Kali Ya Karne: Mlinzi wa Getini amuomba rushwa Rais Uhuru Kenyatta ili amruhusu kutembelea bustani ya taifa nchini Kenya

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Habari Wana Kijiji,

Leo katika pita pita za kusoma habari mitandaoni, nimekutana na kali ya karne katika bara zima la Africa. Kenya wamevunja rekodi ya Rushwa katika bara la Africa (Kama Sio Duniani Kwa Ujumla).

Nirudi kwenye mada husika,

Siku za hivi karibuni, Rais Uhuru Kenyatta alikwenda kutembelea Bustani ya Uhuru (Uhuru Gardens) bila ya kutoa taarifa kwa mtu yoyote kwamba anakwenda huko. Alitumia gari binafsi ili mtu yoyote asijue kwamba Rais anakwenda na alikua maeneo yale.

Mara baada ya kufika getini, mlinzi aliokuwepo lindoni kwa wakati huo alizuia lile gari lisiingie ndani ya bustani, bila kujua kwamba aliomo ndani ya gari hilo ni Rais Kenyatta mlinzi aliomba rushwa ili aliruhusu lile gari kuingia ndani ya bustani.

Cha kushangaza zaidi, Rais Uhuru Kenyatta hakua na hila wala gubu, alizamisha mkono mfukoni na kutoa kiasi cha fedha na kumpa yule mlinzi. Mara baada ya kupokea zile hela, mlinzi aliliruhusu lile gari la Rais Uhuru kuingia ndani ya bustani na kulielekeza mahala pa kulipaki gari, huku akimuahidi kwamba usalama wa gari utakua vizuri.

Kama ilivyo ripotiwa na chombo cha habari cha The Star, haikujulikana nini kilimpata mlinzi yule mara baada ya kuomba na kupokea rushwa kwa Rais wa Nchi.


Screenshot_20210710-005142_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210710-005216_Opera%20Mini.jpg
 
Bila ya ya ushahidi wa video. uzi wako naona ni sawa na story iliyo tungwa tu kumpa popularity Kiranja mkuu wa wakenya
 
Back
Top Bottom