Kaini alipata wapi mke wake?

Bado mkuu
Kaini alioa dada yake sababu kipindi hicho ndio kwanza dunia ilikua inapanuka. Watu wanaweza kusema anaweza vipi kuoa dada,jibu ni kwa kipindi kile hakukua na sheria inayokataza kuoa na kuolewa na dada,baba,mama,au ndugu.

Pia Abrahamu alioa dadayeke(Sara) Isaka alienda kuoa kwa wajomba zake.

Baada ya Sodoma na Gomora wale mabint waliobak na baba yao walilala naye ili mzee wao awaachie uridhi(watoto) sababu mzee alikua kazeeka sana na hakukua na vijana wa kuwazalisha kipindi hicho.

Chanzo: Biblia
 
Halafu walikuwa wanahesabu watoto wakiume wakike ilikuwa kama kuangua embe nakuliweka ndani hesabu ni wanaume tu, kweli ubaguzi haujaanza Leo ulianzia huko huko tulikotokea.
 
Naomba mwenye audio ya Mwana wa Dandu "James" usemao 'mimi msafiri niko njiani nakwenda, sijui lini nitafika' au original yake ya Mzinga troup.
 
Adam na Eva hawakuwa wanadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu, ila ni wanadamu wa kwanza kuumbwa katika bustani ya Edeni. Walikuwa ni aina mpya kabisa na Mungu akawatenga waishi katka bustani ya Edeni maisha yao yote. Ila nje mbali na bustani kulikuwepo binadamu wengine kabisa wakiishi. Baada ya kuasi na kufukuzwa bustanini ndo wakaja kuishi nje ya bustani ambapo pia watu wengine walkuwepo wakiishi kabla yao. Na hao watu waloumbwa mapema walokuwa wanaishi mbali na bistani walikuwa weusi kumbe ndo waafrika.
 
Unataka kukubali eti walifanya mapenzi na dada zao, yaan ndugu kwa ndugu walioana? Nakama ni ndiyo ,walifanya hivyo kwa amri ya nani?
 
Umetoa wap hii!?😂😂😂😂
 
Kwanini sio mtoto wa Adam
Kwa sababu Kaini ni mtoto wa Joka {Serpent} joka hakuwa kiumbe kama viumbe wengine ila alikuwa Mwanadamu na Malaika wa mungu kabla ya kuasi.
 
Ndugu, Ukitaka kuchuma dhambi we endela kuihoji biblia kwenye masuala ya kiutata kwa uwezo wa kibinadamu. Tafsiri ya Biblia ni kitu kizito mno - masuala mengine kwenye biblia unahitaji Roho mtakatifu kupata ufunuo !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…