Intaneti ni biashara si anasa. Intaneti ni ajira, si starehe kama pombe na sigara!

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,759
Mwambieni waziri wa fedha pamoja na TCRA kwamba internet ni biashara sio anasa kama wao wanavyoweza kudhani vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara nyingi za mitandaoni zinazotegemea zaidi internet na bando.

Wapo YouTube, wapo Instagram, wapo kila mahali wanajiingizia kipato na kodi wanalipa! Sasa kwa nini serikali haisikilizi kilio hca bando kuwa juu? Hivi mnajua vyuoni wanafunzi wanasoma kwa kupakua mtandaoni, na kuna watu pia wanasoma online?

Mmekosa sehemu nyingine ya kukusanya mapato ili kuwa saidia vijana wanaotegemea internet kuendesha maisha yao? Au mnadhani internet ni anasa kama pombe na sigara?

Tafadhari pungezeni bei ya bando muifanye nchi kuwa ya kisayansi. Mtatuua mwaka huu, kila mahali ukigusa unamkuta Mwigululu anakusanya kodi, mwe! Hatukatai, ila punguzeni kidogo!
 
Hawwezi kukuelewa maana wao wanalipiwa internet ofisini na wana wifi za bure na hata simu zao zina free internet unlimited, hiyo ndio inaitwa aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Back
Top Bottom