Financial Intelligence
Senior Member
- Sep 29, 2023
- 160
- 363
Kafulila anasema " Tatizo la ajira ni halisi lakini ni mtambukwa.
Kuna wakati sekta binafsi ilikuwa inatafuta watu wenye sifa fulani inakosa wakati sokoni kuna wasomi bila ajira.
Mtaala mpya chini ya Rais Samia utakabili changamoto hii ya mismatch kati ya mahitaji ya soko na wasomi tunaotengeneza"
Alisema David Kafulila, Mkurugenzi kituo cha UBIA( PPP) nchini katika kipindi cha DK 45 ITV,
Kafulila aliongeza kwa kusema kasi ya kuvuta mitaji ya sekta binafsi inapunguza tatizo la ajira.
Kwamba kati ya Mwaka 2021 na 2023, Idadi ya watalii imeongezeka mara mbili kutoka takribani watalii 900,000..mpaka watalii 1,800,000.
Mapato ya utalii yameongezeka karibu mara tatu zaidi kutoka dola 1.3bn mpaka dola 3.3bn.
Hii inathibitisha sio tu ongezeko chanya la watalii bali pia ubora wa watalii wanaingia nchini.
Ndio maana idadi imeongezeka mara mbili wakati mapato yameongezeka karibu mara tatu zaidi.
Nikweli changamoto ya ajira ni kubwa lakini nikweli pia Serikali inafungua uchumi kupunguza makali.
Takwimu leo zinaonesha kwamba idadi ya mobile bank accounts zimeongezeka kutoka 32m mwaka 2021 mpaka 52m mwaka 2023.
Watu wanaweza kubishana kuhusu ongezeko hili lakini kusema kwamba namba hizi hazimaanishi juhudi yoyote ya Serikali ya Samia Suluhu Hasssan ni uonevu, sio haki.
Namba hizi zinaonesha kuna kazi imefanyika kuongeza shughuli za watu na hivyo mzunguko wa pesa umeongezeka na ajira zimeongezeka."
Amesema David Zacharia Kafulila Mkurugenzi Mkuu wa Ubia nchini PPP.