Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,677
- 870,411
Viongozi wa kiimani (kidini) na waumini wao
Watabibu na wagonjwa wao
Waganga wa kienyeji na wateja wao
Makundi yote haya matatu yamegawana imani
Yamegawana mashaka
Yamegawana undumilakuwili
Hayajiamini kwa asilimia 100, hayaaminiani kwa asilimia mia moja.. Lakini yana muingiliano na ushirikiano kwa asilimia 100
Siku za ibada ni mawaidha na mahubiri ya kuwasema vibaya waganga wa kienyeji na kazi zao.. Na uchawi, mbele ya waumini ambao ni wateja wakubwa wa ulozi wakiwemo viongozi wenyewe
Siku za kazi wao na waumini wao watafurika kwenye tiba za asili na za kisasa
Tabibu bingwa atamshauri mgonjwa aende kwenye maombi ama kwenye dua na kisomo! Akishindwa huko aende kwa 'wataalam' yaani waganga wa kienyeji
Unakutana na mke wa mganga kaenda hospital za kisasa, au kampeleka mtoto, ah mganga mwenyewe kalazwa😀
Unakutana na kiongozi wa dini naye ana booster kiunoni ama analalamika kurogwa!
Vipi kuhusu tembe za kutuliza maumivu kwenye kilinge cha mganga?
Kwenye kabati la tabibu kuna msahafu, na kuna madawa ya kutibu magonjwa lakini mwilini kachanjwa😀
Kitu kimoja kilicho dhahiri wote wanatambua uwepo na ukuu na nguvu za Mungu lakini imani zao si timilifu! Ni haba
Imani zao zimegawanyika katika makundi makundi ... Yaani wanamiliki imani tatu kwa wakati mmoja, kinachotofautisha ni mazingira tuu
Mtumishi wa kidini anaroga asihamishwe kituo au apate mvuto
Daktari anaroga ili apate kinga ya kiroho au apandishwe cheo
Mlozi anawaagua kisha anawaambia wamuombe Mungu.😂
Lakini ni mlozi huyuhuyu wanawe wanahudhuria hospital za kisasa na wanahudhuria nyumba za ibada kujifunza mafundisho ya Kimungu
Mwisho unapata suluhu moja tuu.. Wote wamechanganyikiwa na hawajui wanataka nini na wanaamini nini kwa hakika