Nihivi karibuni nilipokea simu kutoka kwachumba wangu huku akiwa na huzuni sana,kwa kweli juzuni yake ilikua zahili. aliniambia ahadi yetu ya uchumba imefika kikomo.
SIkuamini hilo kwani kwa jinsi mapenzi yetu yalivyokua ya dhati sikufikiri tungeachana tena kwa gafla kiasi hicho bila kugombana. basi binti akanieleza kua alikua anasubiri nimaluze UE (university exam) ili anieleze nn sababu
Binti alidai kuwa alimueleza mama yake kwamba kapata mchumba na kwa kua wote tunaishi kijiji kimoja alimueleza mchumba huyo ninani.binti anadai mama yake alimkalipia mno na kumweleza kua akiendelea kua na Mimi atamlaani yeye kama mama hataki kusikia hilo jina langu kwake
Nilimuliza sababu za mama yake kuwa mkali hadi kutishia kumlani mwanae.binti alisema kisa ni mababu zetu waligkmbana hapo zama I na wakaapa familia zetu kutoshilikiana kwa lolote. akasema chanzo ni babu Yang(ambalo ni Nina langu) kumdhulumu babu yake ng'ombe wake.
Anasema babu yake alitaka babu yangu ampatie binti ili endeleze ukoo wake baada ya mke wake kushindwa kupata mtoto.,walikubaliana na babu yake akatanguliza ng'ombe kazaa binti akikua na kutauluwa basi angempa mzee Hugo. ila alipokuwa hampa binti na wala hakumrudishia ng'ombe wake. hivyo wakalaniana.
Binti alitisha kwa kusema matatizo yote yaliyo ktk familia yetu yanachangiwa name swala hilo. nikifikiria fimilia yangu naona kama ni kweli kwani kuna matatuzo makubwa mno. so alidai bila kurudisha hzo mali sitafanikiwa na elimu yangu ni bure.
huwezi kuamini ila niko njja panda sijui la kufanya nawaza sana sana.kama huna ushauri basi jifunze kutimiza ahadi. asanteni na pole kwa kuwachosha name article hii ndefu.