Kama CCM na Upinzani wanaungana kutetea Maovu, kuna haja ya kuwa na Vyama vya upinzani.?

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,282
38,359
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
 
Idawa unahamisha magoli ufunge kwa urahisi kaka. Ni dhahiri kinachofanywa na RC ni kurefusha vita dhidi ya unga badala ya ukimaliza. Bunge halijakataa hoja ya kupambana na madawa bali ni dharau iliyoinyeshwa kwa Muhimbili wake. Mbona huongelei yule Mnyeti aliyeitwa na Bunge unamdhania RC peke yake? Nakwambia Idawa RC anawaficha wauza mihadharati kuliko kupambana naye kwa hii approach. Watakimbia tu watachukua tahadhari mno na watazidisha umakini. Namkubali Mh. Kitwanga wengi waliojihusisha walikamatwa kilaini hasa na kimya kimya wako mahabusu
 
Watz tu wagumu kuelewa aiseeee...Spika kaeleza kinagaubaga, kinachogomba hapa ni kutokufuatwa kwa kanuni na taratibu.
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?

Hilo ni bunge la wapi unafanya marejeo yako ndugu Idawa?

Kama ni bunge la Tanzania utakuwa ama unapotosha au huelewi ulichoandika na hujui umesimamia kipi.

Wabunge hata mmoja hayupo anaepinga biashara ya mihadarati, tatizo lao na RC wetu ni approach inayotumika.
Na kingine wameungana kutetea haki yao ya kutokamatwa bila utaratibu,kumkamata au kumhitaji kiyuo cha polisi mbunge anapokuwa bungeni kuna taratibu zake,unapozikiuka unataka wakae kimya?

Naomba uje kwa upya, kama ndo ulijipanga kutetea kufutwa kwa vyama vya upinzani Tanzania, basi kaanze upya kuandaa post yako.
 
Vita ya unga ni ngumu sana leo hii Chadema wameungana na ccm kuikwamisha vita kwa kisingizio bunge limedharauliwa. Ndio maana mimi namkubaligi Magufuli tu haya mavyama ni vichaka vya wapigaji leo hii Zitto na Mbowe wapo meza moja na kila mtu anawashangilia.
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?

weka video hapa inayoonyesha wabunge wakitamka kuwa wanapinga vita dhidi ya madawa ya kulevya.

kila mwenye akili timamu amesema anaunga mkono vita ya madawa ya kulevya ila tunapinga upumbavu unaofanywa na Makonda wa kutangaza majina ya watu hadharani na kupelekea kuwaepusha real drug dealers na mkono wa dola.

mleta mada na Makonda mmeingiza wenyewe kichwa kwenye mzinga wa nyuki.
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
Thread ya kimwendokasi, hivi umejiuliza tu kuna haja gani ya kuwa na vyama vya upinzani? mbona hujajiuliza kuna uhalali gani wa kuwa na chama kama CCM ambacho ndicho kimejaa ma druglord wanaosponsor kampeni za CCM kwa miaka nenda rudi?
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
Unajitahidi kumtetea Makonda kwa kupindisha ukweli, azimio gani la bunge liliazimia kupinga vita ya madawa ya kulevya, acha uongo.

Kwahiyo kwako CCM wakitetea maovu sawa kuendelea kuwepo ila vyama vya upinzani vikitetea havitakiwi kuwepo?

Ninachojua azimio lililopitishwa na wabunge wote ni la Makonda kulidharau bunge.
 
Sio kwamba hakuna haja ya kuwa na Upinzani....

Ila kuna haja ya kuwa na overall ya Ku review na kufanya vetting kwa wote wanaotaka kuwa wapinzani kwa kujiridhisha je wanafaa..........

Sasa hivi tupo na Upinzani butu pia tupo na chama kibovu cha mapinduzi..........

Kuna wagombea wanapitishwa na wapinzani kugombea ambao ni mabomu kama wanavyofanya Ccm hapo ndio tunatakiwa kuanzia kuwakataa bila kupepesa macho...

