Kama Jeshi la Polisi linafanya juhudi kubwa kumtafuta mtu anayedaiwa kumpa sumu Mangula, ni kwanini halifanyi juhudi hizo kwa waliompiga risasi Lissu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Tumemsikia kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum wa Dar, Lazaro Mambosasa akielezea kuwa kutokana na taarifa walizozipata kutoka vyombo vyao vya usalama, wamebaini kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, alipatikana na sumu mwilini mwake, iliyosababisha aangukuke ghafla kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM na kusababisha akimbizwe hositalini Muhimbili na akaahidi kuwa Jeshi hilo litawasaka kwa nguvu zote, watu wote waliohusika na Uhalifu huo

Tunalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua ya haraka mno, ya kuwasaka hao watu ambao wanadaiwa walitenda kosa hilo la jinai.

Hata hivyo ninavyofahamu mimi ni kuwa wajibu namba moja wa Jeshi la Polisi nchini, ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Ninacholiomba Jeshi hilo la Polisi ni kuwa juhudi hizo wanazozifanya katika kuwasaka watu waliofanya jaribio la kutaka kutoa uhai wa makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Mangula, juhudi hizo hizo wazifanye kwa waliotaka kutoa uhai wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu, waliofanya jaribio la kutaka kumwua, kwa kumminia risasi 16 kwenye gari lake, ambazo zilimwingia mwilini na hivyo kulazimika kukimbizwa nje ya nchi, ambako anaendelea na matibabu, zaidi ya miaka miwili hivi sasa

Vilevile, ningewaomba Polisi hao wafanye juhudi hizo hizo kwa kuwasaka waliomuua, Mwenyekiti wa Chadema, wa mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, zaidi ya miaka mitatu hivi sasa.

Jeshi la Polisi halipaswi lifanye ubaguzi katika matukio ya uhalifu nchini, kwa kuangalia ni nani amefanyiwa, kama ni kiongozi wa CCM juhudi kubwa zinafanyika, lakini kama ni kiongozi wa Chadema, haufanyiki uchunguzi wowote!

Tunajua kuwa Jeshi hilo linagharimiwa na walipa kodi wa nchi hii, bila kujali itikadi zao za kisiasa, hasa tukitilia maanani kauli ya mara kwa mara inayotolewa na Rais Magufuli kuwa maendeleo hayana chama.
 
Hii ya sumu ni geresha ili kuwasingizia baadhi ya watu ndani ya CCM na kuwabambikia makosa na kuwachafua kisiasa. Hasa wale wanaompinga bwana mkubwa. Michezo ya uchaguzi 2020.

Nadharia za power zinasema kuwa mtafute adui na ukikosa mtengeneze. Kisha waaminishe wafuasi wako kuwa kuna adui ambaye ni wewe tu unayeweza kumdhibiti.
 
Duh! Jambo limezua majambo!
Tunataka kama kweli Jeshi letu linafanya kazi kwa weledi, basi lisifanye ubaguzi katika kushughulikia masuala ya uhalifu

Ni dhahiri kwa mwenendo tunaouona sasa, Jeshi letu linafanya upendeleo wa wazi kwa viongozi wa CCM, huku likiwaacha bila msaada wowote viongozi wa Chadema.
 
Hivi kwanini ni Lissu tu ndio inaonekana hajatendewa haki? Je sisi huku tusio na umaarufu wala uwezo nasi vp?

Kama na wewe ulionewa sema tu ili usikike, pia Lissu ni Mwana Siasa maarufu sana jumlisha na Tukio lililompata na namna lilivyo chukuliwa na wenye Dhamana.Tuta Hoji tu Vizazi na Vizazi.
 
Mi nadhani swala na mh.Tundu A.Lisu analicherewesha mwenyewe swala lake! Siku akirudi lazima wakamatwe police ya tz nawaamini sana.

Una waamini kwa kuvunja na kuchukua Haki za Raia wengine ,sio !!?.
 
Policcm kama alivosema Katibu wa ccm Bashiru
tapatalk_1583577109778.jpeg
 
Hii ya sumu ni geresha ili kuwasingizia baadhi ya watu ndani ya CCM na kuwabambikia makosa na kuwachafua kisiasa. Hasa wale wanaompinga bwana mkubwa. Michezo ya uchaguzi 2020.

Nadharia za power zinasema kuwa mtafute adui na ukikosa mtengeneze. Kisha waaminishe wafuasi wako kuwa kuna adui ambaye ni wewe tu unayeweza kumdhibiti.
Kwa hiyo kama kawaida yao, hao CCM wakishirikiana na Jeshi "lao" la Polisi, wanafanya mpango wa kutaka kuwabambikia kesi "wabaya" wao!
 
Back
Top Bottom