Huyo waziri wa PK aliyefukuzwa kazi alipewa haki ya msingi ya binadamu ya kujitetea. Ikiwa Mungu alimpatia Adamu, katika bustani Edeni, nafasi ya kujitetea kwa nini alikula matunda ya mti wa mema na mabaya, iweje PK asimpe nafasi ya kujitetea binadamu mwenzake? Ni kweli hatuwezi kuendelea kwa maneno lakini pia hatuwezi kuelewana pasipo kuzungumza maneno. Hakuna maendeleo pasipo maelewano. Maendeleo ni kwa ajili yetu iweje tufarakane kwa ajili ya maendeleo
Kagame ni dictator, na anataka Mawaziri wake wafanye kazi kama anavyotaka yeye.
Hii taarifa ni ya upande mmoja; hatujasikia kutoka kwa waziri aliyefukuzwa. Tusichukulie tu kuwa Waziri alikuwa na makosa kwa sababu Kagame kasema.
Inawezekana Waziri alikuwa sahihi, ila walitofautiana kimtizamo, na Kagame akamtimua kwa kuwa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho!