Kampuni ya Crown Co.ltd inatuhumiwa kuajiri bila mikataba, ukilalamika unapewa kipigo

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Na Mwandishi Wetu,Arusha

Wafanyakazi 120 wa Kampuni ya Crown Co.ltd iliyopo Jijini Arusha eneo la Unga ltd inayojihushisha na uchanganyaji rangi mbalimbali inatuhumiwa kufanyisha kazi wafanyakazi bila ya kuwapa mkataba wa ajira na ukidai mkataba wa ajira tu unatengenezewa ajali ya wizi na kupewa kipigo kizito zaidi ya mbwa koko.

Baadhi ya wafanyakazi wakiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha walisema kuwa kampuni hiyo inayomilikiwa na raia wa Asia wenye Uraia wa Nchini Kenya kuwa serikali yote iko kiganjani kwao na wanafanya hivyo kwa kuwa wana jeuri ya baadhi ya viongozi wakubwa serikalini wanawalinda na hawezi kufanywa lolote hapa Tanzania.

Mfanyakazi mmoja alisema kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya Crown Co.ltd hawana mikataba wa ajira na wengi wao wako kwa zaidi ya miaka minne bila ajira wala kuchangia michango ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kama {NSSF} na malipo hulipwa kwa wiki kiasi cha shilingi 42,000 ambapo kwa siku wanalipwa shilingi 7000 tu hiku wakipigishwa kazi pasipo vifaa vya kumlinda na akiumia kazini husimamishwa hadi atakapo pona na halipwi chochote kutokana na kutokuwa na mkataba wa ajira kwahiyo wanakosa stahiki muhimu za mfanyakazi anapo umia akiwa kazini.

‘’Tunaiomba Serikali ya Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan itusaidie sisi wafanyakazi wa Crown Co.ltd Arusha kwani hawa Wakenya wa nanyanyasa wafanyakazi kupita kiasi,hawalipi kodi,hawachangii Mifuko ya Hifadhi na ni wajeuri kupitiliza na mbaya zaidi wameungana na watanzania wenzetu kutunyanyasa hasa HR wetu ni mmeru huyu anatutesa sana kama yeye siyo mtanzania‘’. Walieleza wafanyakazi hao.

‘’Hii jeuri wanayoipata inawezekana kuna siri ndani yake kwa maana ukifikia muda wa zaidi ya miaka minne unasingiziwa umeiba na unafukuzwa kazi kama mbwa na hata ukilalamika Idara ya Kazi hakuna hatua zinazochukuliwa’’ alisema Mfanyakazi Mmoja.

"Tinaiomba serikali kupitia wizara ya kazi vijana na watu wenye ulemavu iliyopo chini ya mama yetu mpendwa Prof Joyce Ndalichako pamoja na kaka yetu katambi walione hili tabu tunayo pitia wao wakiwa kama viongozi waliyopewa dhamana na mama yetu mpendwa Samia Suluhi Hassan, tunaomba sana tupo chini ya miguu yao watusaidie tuweze kupata mikataba ya kazi na kulipwa fidia zetu za kipindi chote tilichofanyishwa kasi kama vibarua". Walieleza kwa uchungu mkubwa.

Akizungumzia tuhuma hizo Afisa Mwajiri Msaidizi wa Kampuni ya Crown Co.ltd Grory Kilango alisema hawezi kusema chochote kwa waandishi wa habari kwa kuwa waandishi sio idara ya kazi wala polisi na hata kama mkiandika nyie andikeni mnavyoweza na hata Waziri yeyote akija hatutatishika kwa hilo.

Kilango aliyekuwa akiongea kwa kujimwambafai alisema kuwa HR Elisaria na yeye ndio kila kitu katika kampuni hiyo na hakuna kiongozi wa serikali ya Mkoa hata Taifa atayeweza kuiongoza Kampuni hiyo ifanye kazi kwa misingi yao bali watafanya kazi kwa misingi yao na sio vinginevyo.

‘’Kwanza siwezi kusema chochote juu ya wafanyakazi kuajiriwa ama kutoajiriwa kwa waandishi wa habari kwa kuwa nyie sio Idara ya kazi na hata Waziri akija mimi simwogopi chochote atafuata matakwa yetu na sio yake nendeni kaandikeni hivyo’’.

Mwisho
IMG-20230209-WA0014.jpg
IMG-20230209-WA0015.jpg
 
Mtanzania anasimamia unyonywaji wa Mtanzania mwenziye huku akijinasibu kuwa Tanzania haina cha Kumfanya.Ndugu Saria na Grory Kilango kama ni kweli,mnafanya hivyo na mna mtu wa kuwalinda huko juu,Angalieni yule bwana Aliyepo hapo Kisongo.Dunia inatazama.Wapeni watu stahiki zao,endesheni kampuni kwa mujibu wa sheria za kazi.
 
Back
Top Bottom