KAGERA: Mwanamke aokotwa akiwa amekatwa matiti

KAGERA: Mwanamke aokotwa akiwa amekatwa matiti

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,303
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi.jpg

KAMANDA WA POLISI MKOA WA KAGERA, AGUSTINE OLLOMI.


MWILI wa Betia Felix (18) mkazi wa Kijiji cha Nyakatete, wilayani Kyerwa mkoa wa Kagera, umeokotwa ukiwa umekatwa matiti na kufungwa kamba miguuni.

Marehemu huyo, alionekana kichakani Ijumaa iliyopita saa 4:00 asubuhi karibu na maeneo ya mashamba ya wanakijiji hicho baada ya ndugu kutokumwona nyumbani kwao kwa muda wa siku saba na kutoa taarifa ofisi za kijiiji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Josephat Mtayoba, alisema baada ya kupokea taarifa za binti huyo na kuwasiliana na ndugu wa marehemu walisema wakati akiondoka alikuwa anawasiliana na watu ambao ndugu zake hawakuwafahamu.

"Kwa kijiji hiki ni tukio la kwanza kushuhudia mauaji ya kushtua kama hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni kuweka na kuimarisha ulinzi shirikishi, "alisema Mtayoba.

Baba wa marehemu huyo Felix Gabriel , alisema binti yake, alitoka shambani akiwa na jembe na kuliweka nyumbani kisha kuondoka akiwa anaongea na simu, lakini hakufahamu alikuwa akiongea na nani.

Aidha alisema baada ya kukaa kwa muda mrefu akiwa haonekani nyumbani alidhani kuwa mwanae atakuwa ameolewa hivyo anasubiri kupokea mahari kutoka kwa wakwe.

“Aliondoka nyumbani tangu Januari 5, mwaka huu na mwili wake kuokotwa na mdogo wake mchunguzi Felix Ijumaa iliyopita Januari 12 mwaka huu,”alisema Gabriel.

"Nilivyoona anaondoka sikushtuka kwani nilijua atarudi na alivyokaa siku nyingi nilidhani atakuwa ameolewa nilijipanga kupokea mahari ya binti yangu, "alisema Gabriel kwa uchungu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi, alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta wahalifu hao na kwamba hakuna aliyenaswa.



Muungwana
 
eti alidhani kuwa mwanae itakuwa ameolewa ...alikaa nyumbani akisubiri mahali ...aiseeeee
 
eti alidhani kuwa mwanae itakuwa ameolewa ...alikaa nyumbani akisubiri mahali ...aiseeeee
Nikitu cha kawaida kabisa mkuu kwa maeneo ya vijijini mzazi/mlezi kuwa na fikra kama hizo kutokana na umri wa binti yao. Tatizo ni kutokuwa na taarifa sahihi za wapi anapoelekea binti kuanzisha familia na mwenzawake.
 
Nikitu cha kawaida kabisa mkuu kwa maeneo ya vijijini mzazi/mlezi kuwa na fikra kama hizo kutokana na umri wa binti yao. Tatizo ni kutokuwa na taarifa sahihi za wapi anapoelekea binti kuanzisha familia na mwenzawake.
hiyo sentensi yako ya mwisho ndio imenifnya mimi nipatwe namshangao..unaweza vipi kutokuwa nawasiwasi pindi mwanao anapokuwa nje ya nyumbani kwako..wakati bado hajajitoa chini ya himaya yako..yaani bado anaishi kwako..yaani unalala kbisa na usingizi wapata..baada ya kuanza kuhisi kuwa itakuwa amefikwa na jmbo baya ..wafikilia kuolewa tena..
neno nilikuwa nasubiri posa yake ..it means MZEE alikuwa anaweza Pesa tu .kuliko usalama wa bint yake
 
So sad! Haya maongezi mengine tuachane nayo Kwani Hakuna aliyekamilika! Cha muhimu serekali ifanye kazi yake!!!
 
Hawo ndobinadam kwa suala la ushirikina hawakuach kukufanyia RIP marehem
 
polisi kwa kushirikiana na TCRa wachunguze mawasiliano ya mwisho ya huyo marehemu... wanaweza kuwapata watuhumiwa...
 
Huyu itakua amebakwa,afu kingine hawa mabinti kufanyiwa haya sometime unakuta kamtenda mtu huko
 
Back
Top Bottom