Upinzani maana Yake ni uadilifu kwanza sio vinginevyo...........

Cha kufanya ni kuwa na mkakati wa kuwatafuta wapinzani wa kweli ambao wanaweza kuungana na serikali kwenye mambo ya maendeleo na kuitosa serikali kwenye mambo ya kiuni kama walivyofanya ......

Ni hatari kwa nchi kukosa Upinzani..
 
Kuna watanzania walifaa kuzaliwa Nyati ili tuwafuate mbugani kuwatizama kutokana na vioja vyao. Kuna watu mnaamini viongozi wa serikali ni malaika hawapaswi kusahihishwa au kushauriwa.

Hii ni kufuru kwa muumba wako maana umekabidhi uwezo wako wa kufikiri kwa viongozi wa serikali hii.

Bunge, limetetea hadhi yake na kuukumbusha mhimili mwingine (serikali/dola) wawe wanafuata sheria na taratibu wanapohitaji kumuweka kizuizini mbunge na pia RC na yule DC wamelitukana bunge.

Pia wao kama wasimamizi wa serikali, wameishauri serikali ifuate sheria zilizopo katika kupambana na madawa ya kulevya na kuiepusha serikali kuingia matatani mbele ya safari.

Kuna wakati tuache upofu wa mahaba ya kichama
 
Upinzani si kazi yake kuonesha maovu ya serikali bali kuwa mbadala wa serikali, Kwa kila serikali itakachofanya wapinzani huonesha jinsi gani kingefanyika kwa ubora zaidi. Kama upinzani utaungana na serikali kwa iyafanyayo hapo ndio hakuna maana ya upinzani.
 
Idawa unahamisha magoli ufunge kwa urahisi kaka. Ni dhahiri kinachofanywa na RC ni kurefusha vita dhidi ya unga badala ya ukimaliza. Bunge halijakataa hoja ya kupambana na madawa bali ni dharau iliyoinyeshwa kwa Muhimbili wake. Mbona huongelei yule Mnyeti aliyeitwa na Bunge unamdhania RC peke yake? Nakwambia Idawa RC anawaficha wauza mihadharati kuliko kupambana naye kwa hii approach. Watakimbia tu watachukua tahadhari mno na watazidisha umakini. Namkubali Mh. Kitwanga wengi waliojihusisha walikamatwa kilaini hasa na kimya kimya wako mahabusu
Mara nyingi tu bunge linadhauliwa mpaka leo linaendelea kudharauliwa kutokana na udhaifu wake wa kushindwa kisimamia mambo ya msingi.

Kwani wabunge wa upinzani wameanza kukamatwa leo, Mara ngapi serikali inafanya mambo kinyume na maagizo ya bunge lakini hatujasikia wakilalamika kudharauliwa.

Kwa kauli gani ya Makonda aliyoongea hadi aonekane amedharau Bunge?
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
Mbona mnakuwa sio waelewa? Hakuna anaye pinga jitihada za kupambana na madawa bali njia iliyo tumika inaonesha kabisa hakuna nia ya dhati ya kupambana na hilo, njia iliyo tumika si sahihi na ndio kinacho pigiwa kelele msiwe wajinga kiasi hiki,kwa njia iliyo tumika ni vigumu sana kupata wauza madawa halisi na hawata patikana kamwe, biashara ya madawa sio kama kukamata kokoro mkuu.
 
Sijawahi kufikiri kuwa una UFAHAMU mdogo kiasi hiki.
Sijaona wakitetea uovu bali wanapinga njia zinazotumika kupigana na uovu.

Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
 
Hata wabunge wenyewe wakati wanapitisha azimio la kumuita Makonda hawakufuata kanuni......
Hujui lolote zaid ya ushabiki na kujipendekeza kwako kwa makonda. mkuu na ushabiki huo utakujaza ujinga na utalemaa kiakili tumia akili yako sawasawa ili utafakar mambo kwa upana wake.
 
Back
Top Bottom