya CDM je CCM hawarusiwi kuchangia hoja!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama JF ni ya CDM je CCM hawarusiwi kuchangia hoja!??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Imnyagi, May 11, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. I

  Imnyagi Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku kadhaa zilizopita kumekuwepo na madai kwamba JF ni ya CHADEMA na inatumika kuishambulia serikali iliyoko madarakani na wana chadema wenyewe lakini kuna maswali najiuliza hivi kama kweli JF ni ya chadema kuna mahali wakati wa kujisajili humu ndani lazima sehemu ya chama? Sijaona na kama hakuna ina maana kila mtu ana uhuru kujisajili na kutoa mawazo yake bila kujali ni wa aina gani na ni wa itikadi gani ili mradi tu anafuata taratibu za JF.

  Napata shida kuelewa hizi kelele ni za nini wakati ccm kama wanaweza kuwahonga fulana kofia na kanga na kuhudhuria mikutano yao hata kama hawapendwi wanashindwa nini kuwakusanya wanachama inaowaamini na kuwanunulia simu za Blackberry na laptop ili waendeleze biashara ya Tambwe Hizza humu ndani matokeo yake wanakurupuka wakitaka waonewe huruma maana humu ndani ni home of Great Thinkers na wao sio kundi hilo wako wachache humu ndani lakini hawana nguvu kutokana na uwezo wao wa kufikiri na wanachadema wenye kujua kuchambua mambo kiundani tena bila woga wanakereka na kurusha tuhuma zisizo na maana kwa chama cha miaka mingi lakini hakijifunzi na kusoma alama za nyakati badilikeni jamani!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...