Kali za mwaka 2014 nilizokutana nazo

Kali za mwaka 2014 nilizokutana nazo

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Niliwahi kuishi maeneo fulani hapa Mjini, kwa hiyo kuna Mwanamke fulani alikuwa jirani yangu, nilikuwa tu namsalimia shikamoo kila nikimwona basi, maana alikuwa mtu mzima (ana tako balaa tupu), baadaye nilihama hapo nikaenda kwingine. Hatukuwahi kuwa karibu wala hatukuwahi kuwasiliana kwa njia nyingine zaidi ya kusalimiana tukionana tu. Sasa siku moja akakutana na rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa anatufahamu wote:

Akamuuliza "Rafiki yako yule nilikuwa nawaona wakati mnaishi sehemu fulani ameenda wapi?" Jamaa alimjibu, huyo mama akamwomba namba yangu, akampa.

Yule mama: (alinipigia akanieleza) nimepewa namba yako na rafikiyo yule mlikuwa mnaishi maeneo fulani enzi zile, unajua tumepoteana miaka mingi nikaona nikusalimie

Mimi: Ahsante mama fulani, dah miaka mingi kweli

Baada ya story kadhaa alikata simu, lakini alisistiza kwamba nipate muda japo siku moja nikasalimie. Nikamwambia sawa, nitajitahidi.

Siku moja akaniuliza, wifi yupo nije kumsalimia? Nikamjibu yupo. Akaniuliza, yupo hapo sasa hivi? Nikamwambia mie nipo kazini na yeye pia kaenda kazini. Halafu:

Yule mama: (msg) Unajua mapenzi ni kitu cha amani lakini kinapiganiwa sana.
Mimi: (sms) Kweli kabisa mama
Yule mama: Utaweza kulilinda penzi langu? Isitoshe wewe una wako umpendaye! Nakupenda wewe kijana acha tu.
Mimi: Sikujibu (mpaka kesho)

Nilidelete sms zake na kumblock. Kuna siku alipiga kwa namba ngeni, akaongea kwa nidhamu na kuniambia nilitaka tu kumsalimia wifi yangu huku akikisistiza niende kumsalimia (sio tuende).

Kuna kali nyingine, duh, this world! Hiyo ilikuwa ni 2014. Kuna akina mama wengi siku hizi hawafai, kaa mbali nao.
 
weww kweli boya sasa hizo sifa ulizompa za nini sasa kama humtaki
 
Mbona ulipost kama Kali za mwaka 2014,kumbe ni hiyo moja tuu,na sii kali maana umeanya bams.
 
Mbona ulipost kama Kali za mwaka 2014,kumbe ni hiyo moja tuu,na sii kali maana umeanya bams.

Kali ni hii hapa: Yule mama: Utaweza kulilinda penzi langu? Isitoshe wewe una wako umpendaye! Nakupenda wewe kijana acha tu.

Maana sikumtongoza!
 
Back
Top Bottom