Kama hatuwezi Kuwasaidia kila Siku basi ni vyema tukauacha ' Unafiki ' unaokera mara moja kwani ' tunajilaani ' bila kujua

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,920
Nachukizwa sana kama siyo mno na tabia ya Watu mbalimbali hasa Makampuni kujifanya wakati wa Sherehe mbalimbali hasa hizi Kubwa za Kidini ndiyo Wanatembelea Makundi ya Watu wasiojiweza kama Watoto Yatima na Wazee bila kusahau Wagonjwa huku wakiwasaidia Vitu mbalimbali.

Kwangu Mimi nautafsiri huu ni ' Unafiki ' wa Kiwango Kikubwa sana kwani haingii akilini katika Siku 365 za Mwaka yaani tunawakumbuka hawa Watu wenye kuhitaji Msaada wetu kwa Siku 1 tu halafu hapo hapo tunajisifu Mitandaoni na katika Vyombo vya Habari wakati kumbe ni ' Upuuzi ' mtupu.

Uwekwe utaratibu wa kuwasaidia kila Siku na siyo kusubiria katika hizi Sherehe Kubwa za Kidini. au la sivyo tuache tu Kuwasaidia na Mwenyezi Mungu atajua Yeye mwenyewe jinsi ya Kuwapigania kwani nilichogundua ni kwamba 99.9% ya wanaojifanya kuwa wanawasaidia wanafanya hivyo kwa ' Maslahi ' yao binafsi hasa hasa ya Kutafuta Sifa kwa Jamii, au Kuwaridhisha Wafadhili Wao au wapo wengine pia wanafanya hivyo kama sehemu yao ya ' Maagano ' na Waganga Wao wa Kienyeji ili tu mambo yao yazidi Kunyooka ' Kishirikina ' lakini huwa siyo ' Utashi ' Wao.

Nawasilisha.
 
Kweli umetoa dozi kama ilivyo dawa ya gentamycine nimefurahi sana maana utaona wanajidai wamekuja kufurahi pamoja na watu wale inamaana kama ni msaada lazima utoke siku ya sikukuu siku nyingine wanaishije?
Nachukizwa sana kama siyo mno na tabia ya Watu mbalimbali hasa Makampuni kujifanya wakati wa Sherehe mbalimbali hasa hizi Kubwa za Kidini ndiyo Wanatembelea Makundi ya Watu wasiojiweza kama Watoto Yatima na Wazee bila kusahau Wagonjwa huku wakiwasaidia Vitu mbalimbali.

Kwangu Mimi nautafsiri huu ni ' Unafiki ' wa Kiwango Kikubwa sana kwani haingii akilini katika Siku 365 za Mwaka yaani tunawakumbuka hawa Watu wenye kuhitaji Msaada wetu kwa Siku 1 tu halafu hapo hapo tunajisifu Mitandaoni na katika Vyombo vya Habari wakati kumbe ni ' Upuuzi ' mtupu.

Uwekwe utaratibu wa kuwasaidia kila Siku na siyo kusubiria katika hizi Sherehe Kubwa za Kidini. au la sivyo tuache tu Kuwasaidia na Mwenyezi Mungu atajua Yeye mwenyewe jinsi ya Kuwapigania kwani nilichogundua ni kwamba 99.9% ya wanaojifanya kuwa wanawasaidia wanafanya hivyo kwa ' Maslahi ' yao binafsi hasa hasa ya Kutafuta Sifa kwa Jamii, au Kuwaridhisha Wafadhili Wao au wapo wengine pia wanafanya hivyo kama sehemu yao ya ' Maagano ' na Waganga Wao wa Kienyeji ili tu mambo yao yazidi Kunyooka ' Kishirikina ' lakini huwa siyo ' Utashi ' Wao.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli asilimia 90%
 
Back
Top Bottom