Kama haki itatendeka ndani ya CC ya CCM, Dkt Salim A Salim ndie Rais bora ajaye

Salim Ana fit hata Mimi nitampigia kura atasaidia sana kujenga muundo wa muungano na katiba
 

Umenena yote mkuu.

Fursa ya Salim kuongoza taifa ilishapotea tayari. WaTanzania wa leo wanahitaji kiongozi mkakamavu ambaye atakuwa tayari kuwa muhanga wa vita ya ufisadi na hilo silioni kwa SAS.

SAS amekuwa muoga mno hata kukemea mambo ambayo sivyo ndivyo kwenye chama na serikali yake. Sasa mtu asiyeweza kutetea mambo madogo atawezaje kukemea au kubadilisha mfumo wa kulindana na hatarishi kwa mustakabali wa maisha ya mTanzania wa leo?
 

Ndugu yangu Lizaboni, hako ka mfumo sio rasmi na hakana maana, kinachotakiwa sio Shehe au Mchungaji/padri anatafutwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiongozi aliyebora ni zaidi ya mwislam na mkristu.
 
Dr. Salim simpingi ila muda umeisha. Nchi hii ya wezi, mafisadi tena papa wehu kibao. Anatakiwa rais anaefanana na Edward Sokoine au Augustin Mrema wa 1990 na 1995. Nchi hii haiitaji tena uswahili na uswahiba.
 

Sidhani kama atagombea ila kama umemsikia akisema hivyo sawa.

Kupita CCM ni vigumu sana kwa sababu kwa sasa kamati ya walioba iliyopita na kukusanya maoni haiko vizuri na CCM, kulikuwa na ile misuguano ya katiba mpya. pili Huyu mzee alidhalilishwa sana mara ya mwisho kugombea na waliomdhalilisha bado wapo.
 
labda achukue form kugombea zanzibar. wabara wazuri hawakosekani. rais wa muungano ndio pia rais wa tanganyika. muda wa salim ulishapita akijitokeza sasa atapata dissapointment.
 

Kama unampenda kanywe naye chai, au kalambe miguu yake. Sasa hivi ni zamu yetu wa...... Nafikiri umenipata
 
labda achukue form kugombea zanzibar. wabara wazuri hawakosekani. rais wa muungano ndio pia rais wa tanganyika. muda wa salim ulishapita akijitokeza sasa atapata dissapointment.
Ukweli ambao sijui kwanini watu wanakwepa kuusema. Watanganyika hatuhitaji expatriate president. Muda wa wazanzibar ulikwisha na mwinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…