Kagame hails Magufuli for his tough measures to root out corruption and inefficiency at the Dar Port

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,297
15,583
Rais Paul Kagame ambaye miaka miwili iliyopita aliikosoa waziwazi serikali ya TZ kwa uzembe wa uendeshaji bandari amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi za kuimarisha utendaji katika bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda huitegemea kupitisha 70% ya mizigo yake.

Salaam za pongezi ziliwasilishwa jana ikulu na balozi wa Rwanda nchini Bw. Eugene Kaihyura....

JPM+IKulu+Rwanda+PHOTO.jpg

Rais John Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura (kushoto) baada ya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha Ikulu

Dar es Salaam. Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ya usafirishaji.

Rwanda, ambayo haijapakana na bahari, imekuwa ikiitegemea Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo yake.

Rais Kagame, ambaye miaka miwili ilkiyopita aliwahi kukosoa waziwazi utendaji wa Bandari akieleza kuwa angepewa taasisi hiyo angeweza kukusanya mapato ambayo yangeiendesha Tanzania, sasa anaonekana kuridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano za kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi kwenye bandari hiyo kongwe.

Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.

Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.

Mapema mwezi huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kushughulikia matatizo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

Pia, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe na kuagiza uchunguzi dhidi yao uanze mara moja, alivunja Bodi ya Wakurugenzi TPA.

Kushirikiana na ADB

Katika hatua nyingine, Rais amemhakikishia mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na kumhakikishia ushirikiano, Rais ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unaowezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa.

Kwa upande wake, Dk Kandiero alisema benki hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga Dola 2.3 bilioni kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Alisema ADB imelenga kujielekeza kutoa mikopo katika sekta ya nishati na usafiri.

Chanzo: Mwananchi

=====
Toka Daily News:

President Kagame congratulated President Magufuli in a special message delivered to President Magufuli by Rwanda Ambassador to Tanzania, Uegene Sagore Kayihura, at the State House in Dar es Salaam.

According to a State House statement, President Kagame said he was pleased by the measures taken by President Magufuli to crack down on tax evasion and inefficiency at the port, which handles over 70 per cent Rwandan cargo. Dar Port acts as a trade gateway for landlocked states such as Zambia, Rwanda, Malawi, Burundi and Uganda as well as the Eastern Region of the Democratic Republic of the Congo (DRC).

The World Bank said in a report mid-this year that inefficiency at the Dar es Salaam port cost Tanzanians and other East Africans dearly as they had to pay more for imported goods, including basic products such as crude oil, cement, fertiliser and medicine.

According to the report - in 2012, the total global welfare loss resulting from inefficiencies at the port was estimated to reach value of US$ 1.8 billion for the Tanzanian economy and 830 million US dollars for the neighbouring countries.

These losses were equivalent to approximately seven per cent of Tanzania?s annual GD, affecting a wide range of local consumers, businesses and government agencies. President Magufuli has launched a crackdown on tax evasion and inefficiency, dismissing the Director-General of the Tanzania Ports Authority(TPA) and some officials in the Transport Ministry over graft and tax evasion allegations at the port.

He has also suspended six high-ranking officials at the Tanzania Revenue Authority (TRA, including its commissioner-general, pending investigation into the allegations. The latest casualty in President Magufuli?s crackdown is the long-serving Director General of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), Dr Edward Hoseah, who was sacked last week due to the slow pace in the fight against graft.

The President?s Office said the dismissal of the PCCB chief came after two surprise visits to the Dar es Salaam Port by the Prime Minister, Mr Kassim Majaliwa. Police are investigating the disappearance of over 2,700 shipping containers from inland container depots that serve the port that were cleared without relevant taxes being paid.

In another development, President Magufuli has ensured Resident Representative of African Development Bank, Dr Tonia Kandiero that the fifth-phase government will continue to cooperate with the multilateral bank in implementing various development projects.

President Magufuli also called upon the bank to cut on long process in implementation of development projects and advised to expedite procedure to enable beginning of projects shortly after release of funds, according to State House statement.

Apart from congratulating President Magufuli for being elected as the fifth president of Tanzania, Dr Kandiero assured her host of continued cooperation with Tanzania in carrying out development projects.

She said ADB had set aside 2.3 billion US dollars for financing implementation of development projects in Tanzania. ADB would focus on issuing credits to energy and transport sectors, she noted.

President Magufuli congratulated ADB for choosing the two sectors which are vital in speeding up development and economic growth and stressed to look into how it would support construction of the central railway line to standard gauge.

A Chinese consortium had been awarded a contract to build a 2,561 km (1,536 miles) standard gauge railway connecting Dar es Salaam port to land-locked neighbours at a cost of $7.6 billion, former Transport Minister Samuel Sitta said in Parliament last May.

The consortium will provide 10 per cent of the funding for the project while financial adviser Rothschild is finalising procedures for financing of the project through banks, Sitta said.
 
Go Magufuli...go... We'll overtake Kenya just like Lowassa said.
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.
 
Lile jamaa la msoga liliiharibu sana hii nchi

Namhurumia tu Magufuli, atapiga kazi miaka 10 yake ikiisha inakuja tena 10 ya kutumbua tu! Nafikri huu utaratibu ufe kama kuna wa kununa na anune tu! Watu wa Pwani Hawawezi!! Hili taahira lilishangilia lilipokabidhiwa hazina iliyonona, lenyewe linakuja kuondoka hazina ikiwa tupu!!
 
