Kagera: Mama wa Kabendera kuzikwa Kashenge Katoma Jumatatu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
dailynews_habarileo_20200104_5.jpg

Mwili wa marehemu Verediana Mujwahuzi mama mzazi wa Erick Kabendera utawasili Bukoba leo tayari mazishi yatakayofanyika kijiji cha Kashenge.

Mtoto wa marehemu Claudius Kabendera amesema kuwa, mwili wa marehemu mama yake utasafirishwa kutoka jijini Dar es salaam Januari 4 mwaka huu na kuhifadhiwa katika hospital ya mkoa wa Kagera, Bukoba
Amesema siku ya jumapili mwili wa marehemu Verediana utatolewa hospitalini na kupelekwa Rwamishenyi kwenye nyumba yake aliyokua anaishi wakati wa uhai wake na itafanyika Ibada fupi na mwili huo utalala katika nyumba hiyo hadi siku ya jumatatu.

Mwili huo utatolewa na kupelekwa katika kijiji cha Kashenge kata ya Katoma aneo ambalo ndipo mume wake alikuwa anaishi na ndipo alizikwa kipindi cha uhai wake na yeye atahifadhiwa katika nyumba yake ya milele.

Maandalizi yanaendelea ambapo wananchi walikuwa wakiendelea kuchimba kaburi huku vifaa mbalimbali kama matofari mchanga maji vikiwa tayari vimewekwa kwa ajili ya ujenzi wa kaburi hilo.

Hata hivyo mtoto huyo wa marehemu ameonyesha wasiwasi wake juu ya Kaka yake Erick Kabendera aliyepo mahabusu kama ataweza kuruhusiwa kumzika mama yake au la.
 
Kashenge Katoma ndicho nguzo ya ukoo wa Baihuzi tupu pale. naona barabara ya kwenda Kanyigo na Mugana! RIP mama yetu Verdiana
 
Nasubiri kuona ,,guest list” kwenye hayo mazishi, nategemea kuwaona Zito Kabwe, Mnyika, F.Karume, Mbowe, M. Sarungi, kwa kifupi nategemea kuona watu wengi sana kwenye hayo mazishi, kikosi chote cha Upinzani.
 
Back
Top Bottom