comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Mahakama kuu nchini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majaji kwani 69 waliopo kwa sasa bado hawakidhi utendaji kazi wa kila siku wa mahakama Kuu na kufanya msongamano mkubwa wa majalada na kufikia hatua ya kila jaji kuwa majalada ya kesi zaidi ya 478, jambo linalowafanya washindwe kuzimaliza.
Hayo yalisemwa Arusha na Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafunzo ya majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji Wafawidhi na Majaji wa mahakama kuu waliokutana Jiji Arusha kutathimini utendaji kazi wa mahakama na kuboresha katika mwaka ujao.
Kaimu Jaji Mkuu alisema mapema mwaka 2014 kulikuwa na Majaji 90 kote nchini na ufanisi katika kazi ulikuwa mzuri na msongamano wa kesi mahakama kuu haukuwa mkubwa lakini majaji hao wengi wao walistaafu na kufikia idadi ya Majaji 75 mwaka 2015.
Jaji Mkuu alizungumzia namna ya ilivyojipanga kuhakikisha kila mkoa kote nchini unakuwa na mahakama Kuu na makama za mwanzo zinajengwa katika kila tarafa au kata lengo ni kutaka kuona msongamano wa kesi unamalizika kote nchini kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu.
Alisema fedha ziko kwani Benki ya Dunia na serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa mahakama zilizopo na kujengwa nyingine zenye hadhi.
Akizungumzia kupotea kwa majalada ya kesi za watu na kutotolewa kwa hukumu kwa wakati kuwa ni malalamiko makubwa ya wananchi dhidi ya mahakama kwani yanajenga hisia kuwa ili upate vitu hivyo kwa wakati ni lazima utoe rushwa.
Chanzo: Habari Leo