Kali Ya Karne: Mlinzi wa Getini amuomba rushwa Rais Uhuru Kenyatta ili amruhusu kutembelea bustani ya taifa nchini Kenya

Hili ni jambo dogo sana ambalo mwandishi amelikuza sijui kwa sababu gani. Kwa kawaida watu wanapotembelea maeneo kama hayo walinzi huomba hela ili kutoa ulinzi wa magari - na hii haiwezi kuitwa rushwa- ni huduma tu.
 
Kwaiyo ina maana mlinzi hamjui raisi wa nchi yake au ni Mimi ndio sijaelewa kisa icho,,, maana jamaa kaomba Ela na imeelezwa kuw Uhuru katoa Ela mfukoni na kumpa mlinzi,, Mbn Kama tea ya rangi na tangawiz kw mbali
 
Siamini hata.
Mpaka wanaongea kuomba rushwa ina maana walitizamana uso kwa uso ina maana huyo mlinzi hakumwona mtoa rushwa usoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unasema kavunja rekodi umesahau yule mzee mmoja Nshomile kutoka kule Bukoba alimtapeli raisi Nyerere matofali na tena akijua kabisa ni raisi wa nchi.Raisi Nyerere wa watu hakumfanya lolote nani anajua jina lake atuambie.Watu kama hawa ni adimu sana kupatikana wanatakiwa wapewe ulinzi na nishani ya ujasiri
2.Mme msahau yule mwalimu mkuu wa shule flani sijui alikuwa anaitwa Kamuzora mtoto wa Nyerere alifanya kosa shule akamuambia namuhitaji baba yako.Mkuu wa mkoa akatumwa akasuluhishe akakataliwa mwalimu akasema baba yake huyu namfahamu ndio namuhitaji wakaenda wazee mbali mbali aliwakataa hadi mzee Nyerere akaenda mwenyewe na landrover yake.Mwalimu akasema nilikuwa najua wewe ndio baba yake ndio nilikuwa nakuhitaji.Nyerere akachukua kiboko kengele ikapigwa akamchapa mwanaye mbele ya wanafunzi wenzake.Mwalimu Nyerere alivorudi dar baada ya muda akamteua yule mwalimu mkuu kuwa mkurugenzi wa National Milling.
 
haaaahaaa yule mzee wa Msasani aliemtapeli Mwalimu Nyerere matofari alikua mtani wake, jamaa nasikia kabla ya tukio akaenda site akaanza kupiga zogo na mchonga akazizisifia tofari kua nzuri kwelikweli baadae akaagiza roli akazikomba zote dadeq

Mwalimu alipopata taarifa akacheka Sana akasema mtani kamuweza halafu ikawa imeisha hiyo nasikia Kama ni kweli kua zile tofari ndio zilizojenga Morogoro store ya pale masaki Kama sikosei!
😂😂😂😂🙌
 
Nyerere alikua anavumilia mengi,alishawahi kupigwa kwenzi kanisani na padri,padri hakujua ni Nyerere,alijua ni watumishi wakanisani ,alikuja kwa nyuma akamlima kwenzi,akamwambia unafanya nini apa badala ya kuandaa vitu kwa ajili ibada,baada misa kuisha wakaenda kupata chai nzito
 
Kumbe syo rushwa ni pesa ya kurinda gari
 
Hahahaha. Hii imenichekesha sana
 
Nyerere alishawahi sema... MTOAJI NA MPOKEAJI RUSHWA WOTE MANJI GA NYANJA...
 
Dah! Kwa namna ulivyowasilisha kwa mihemko nikadhani jamaa aliagiza rushwa akijua fika ni rais, kumbe mlinzi alijua zali la kawaida ila ikawa ndio zake za arobaini. Haya ni matukio ya kawaida sana Afrika, nakumbuka hata Tanzania marehemu rais Magufuli aliwahi kuhalalisha kwa kusema wawe wanapewa hela ya rangi ya viatu.

Afrika ni usen.ge wa kijinga sana, yaani maaskari wanaomba rushwa kwenye kila kitu, ukiibiwa mtaani inabidi upambane na hali yako maana ukienda kushtaki, pale eti askari watoke kwa defenda kuja mtaani kukusaidia lazima uchomoe noti kadhaa, wakati Ulaya unapiga 911 magari ya mapolisi yanakusanyka kwako mlangoni zaidi ya balaa.

Tatizo la rushwa limekithiri sana nchi hii, sema ni aibu kwa Mtanzania kuchekelea wakati nawafahamu sana kwenu huko......hamna utofauti wowote hovyo bin hoi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…