Kalala Jr, Chokoraa hao Extra Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kalala Jr, Chokoraa hao Extra Bongo

Discussion in 'Entertainment' started by kilimasera, Dec 18, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo ‘Next Level Wazee wa Kizigo’, imeibomoa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa kuwachukua wanamuziki Kalala Junior na Khalid Chuma ‘Chokoraa’.

  Kujiunga kwa wanamuziki hao na Extra Bongo, kumekuja siku chache baada ya kutokea msuguano baina yao na uongozi wa bendi ya ‘Twanga Pepeta’, kwa kile kilichodaiwa kuwepo mgongano wa kimaslahi, baada ya wanamuziki hao kufanya maonyesho na bendi yao binafsi ‘Mapacha Watatu’.

  Akithibitisha kujiunga kwa wanamuziki hao na bendi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alisema Kalala na Khalid wamejiunga na bendi hiyo ili kuimarisha safu ya uimbaji, pamoja na kuendeleza vipaji vyao baada ya kuamua kuitosa Twanga Pepeta kutokana msuguano huo.

  Alisema, wanamuziki hao watatambulishwa Desemba 31 mwaka huu katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa Vatican City Sinza jijini Dar es Salaam.

  Aidha, Choki alisema, katika sikukuu ya Krismasi bendi hiyo itajivinjari mkoani Morogoro, wilayani Kilosa kabla ya kutua jijini kwa onyesho hilo maaalumu.
   
Loading...