Kalamu ya Shaaban Robert Katika Sauti

Kalamu ya Shaaban Robert Katika Sauti

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,455
Reaction score
32,981
KALAMU YA SHAABAN ROBERT KATIKA SAUTI

Vijana wamenambia, "Mzee Mohamed wewe hasa ndiye unaefaa kuwasomea watu Shaaban Robert."
"Kwanini mnasema hivyo?"

"Lafidhi yako inaendana na mwandishi."
Hawa vijana wala hawajamsikia Shaaban Robert.

Sana wamemsoma shule.
Kumsoma kwa sauti Shaaban Robert ni kazi inayochosha baadhi ya nyakati.

Shaaban Robert kuna wakati kalamu yake inateleza juu ya karatasi "smooth ride," Waingereza wangesema.
Lakini kuna wakati Shaaban Robert atakupandisha vilima na kukushusha kwenye mabonde.

Hapa utarudi nyuma kurudia sentensi tena na tena na tena.
Msimamizi ana sikio na jicho kali.

Ukijikwaa kakusimamisha unaanza upya.
Inanikumbusha "audition" niliyofanyiwa miaka mingi iliyopita na BBC Scotland, Glasgow.

Sound Engineer msichana wa Kiingereza neno moja la Kiswahili hajui.
Mimi nafanya kipindi cha kila Jumamosi "Barua."

Hii ilikuwa "Barua Kutoka Glasgow."

Nikawa nashangaa huyu dada anajuaje kuwa nimeliuma neno la Kiswahili ananisimamisha nirudie ilhali yeye hasemi Kiswahili?

Nirudi kwa Shaaban Robert.
Shaaban Robert akieleza jambo anateleza.

Lakini akiingia kwenye filosofia hapo unaweza ukautoa damu ulimi wako.
Raha kumsoma Shaaban Robert.

Utastarehe.
Nadhani ni raha na starehe pia kumsikiliza.

Hili neno, "Mbambamba," mie nikidhani ni neno jipya wamelileta vijana wa leo.
Shaaban Robert kalitumia neno hili zaidi ya miaka 70 iliyopita.

Jingine analonishangaza Shaaban Robert.

Neno, "Kashifa."
Mimi toka nizaliwe najua, "Kashfa."

Naanzisha ligi ndani ya studio na vijana.
Wananisikiliza hawatii lao.

Akili inaniambia, "Wewe nani umsahihishe Shaaban Robert kwenye lugha ya Kiswahili?"
Siiwezi vita na BAKITA.

Shaaban Robert anaandika, "Umi Kulthum."
Nawaambia vijana, "Shaaban Robert kakosea huyu ni "Umm" Kulthum siyo Umi."

Hapa tunasoma, "Wasifu wa Siti Binti Saad."
Nadhani vijana wakahisi haya maneno yangu mengi nishachoka kusoma.

Wananipumzisha kwa kuniwekea video ya Siti mjukuu wa Siti Bint Saad.
Naam.

Si tu anaimba bali anapiga gambusi pia tena kwa ustadi wa hali ya juu.
Maji hufuata mkondo.

Nimeingia Maktaba natafuta kitabu kimoja kaandika Laura Fair: "Historia ya Jamii ya Zanzibar na Nyimbo za Siti Binti Saad."

Kitabu hiki kaninunulia rafiki ndugu yangu Prof. Mohamed Khalil katika mizunguko yetu tuliingia duka la vitabu Stone Town, Zanzibar.

1746330542686.jpeg

1746330604405.jpeg

1746330659896.jpeg

1746330697412.jpeg
 
Nimesoma vitabu vingi vya Shaaban Robert. Kumsoma hata siyo starehe, ni mateso matupu. Sema watu siku hizi wanahisi kuna maneno wamegundua, maneno kama Msimbe na Vijora. Maneno hayo Shaaban aliyatumia kama miaka 70 iliyopita.
 
Jamani mwenye soft copy za vitabu vya shaabani Robert anipasie na mie
 
Back
Top Bottom