Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 21,657
- 46,837
Pole sana.Wengine tushaathirika kabisa na malezi ya manyanyaso ya utoton,mi nakumbuka nikiwa kwa bibi nachunga ng'ombe nimechoka nina njaa kali narudisha mifugo home ghafla kaka(mtoto wa uncle) kanivuta na kunisukumiza kwenye mzinga wa nyuki,kiufupi ni rehema za Mungu maana ningekufa.Nilijenga chuki na kaka mpaka tunakua tunapata kaz tunakuwa na miji yetu nilishindwa kuachilia ile chuki(kafa mwaka Jana kwa kudondokewa na mti,I swear hakuna MTU aliyelia kwa maumivu na uchungu kama mimi..... sijui kwann but nililia mpaka nikaumwa na kupelekwa hospital maana tumbo lilikaza nikashindwa kutembea kabisa) Since miaka hiyo naaminigi wanaume ni katili sana(I was just 9 years only) TUSIWAACHE WATOTO MBALI NASI TUWALEE . ...Nimeanza kuishi na mama nikiwa na 11
Yes...from To yeye 😜Pole sana.
Ndio maana ukajiita beesmom??
Anhaa kumbe umebadili jina mmanyani gwangu.Yes...from To yeye 😜
Ee kalumbu🤣Anhaa kumbe umebadili jina mmanyani gwangu.
Mimi hapo kwenye kufoka...ni hatari na nusuNi rahisi sana kujua kuwa una matatizo ya kitabia yanayotokana na makuzi yako ya utotoni maana tabia hazianzii kuharibikia ukubwani.
Mfano, leo hii mabinti na vijana wengi katika mahusiano unaweza kuwatambua kuwa si wazima kutokana na tabia zao.
Mfano. Binti kuomba sana pesa na kufosi kupewa mahitaji ambayo si stahiki yake maana si mke wa mtu ni ishara ya kutoka familia au maisha ya kukosa kipato sasa anataka kupata au kufidia alichokosa.
Kijana unakuta anapenda mwanamke wake achangie gharama za maisha hata kama yeye ana uwezo wa kufinance kila kitu. Hii ni dalili katoka katika familia ambayo ili mlea kutokuwa responsible kama kiongozi wa familia.
Au ana hasira hasira za haraka, kuna uwezekano mkubwa ni kuwa alikuwa hasikilizwi alipokuwa katika familia yake sasa namna ya kujenga hoja ni kwa kutumia ukali au sauti ya kufoka ili kuweza kusikilizwa.
Au unakutana na binti anadharau sana na hawezi kutii maelekezo ya mwanaume wake. Ukichunguza ni mama yake kamjenga na hiyo tabia kutokana na mahusiano mabaya na mume wake au ni binti aliona mama yake na baba wakiishi kwa kutokuheshimiana so na yeye anacopy hivyo hivyo.
So its better kupata therapy before mtu hajafika 30 years of age sababu ikifika hapo uwezo wa akili kurepair tabia unaanza kupungua kwa kasi sana. Ndio maana hatushauri mwanamke kuingia mahusiano serious above 25 hadi 30 sababu ni umri mbaya sana kwa mtu ambaye hajitambui kitabia. Akifika huo umri itabidi akubali kuishi alivyo maana hatoweza badilika kirahisi na akijaribu itamtesa sana kuadopt tabia mpya.
Kwa wanaume tabia huwa inatengenezwa mapema zaidi. Ukikosea ndio basi hata akifika 30 tayari ni umri anasimama mwenyewe inakuwa tayari kishachagua tabia za kuishi nazo.
fact kubwa sanaSuch a sensible thread lakini not many will heed to it.
Watu wengi wamekuwa hawana furaha ya maisha kwa kubeba mizigo inayotokana na childhood trauma. Kuna mahitaji (psychological) ambayo waliyakosa kutoka kwa wazazi au walezi wao na kuwaathiri katika njia moja au ingine.
Wanapokuwa na kuanza kuwa na wapenzi wanaowaonyesha mapenzi yule inner child ambae alilazimika kukua bila yale mahitaji anakuwa anatarajia kuyapata kutoka kwa mpenzi wake, kitu ambacho in reality hakiwezekani.
Ulichokikosa kwa mzazi wako sio rahisi mpenzi wako aki fulfill.
Au sometimes unakuta mahusiano fulani ya kimapenzi yalikuwa na manyanyaso fulani na yakaja kuvunjika. Sasa kabla ya kupona kutokana na maumivu hayo na kujifundisha kosa lilipotendeka unakuta tayari mtu kajiingiza kwenye mahusiano mengine.
Sasa kunakuwa na never ending chain of trauma, never healing, never letting go. Matokeo yake tunakuja kuwapa watoto wetu zile trauma na hivyo basi kuanzisha generation of damaged traumatized kids.
Ndugu, wataalamu wapo wa afya ya akili, psychologists na wapo kwa ajili ya kutusaidia kupona. Tuwatumie basi kwa kupata msaada katika masuala haya.
Samcezar big up sana. Nice thread.
Namfokea mke wangu mpk nikikaa mwenyewe najiskia vibaya, why nakua hivi u can't help itMimi hapo kwenye kufoka...ni hatari na nusu
Hii imenipa somo kubwa sana katika kuwalea watoto kiusawaKimsingi mimi mtoto akija kunirepotia kuwa ndugu yake kamtendea jambo lisilo la haki kama kumnyima kitu au kumdhurumu au kumnyang'anya kitu huwa nakuwa mbogo sana na nitataka haki itendeke haraka sana.
Kwasababu hivyo vitu vikiachwa chuki za utotoni huwa zinamea nakuwa kubwa utu uzimani.
