chuki binafsi..je anataka karama apewe yeye tu?
Hilo ndilo tatizo, ...
1- pia lazima watu waelewe kuwa viongozi wengi wa makanisa yenye mrengo wa kipentekoste hudhani ya kuwa wao tu ndiyo wenye hati miliki ya kuzungumza na Mungu kwa kisingizio cha kuwa wao ndiyo waliookoka kwa sababu tu ya ubatizo wa maji mengi, kunena kwa lugha etc. Na inapotokea mtu wa madhehebu mengine akaonyeshwa/akafunuliwa jambo si wepesi wa kulikubali kuwa linatoka kwa Mungu. Wapentekoste wanapopaka watu mafuta, kugawa chumvi, vitambaa vya upako hakuna mprotestant anayewalalamikia, inakuwa shida pale mprotestant anapofunuliwa jambo.
3 - Ni jambo la ajabu analinganisha jambo hili na deci (ya wapentekoste) ilhali huyu Babu hachukui pesa ya mtu bali wenye pesa wote wanaotaka kumpa kama shukrani anawaambiwa wazipeleke makanisani au misikitini kwao.
4- Mwelezeni kakobe pia ikiwa jambo hili ni ufunuo (rhema-neno/jambo linalotolewa kwa wakati maalum), basi tiba hii itakoma kwani itakuwa imetolewa kwa situation fulani. na situation hiyo ikipita ukomo wake hufika.
5- Na kama kakobe na watu wa design yake WANAKWAZIKA KWA SABABU TU NI MIZIZI INACHEMSHWA, WANAPASWA KUJUA KUWA MUNGU HUZUNGUMZA KUPITIA UTAMADUNI WA KILA MTU, NA KILA JAMII INA UTAMADUNI WAKE ULIO NA SURA MBILI, GIZA NA NURU-MUNGU HUZUNGUMZIA KUPITIA UTAMADUNI WA NURU. HATA YESU KRISTO ALIZUNGUMZA NA KUISHI KATIKA UTAMADUNI NURU WA KIYAHUDI. TATIZO WATU WENGI TUMEKUBALI UONGO WA WAMISHENI WAFANYABIASHARA WALIOTUKATAZA KUTUMIA MIZIZI ILI TUNUNE ASPIRINI ZAO. AMBAZO NI DAWA ZINAZOTOKANA NA MITI PIA.
CHUKI YA KAKOBE NI KWA SABABU TU ALIYEFUNULIWA JAMBO HILI NI MLUTHERI NA SI MPENTEKOSTE KAMA YEYE AU YEYE MWENYEWE.
JIULIZE ANGEKUWA YEYE NDIYE KAFUNULIWA HALI INGEKUWAJE PALE SAM NUJOMA ROAD. NINA UHAKIKA ANGEITISHA MKUTANO WA WAUMINI WA KANISA LAKE NCHI NZIMA WAJE DAR KWA MKUTANO MAALUM WA TIBA.