Kama haisaidii inaumiza

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
KAMA HAISAIDII INAUMIZA

Hakuna katikati kwenye hilo, ni iwe inasaidia au la inaumiza.Kama kazi unayofanya haiwasaidii watu basi inawaumiza, na kwa kufanya kazi ya aina hiyo, huwezi kupata mafanikio makubwa.

Kama biashara unayofanya haisaidii watu, basi inawaumiza na kwa aina hiyo ya biashara usijioteshe kwamba siku moja utakuwa na mafanikio makubwa.

Kama unaona kuna watu wanaumia mahali na wewe una uwezo wa kuwasaidia, kama utaona sio jukumu lako na hivyo kutokuwasaidia basi na wewe umechangia kuwaumiza.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, hakikisha upo kwenye upande wa kuwasaidia wengine na sio kuwaumiza.Kwasababu mafanikio yako yanategemea sana mafanikio ya wengine, ukishakuwa kwenye upande wa kuumiza watu, huwezi kupata mafanikio. Na hata ukiyapata yatakuwa ya muda mfupi tu, hayatadumu.
 
dunia ya kibepari hii mjomba, sasa wewe leta ujamaa usombwe na maji.

Maisha ni kupambana, na yeyote ambaye utamwona ni kikwazo kwako katika kusonga mbele ni kumwondoa na km ikiwezekana nikumpoteza kwenye ulimwengu huu kama utakuwa na uwezo huo, km huna basi badili giaa

Survival of the fitness.
 
Back
Top Bottom