Kama bajeti inategemea pombe na sigara!!!

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Wakuu habarini za kazi,Nilikuwa nawaza hili kama serikali bajeti yake inategemea sana vinywaji kama pombe na sigara basi serikali haina budi kuwaheshimu wanywaji(walevi) na makampuni yao yanayotengeneza vinywaji hivyo.Na hata zile kamatakamata za usiku kwenye mabaa zingesitishwa maana hao ndio wanaolipa kodi kubwa serikalini na kamatakamata hiyo iamishiwe migodini na kusiwepo na shifti ya usiku migodini kwa sababu hakuna mchango wao mkubwa serikalini.Tena ule ulinzi wa jeshi la polisi unaopelekwa migodini ungelihamishwa na kuletwa kwenye kila baa maana bila hao serikali haiendi.
 
Kuwepo na matangazo ya kuhamasisha unywaji pombe na uvutaji sigara. Tena tangazo liseme, "ewe mtanzania, onyesha uzalendo wako kwa kuvuta sigara na kunywa pombe. Mzalendo halisi ni yule anayechangia pato la taifa?"
 
Back
Top Bottom