Kakobe asalimu amri mradi wa umeme

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
mnara.jpg

Baadhi ya mafundi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), wakiwa kazini huku mtambo ukinyanyua nguzo ya umeme na kuisimamisha eneo la Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship linaongozwa na Askofu Mkuu, Zakaria Kakobe lililopo eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.







Kakobe%20Z%282%29.jpg

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe.



Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe, amesalimu amri iliyotolewa na serikali kwa kutaka kuweka nguzo za mradi wa umeme wa msongo mkubwa wa kilovoti 132 na kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liendelelee na kazi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika eneo la kanisa lake, Askofu Kakobe alisema asingeweza kupingana na maamuzi ya serikali.
Hata hivyo, alisema ameshangazwa na taarifa aliyoitoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuwa walifikia mwafaka.
"Nasema sio kweli taarifa aliyoitoa Waziri Ngeleja kwamba tulifikia mwafaka wakati nilizungukwa kama mbwa mwitu," alisisitiza.
Alisema lengo la serikali ni kutaka kuwakaanga waumini wake kwa kuweka umeme huo wenye madhara kwani maeneo mengine waliambiwa wahame au waache umbali wa mita 15 lakini kwa upande wao hakupatiwa taarifa hiyo.
Hata hivyo, Askofu Kakobe alisema serikali isiwe na woga wowote wa kwenda kuweka nguzo hizo eneo hilo kwa kuhofia kuwa waumini wake watafanya fujo.



CHANZO: NIPASHE
 
NGUZO ZA KAKOBE ZASHIKA KASI

photos
pix.gif
Zile nguzo za chuma za umeme mkubwa ambazo siku chache Askofu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ametia ngumu zisikatize yalipo makao makuu ya kanisa lake, Barabara ya Sam Nujoma hadi hapo serikali itakapokubalina naye, zimeendelea kuota mithili ya uyoga, kazi inayofanywa na makandarasi wa kichina.
Baadhi ya nguzo hizo kwa sasa ziko katika hatua za mwisho kabisa kama zinavyoonekana pichani. Hii inamaanisha nguzo za magogo ya miti ‘baibai’.


...moja ya nguzo hizo inavyoonekana maeneo ya Makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Shekilango.


...hapa nguzo ikiwa tayari ikisubiri nyaya za umeme kupitishwa.

 
Back
Top Bottom