Umenichekesha kweli, kwa hiyo kama nchi ni ndogo ndo hana uwezo wa kujua kama JK alizingua na sasa Magu anafanya vyema? Yaani unatumia hicho kigezo ku-rule out? Nenda kaangalie nchi za ulaya zinaukubwa gani wa eneo ukilinganisha na TZ kisha ufananishe Marekani na N.Korea
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.

Inaweza ikawa ni nchi ndogo indio lkn ikawa mfano bora wa nchi inayojitambua,yenye mikakati na mipango thabiti ya kujiletea maendeleo kuliko hili linchi letu likubwa la Tanzania. Fikiria makontena mamia kwa mamia yalikuwa hayalipiwi kodi;viongozi na watumishi wa serikali kufuja mabilioni ya pesa kila mwezi kwaajili ya safari za nje zisizokuwa na tija kwa taifa;rasilimali za taifa zikiporwa na wageni,mashirika na viwanda vya umma vikihujumiwa kwa makusudi kwaajili ya maslahi binafsi ya viongozi/watendaji wachache wasio waadilifu na waliokosa uzalendo.Huu ukubwa wa eneo tunaopenda kujisifia nao ni upuuzi mtupu ikiwa vichwa vyetu havifanyi kazi.
 
Namhurumia tu Magufuli, atapiga kazi miaka 10 yake ikiisha inakuja tena 10 ya kutumbua tu! Nafikri huu utaratibu ufe kama kuna wa kununa na anune tu! Watu wa Pwani Hawawezi!! Hili taahira lilishangilia lilipokabidhiwa hazina iliyonona, lenyewe linakuja kuondoka hazina ikiwa tupu!!

mbona unatutusi watu wa pwani ndugu????
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.

Nchi haipewi hadhi kwa kuangalia ukubwa, magufuli Yuko vizuri kuliko aliyemtangulia
 
Namhurumia tu Magufuli, atapiga kazi miaka 10 yake ikiisha inakuja tena 10 ya kutumbua tu! Nafikri huu utaratibu ufe kama kuna wa kununa na anune tu! Watu wa Pwani Hawawezi!! Hili taahira lilishangilia lilipokabidhiwa hazina iliyonona, lenyewe linakuja kuondoka hazina ikiwa tupu!!

Umenena pointi sana mkuu!
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.
Ahaha nakwambia watu kama nyie mtaugua moyo,kagame hupenda wachapa kazi hapendi wababaishaji ndio maana kampongeza magufuli na tanzania haiwezi kuendelea bila ushirikiano na nchi jirani,watu wababaishaji kama wewe ndiyo hamjui umuhimu wa Rwanda katika uchumi wa tanzania.
 
msogaaaaaaa mojaaaaaaaaa. si mlimtaka wenyewe?na amewatenda kweli>>>>mkome kuchagua rais kwa majaribio
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.

Kagame ni Rais makini sana, alitueleza ukweli na siku zote ukweli unauma, ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi, au unataka kusema mwenye kichwa kikubwa ndio mwenye akili nyingi ? Angalia exchange rate ya Pesa yetu kwa Pesa ya Rwanda, ipi ipo juu ndo ujue sasa, sisi badala ya kufanya maendeleo tulikuwa tunakula maisha...na ilibaki kidogo tu, uganda nao wangetuacha..hongera JPM.
 
nisemeni mimi muacheni magufuli afanye kazi-by JK dec 9 2015
hata mkinisema sigombei tena, kwa hiyo mnapoteza muda wenu by JK
hizi ni dalili za walioshindwa by JK
sasa mmechanganyikiwa, by JK

Lile jamaa la msoga liliiharibu sana hii nchi
 
Balozi ana PARA kama t.@ko..😷😨👌

👉🚶🚶🚶..
 
sidhani kama tunahitaji promo au neno lolote toka kwa kagame, hana hadhi ya kutuambia sisi maneno hayo. Rwanda ni nchi ndogo sana kwa kila kitu kuweza kupewa hata nafasi ya kuongea chochote juu ya Tanzania, angesubiri wakubwa na wenye hadhi zaidi yake waongee halafu yeye aongee mwishoniiii? hapo anajua alishakorika kwa kikwete hadi akasababisha uadui mkubwa kati ya nchi zetu, hadi leo hii hata kama hatutasema, ila mioyoni adui wa kwanza wa rwanda ni tanzania, so is vise versa....anaanza kujisafisha ili tuwe pamoja. unless wanaondoa kiburi cha kuwabagua wahutu, Rwanda will never be a true friend kwa tz. period.

Nikiambiwa nimwokoe mmoja kati ya Kagame na Kikwete namwokoa Kagame.
 
Namhurumia tu Magufuli, atapiga kazi miaka 10 yake ikiisha inakuja tena 10 ya kutumbua tu! Nafikri huu utaratibu ufe kama kuna wa kununa na anune tu! Watu wa Pwani Hawawezi!! Hili taahira lilishangilia lilipokabidhiwa hazina iliyonona, lenyewe linakuja kuondoka hazina ikiwa tupu!!

binti..chunga sana kauli zako
 
Back
Top Bottom