TUTUMIE HUU MUSWADA WA 'RUZUKU SHITIRISHI KWA VIONGOZI WASTAAFU' KUJENGA TABAKA LA STATESMANSHIP NCHINI KABLA GHARIKA HAIJATUKUMBA HAPO MBELENI
Ni kweli wazee wetu wamefanya kazi kubwa sana huko nyuma hivyo kustahili kwao KUSHITIRISHWA UZEENI, lakini hilo kamwe lisifanyike bila kuweka vigezo na
(1) mipana itakayomlinda mlipakodi wa wakati ujao,
(2) kuneemesha wazee bila kulipa MISHAHARA KAMA YA RAIS atakayekwepo madarakani kwa watu ambao tayari wameshatundika daluga (ni posho ya ushitiri na wala si mshahara), hadi kwenye mipaka ya maana ya familia ijumuishayo Baba, Mama, na Watoto wa ndani ya ndoa waliotambuika kisheria siku ile alipokua anaagwa kwenda nyumbani tu.
(3) Kulinda haki za vyama vya siasa hasa vile vinavyochipuka ili visikumbwe na uwanya wa siasa wenye mabonde mengi na milima huku WASTAAFU hao wakionekana kurandaranda tena mitaani kunadi wengine na kujiharibia sifa hasa pale ambapo kunatokea mauaji kama ambavyo kule Igunga tulikowaon.
Mpaka hapo hakuna ubishi kwamba hali hii ikiachwa kuendelea zaidi basi tujue inanyima mgombea wa chama changa uwanja mzuri kuchezea kisiasa kiushindani zaidi (matokeo yake hujenga chuki dhidi ya wazee) kwa kuwa mshindani wake ambaye tuchukulie ni wa chama tawala atakua akipata faida ziadi kutoka kwa wastaafu wetu ambao watamhangaikia kushoto kulia kwa kutumia zile zile fedha ambazo walipakodi wa vyama vyote watakua wamejinyima kimaendeleo na kuamua KUMSITIRISHA NAYO UZEENI kwa heshma ya utumishi kwa taifa.
Kwa lugha nyingine ni kwamba lazima tuweke kwenye muongozi wa MARUPURUPU SHITIRISHI KWA VIONGOZI WASTAAFU wazima piaa ikawavunie walipakodi taswira njema ya kuwepo na tabaka la WAZEE WA TAIFA WANAOWEZA KUTEGEMEWA NJE YA TOFAUTI ZA KIITIKADI za kidini na kisiasa pindi tunapojikuta kutokuelewana sisi vijana wao. Leo hii kukitokea jambo zito tuseme kati ya CDM na CCM ndio tunakimbilia kwa Mze Mashishanga aliyediriki kupanda jukwaani kutakia mbaya chama kimojawapo, aau ndio tunaenda kwa Mzee Edwin Mtei, Benjamin Mkapa au Sir George Kahama?
Jamani tukubaliane kwamba tuliosea sana kutoweka mazingira y kisheria sio tu inayowashitirisha ka Mzee Timothy Apiyo, Hawa Ngulume, Nickodemus Banduka, na sasa Ole Njolay, Babu Shirima na Mzee Yussu Makamba ... bali kubwa zaidi ni kwamba kwa choyo zetu tu tumeshindwa kisheria kujenga tabaka la wazee wastaafu ambao tunaweza TUKAWAMILIKI KWA PAMOJA, tukawa na sababu za kuamini neno lao hadharani au siri, na tukapaatanishwa bila kuhisi hata chembe cha U-ITIKADI kupita hapo katika katika.
Hakika inaweza ikaniyima raha sana kusikia eti Jaji Mkuu Mstaafu anaadi mgombea wa TLP eti yeye ni mwana TLP. Ninachosema hapa ni kwamba enda Jaji huyu atapenda kuendelea kutumia HAKI yke kikatiba kogombea kitu na pengine kuja kuwa wziri wa sheria na katika (Mama Kombona hii ni nadharia kujengea hoja hapa) ni ruksa lakini asipasate ruzuku shitirishi sawa sawa Jaji Mkuu mstaafu Samatta ambaye yeye kajiamulia kwamba ndio basi tena yeye harudi kwenye mambo ya kiitikadi za kisiasa bali ni kwamba kachagua kuingia kwenye tabaka adimu nchini la STATESMANSHIP basi.
Tabaka hili ni adimu sana watu kutulia mle; Mzee Mwinyi Kashindwa, Mzee Mkapa hivo hivo na Mzee Kingunge hasikii na Mzee Makamba ndio usiombe. Hakika tbaka hili kukosekana kwake nchi jirani Kenya napenda kujiaminisha kwamba ndio sababu kuu iliweza kuwafikishaa kwenye kuchinjana kama kuku hivyo wenzetu wenye mswadaa huu tafdhali tupa mipaka yetu ya kuona mambo na tuonyeshe ubunifu kucheza naa sheri hii ili itufae si kwa kulipana tu bali pia kwa kutufanya tuwe salama zaidi kama jamii moja.
Hebu imagine leo Mtumishi wetu Mstaafu Usalama wa Taifa Mzee Apson atakapoanza kusema yeye ni CHADEMA damu au yeye ni CCM Lowassa mpaka hpo mwenzangu unaona nini upande wa pili wa klivati? Haiwezekani tukaendekeza ITIKADI ZA KISIASA kiasi hicho kiasi cha kutunyima TABAKA LA STATESMEN hata huko kwenye taalum; ni aibu sana kusikia kila waongoza fikra kama Dr Banna kusema eti yeye ni CCM Mwandosya damu - mambo yakiharibika nawauliza Wazee Waitara, Askofu Laiser na Mboma, Wa-Tanzania tukaawakimbilieni huko huko kwenye chama kimojawapo?? Take a minute a think about it seriously.
Tabaka hili la Positive and most Active STATESMANSHIP, tangu Mwalimu Nyerere atutoke huko kubakia wachache tu kama vile Mzee Sabodo, Jenerali Ulimwengu, Prof Shivji, Mzee Warioba, Maria Nyerere, ambao ajabu ni kwamba wengine tunashinikiza afukuzwa uanachama wake wa zaidi ya miaka 42 eti kwa sababu tu katenda jambo lenye faida kwa kikundi kingine cha Wa-Tanzania lakini kwa kosa la kwenda nje ya mipaka ya kichoyo ya itikadi.
Wana-JF wenzangu, tujadili miswada hii kiundani zaidi leo ili tukwepe DOWANS za kesho huku tukiendelea kutafuta kuwasulubu wakwapwaji wetu wa sasa ambao hivi sasa tunawaona wakimwaga hela makanisani nchi nzima huku nikishindwa kujiondole mawazo kwamba HUENDA IKAWA NDIO SEHEMU ya yale malipo yasiona baaraka kwa Richmond ambazo huenda hivi sasa ndio zinatafuta kubaarikiwa kwa nguvu huko kwenye midhabahu zetu.