Kama ingekutokea wewe ungefanyeje?

Inabidi uwe mjanja sana kama kweli huo ni babake mdogo kuna maneno hawezi tamka juu ya mtoto wa kakake ambae sawa na kusema wake... Na pia wadada hasa hizi dot com wajanja sana sidhani kama ni mjinga kiasi cha kutumia simu ya babake mdogo...
 
Nikwambie rafiki yangu, hako kabinti kanataka kukupiga kekundu. Hivi kaka kwani we unaogopa nini wakati nyie tayari mmeshakuwa wa2 wazima? We kama huyo kidume akikupigia cm hamuna haja ya kumficha we mweleze ukweli tu. Kuwa makini sana na hawa dada ze2 kwani mara nyingi c wakweli.
 
Inabidi uwe mjanja sana kama kweli huo ni babake mdogo kuna maneno hawezi tamka juu ya mtoto wa kakake ambae sawa na kusema wake... Na pia wadada hasa hizi dot com wajanja sana sidhani kama ni mjinga kiasi cha kutumia simu ya babake mdogo...

Mh! kweli asha d, hapo umenifungua akili ngoja ni waskize werevu wengine wana semaje
 
Salaam wakuu kuna kisa kimenitoke ila nakosa namnaya kukikabili, Nina mpenzi wangu nipo nae huu mwezi wa 9 sasa, yeye yupo moshi mimi nipo arusha maranyingine yeye huja arusha na mimi kwenda moshi, kamliza masomo yake ila bado hajapata kazi yupo nyumbani umri ana 21yrs... Sasa jana kanipigia simu kuwa baba yake mdogo alimuazimisha simu ndipo akakuta msg yangu kwenye simu yake, baada yakuona hyo msg baba mdogo akaenda kumwambia kaka yake ambae ndio baba yake na mpenzi wangu. Baba akakasirika na kumwita alipomuuliza akajibu mimi ni rafiki yake ambae tulisoma pamoja, kutokana na hiyo msg kutokudhihirisha wazi kama mimi ni mpezi wake ikabidi wa mwache. Sasa leo asubuhi kaniambia kuwa amesikia tetesi kuwa baba yake mdogo amesema atanipigia simu naatajifanya yeye ni mpenzi wake kwahiyo mtu akinipigia simu na kuniuliza kuhusu yeye nimjibu kuwa mimi ni rafiki yake tuliesoma wote.. TATIZO nilishapataga tetesi kuwa huyu binti ana mwanaume mwingine ila sijamuuliza kwakuwa nilikuwa bado nakusanya ushahidi. WASIWASI huenda huyo mwanaume ndio aliekamata hiyo msg na akamletea noma, sasa huyu binti anataka kutuliza noma asimkose huyo mwanaume na asinipoteze mimi ndio maana akawahi kuni set, na namba zahuyo jamaa kanipa pamoja na jina. Je, nifanyeje iliniujue ukweli?? msaada wanajf

ndugu,

ningekuwa mimi ni wewe, na ningekuwa ninampenda huyu binti na ninataka kumwoa. ningekubali ushauri wake, ila ninge fanya kinyume cha maelekezo yake. kama ninataka kumwoa , manake kuna siku nitawasiliana na huyo baba, so ni bora wewe ukubali kuwa ni mpenzi wake, na umwambie kuwa upo ktk maandalizi ya kutaka kuja kujitambulisha, kama kweli ni baba yake , ataona aibu, lakini kama ni mume mwenzio, utakuwa umemfukuza na wewe utamiliki nanihii

tahaddhari,

yawezekana binti au huyo mwanaume au huyo baba nae yupo hapa JF , tafakari, chukua hatua mapema
 
Hakuna mzazi anayeweza kumfatilia msichana mkubwa kama huyo we nyamaza 2 kimya hadi atakapo piga sim na akikuuliza mwambie ukweli kwan huyo sio mtoto utapata jibu. pole sana:mod:
 
Hapo kana 21yrs tu kameshakuwa kataalam ka kudanganya hivyo.. kakifika 25yrs si itakuwa balaa..
 
Kundas.bado hujapata ushahidi wakukufanya umtuhumu.kwahiyo nafikiri jaribu kumuamini ila b eyes
 
ushaliwa kitambo for sure hiyo number ni ya kidume chake kingine.
tangu lini baba mzazi aanze kuingilia mapenzi ya mwanae na kusoma msg zake ilihali ni mtu mzima?
hapo hakuna cha dingi mdogo wala baba mzazi huyo ni bazazi tu anaewania tunda na wewe.
huyo msichana sii mwaminifu anajua keshagonganisha magari ili kujinasua kaamua kusuka hoyo ishu..
Man wanawake wana akili sana.Wakati nasoma chuo kuna msichana alikuwa na wavulana
wawili wa chuo na wa mtaani.Yule wa mtaani akatambulishwa kwa yule wa chuo kuwa ni Binamu
yake jamaa kakubali mwishowe akashtuka anaachwa bila taarifa wkt alishamtambulisha hata kwa
nduguze kama mchumba.Kuwa macho
 
Nashukuruni sana kwa ushauri wenu wapendwa hakika hakuna kama jf wote mlio nishauri nimependa ushauriwenu, bado napenda kusikia meng kutoka kwenu.. Ukwel huyu binti nampenda sana na nina malengo nae. Ila ndo hvyo kidudu mtu kimeingia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom