KAHAMA: Zaidi ya wafanyakazi 1,300 wakosa ajira baada ya mgodi wa Buzwagi kufungwa rasmi

Aiseeeeeeeeeeeè. Nilijua tu. Watatumia trick mpaka wafunge vyote. Wametuachia handaki na walishafaidi Shamba la bibi Tanzania.
 
Gram 1.35 kwa mwaka????????
Na kama ni kutoka 1.35 mpaka 1.00 kwanini wasipunguze wafanyakazi, expenditure wakaendelea na Kazi. Badala yake wanafunga rasmi.
Kutokana na nature ya shughuli ya uchimbaji wa madini labour intensive production technique haikwepeki, hauwezi ukapunguza idadi kubwa ya wafanyakazi na vibarua ghafla pasipo Kuathiri ufanisi. wamegundua solution ya tatizo lao sio idadi ya watumishi na vibarua bali investment policies za nchi yetu kwa sasa hazipo stable. Unawekeza leo lakini hujui kesho yako itakuaje, kila siku Mambo yanabadilika(hata katika forex, traders makini hudeal na pair ambazo trend yake inatabilika). Pia inawezekana wameona hiyo trill 1 waliyoiwekeza Tanzania kuna nchi nyingine ambapo inaweza ikawapa faida zaidi. Kumbuka wafanyabiashara ni profit oriented na sio service oriented.
 
Gram 1.35 kwa mwaka????????
Na kama ni kutoka 1.35 mpaka 1.00 kwanini wasipunguze wafanyakazi, expenditure wakaendelea na Kazi. Badala yake wanafunga rasmi.
Kwa tafsiri rahisi ni kuwa wanazalisha dhahabu isiyotosha kutengeneza hata Pete 1 ya gram 2 sasa sijui kwa muda gani
 
Dhahabu haizaani ikitoka ndo imeenda hairudi na hapo buzwagi imeisha watabaki kufanya nini lililopo ni kujipanga na mengine
 
Hii yote ni janja ya wawekezaji katika kuonyesha kuwa hatua ambazo serikali inachukua ni mbaya.
Wakoloni siku zote hawana nia njema na waafrika.

Let them go. tuliishi bila wawekezaji wakati wa Nyerere, madini hayakuoza, wakaja hawa wakatuibia mpaka tumekoma, kwani wakiondoka nani anapata hasara kubwa.

Ningependa JPM aendelee na msimamo huo huo
 
Unatumia magoti kufikiri au ubongo umeambiwa katika 1kg ya unga wa mawe zinatoka 1.3 gm za dhahabu unauliza habari za saa sekunde

We utakuwa punda kihongo wa ccm
Muulize mtoa mada kama haja edit baada ya Mimi kusema ulichosema wewe nafikiri kutumia magoti. Sidhan kama inasaidia chochote. Hiyo kilo ya mawe ndio naiona saivi baada ya mtoa mada Ku edit.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
KAHAMA: Zaidi ya wafanyakazi 1,300 wamekosa ajira, huku Kodi ya Sh. Bilioni 28 ikikosekana baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kufungwa rasmi.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mgodi huo unaomilikiwa na Acacia, umefungwa kwa kushindwa kuzaliwa kiwango cha madini hayo kilichotarajiwa.

Kufungwa kwa mgodi huo pia kumeikosesha Wilaya ya Kahama jumla ya Sh. Bilioni 1.7 zilizokuwa zikilipwa kila mwaka, ikiwa ni mrabaha.

Uongozi wa mgodi huo umeeleza kuwa uzalishaji wa dhahabu katika eneo la mgodi umeshuka kutoka gramu 1.35 hadi 1.00 (kwa kila kilo moja ya mchanga/mawe inayochimbwa) kwa mwaka jana. Mgodi huo ulianzishwa mwaka 2009 kwa mtaji wa wawekezaji unaokaribia Sh. Trilioni moja.

Tayari mgodi huo umeanza kuuza baadhi ya mali zake yakiwamo magari, mashine, majengo na vifaa vingine. Mnada mkubwa wa kuuza mali za mgodi huo utafanyika mapema mwezi Machi, 2018.
Hapo kwenye gm1 kwa kg1 ya mchanga sija kuelewa upo sahihi au umekosea?kama nikweli hiyo ni gold nyingi sana.rudia vizuri hyo tarifa siamini hapo.
 
Back
Top Bottom