Kahama yaangamia kwa Ukimwi

asante kwa maelezo haya lakini hujagusia suala la kinadada bikra kuwa nadra, vile vile kina kaka wasio na uzoefu.

Swali lako limejibika katika paragragh zifuatazo

Boyfriend & Girlfriend mahusiano yanaanza kabla hawajajua ulimwengu ukoje na bado wananukia maziwa ya utotoni, je hayo yatawafikisha kunako ndoa au ni mfumo wa kuiga tamaduni nyingine ambazo wazazi wetu hawakuzoea?

Eti siku hizi lazima watu wafanye majaribio kwanza, na wakijaribiana na kuchokana nini kitaendelea? Katika kujaribiana na kuzoeana hatima yake ni kutwishana mimba baadaye kuchokana hatima yake kila mmoja na njia yake huku hakuna uhakika kama walikuwa makini kujiangalia kiafya. Na mapokea kwa waafrika wengi msichana kisha zaa soko la kuolewa huwa adimu kidogo, bora ajenge njia ya kujitegemea mwenyewe.

Kwa mfumo wa bf na gf ubikira wa msichana na mvulana kutokuwa na mahusiano ya ngono yatakwepeka vipi? Unategemea kumpata msichana mwenye mahusiano ya ngono na vijana wangali teenage kubaki bikira? Unatazamia kijana aliyekwisha zoea kucheza na vimwana bila utaratibu mradi ua linachanua na kuvutia kila nyuki hutua na kufyonza utomvu wake atatulia ukubwani na mwandani wake?
 
Ukimwi upoooo,tuwe makini wana JF.tupime kwanza, tuwe waaminifu.
 
Na hivi vikao vya kujuana wanamitandao hapana budi kuwa makini maana kujuana isiwe nongwa ya kujuana kwa undani zaidi kwa wenye jinsia tofauti hadi kufikia hatua ya kuwa kitu kimoja bila tahadhari.
 

Tohara kwa wanaume pia ni muhimu huko maana jamaa hawatahiriwi kule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…