Nina baba mdogo wangu haivi na dada yake hadi sasa ni watu wazima. Shida ilianza utotoni ni kuwa shangazi alikuwa anaachiwa maagizo ya kuangalia nyumba na kusimamia wadogo zake kipindi cha utotoni.
Sasa akawa anatumia authority hiyo kibabe na kuwafanyika wadogo zake majukumu kibabe na kuwapelekesha na ilitokea wakagoma wazazi wakirudi yeye atachomea utambi na wadogo watachapwa.
Sasa wamekuwa watu wazima na yule mdogo amekuwa na pesa ni meneja wa Tanesco ngazi ya mkoa,dada yake mambo si mazuri anaishi maisha ya kawaida sana. Sasa ikitokea jambo halafu dada mtu akataka kutoa sauti mdogo wake anasusa na hataki mtu amwambie lolote anakuwa mbogo.
Basi sababu ya pesa inabidi asikilizwe basi litakwenda namna anataka hataki majadiriano.
Kuna kipindi baba yao alikuja mjini kupata vipimo, dada mtu bila kumshirikisha mdogo wake alipanga safari ya mzee wao ya kuja Dar. Mdogo mtu akajua akamind sana. Alipofika akampeleka Hospital bila kuzungumza nae walipofika hospital akapewa vipimo, balaa kwenye kulipia akamtumia ndugu kumpigia simu mdogo mtu kumjulisha. Alichofanya hakwenda hospital akakaa kimya hadi walimrudisha mzee wao home kwa dada mtu. Ndugu kumuuliza mdogo mtu akatoa ya moyoni, basi wakabidi kujishusha yeye atoe maagizo.
So akaja akamchukua mzee wake na dada yake wakaenda hadi muhimbili kuendelea na matibabu. Ameenda wamekaa kufanya vipimo walipomaliza dada mtu sijui alitoka nje kutafuta nini mdogo mtu akatekenya gari huyooo kaenda na baba yake nyumbani kwake akamuacha.
Dada mtu anatoka anakuta washasepa. Kupiga simu haipokelewi. Akarudi na daladala.
Kwahiyo chuki huwa zinamea ni vema sana kuwatendea haki watoto wakiwa wadogo ili akikua anakuwa hana kinyongo na ndugu yake.
Mkuu unaweza kujua kabisa una tatizo shida ni kujitibia, ni ngumu sanaUbaya ni kwamba unaweza kuwa na tatizo na hujui kama una tatizo teh
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kimsingi kwa sasa hatuna ile social psycho security inayotupatia ahuweni ya utulivu wa kiakili na kuweza kufocus na maisha.Kabisa
Yaani jmn mtu unampenda,kisa aliumizwa alikotoka nawe anakuumiza bila kosa
Duh inaboa sana
Ila kibongobongo watu huu sio utamaduni wetu ni shida sana
Kuna watu hadi unatamani umtembezee mikanda ya kichwa akili imkae sawa. Sababu huwezi kaa nae chini kumuelewesha juu ya mapungufu yake akakuelewa.Ubishi sasa kumbe ubishi mwingine ni ugonjwa mtu anashauriwa cha maana ila yeye kwasababu anaa degree na anaye mshauri hana uwii anakuona kiazi kumbe yeye ndiye nazi bovu
Na katika kitu kinajenga tabia za watu kutokuwa wanajali wengine ni malezi yale ya familia ya kutojali hisia za mtoto (sio kumdekeza). Unakuta mtoto wa familia ametoka kwenye mizurulo anarudi hawekewi chakula. Akiuliza anajibiwa "'wee ulikuwa wapi?" "Cheza mbali unga robo". Au mtoto anasema najiskia vibaya unasikia mzazi au ndugu yake aidha kaka au dada anajibu kwa kuropoka "Haumwi huyo ni uvivu tu unamsumbua" maneno yanayoshiria familia haina upendo kwa mwanafamilia.Kwa kweli hii issues za malezi ni tabu... mimi nina ndugu yangu ambae alinifanyiaga jambo la ajabu alikua agement mtoto wa baba mkubwa aliniibia manati ya baba na mimi nilichukua tu niirudshe na baba alikua mkali sana.. enzi hizo tunawinda ndege msituni moshi huko akaificha kichakani halaf akaenda kuichukua yani had sa iv najikuta sina imani nae kabsa.. Mwingine ni my step mom alikua ananitesa sana then i don have any feeling for my family at all.. Then mahusiano im so unloveable kila mahusiano mademu wanalalama 2 u dont care no communication yani ad ua najistukia yani na we end in break up za kupotezeana..
Tabia ni matokea ya trend ya aina ya maisha ulikulia au kuexpirience hapo kabla.Asee kwenye maisha unaweza kudhati shida fulani uko nazo peke yako, kumbe tupo wengi sana...... Yani mtoa post na comments za watu naona kama wanazungumzia maisha yangu. Hakuna kitu mmeacha naona kabisa shida zangu, ila remedies ndio inakua mtihani nimejaribu kubadilika lakini wapi, ni kweli unajikuta unawaumiza watu kihisia, hasa wanaume ni waanga sana wahizi traumas za utotoni.
Maisha yanakua ya huzuni bila hata sababu ya msingi, saa zingine unaona una kila kitu unachokihitaji lkn bado hauna furaha
Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna anaekuelewa... Kiukweli mambo ni mengi sana na sijui hata tunafanyaje kujisaidia
Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app
Yeye huwa ana respond vipi?! Au nini husababisha mnafikia hatua ya wewe kumfokea.Namfokea mke wangu mpk nikikaa mwenyewe najiskia vibaya, why nakua hivi u can't help it
Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app